Wabongo wengi wanaoishi Marekani wana maisha magumu tofauti na wale wanaoishi nchi za Scandinavian

Ananipenda huyo wala usihofu.
Si unaona nilikua nimetulia zangu kanifata mwenyewe?
Na unajua nini?
Ukiona ID yeyote inanitukana kaa nayo mbali,ni ya tapeli.Hapo atanivizia na Id nyingine sehemu nyingine anitukane
Kumbe?!!! Basi limeisha hilo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nchi za Scandianvia unabebwa sana na serikali ukiwa hujiwezi kiuchumi tofauti na USA. Lakn hakuna maendeleo yoyote ya maana utayapata zaidi ya kula kulala. Hizi nchi gharama za maisha zipo juu mno kuanzia kodi ya nyumba, kodi ya makato kwenye mshahara, nguo, vyakula, usafiri, starehe. Kila kitu ni super expensive. Kama unalipwa mshahara wote utaishia kwenye kulipia bills
 
Imeandikwa wapi kwamba wanaoishi ulaya au marekani wanastahili mafanikio zaidi ya sie tuliopo africa/nyumbani, maisha ni kumtanguliza Mungu na kupambana mafanikio yatakuja tu hata ukiwa somalia
 
Maskini wanazidi kuongeza huko Marekani 😁😁😁

View: https://twitter.com/BusInsiderSSA/status/1714995715590463908?t=MtOo5D9gzFnbtzXE9nQ6rA&s=19
 
Issue ni kupata kazi za kitaaluma ni rahisi zaidi Europe. Na ukiwa na taaluma na ukijua lugha, kufeli huku ni uzembe wako.
 

Bora ukae kimya tu. jiulize swali moja tu, kwanini marekani kuna wageni wengi, kwanini Marekani ni ndoto ya wengi, kwanini balozi zinajaa watu kuomba visa. hilo tu linatosha
 
Kuna ukweli kiasi fulani. Wengi wa Wanaoishi Marekani hata kama wana hela kuna style fulani ya maisha inakuwa sio sawa. Uvaaji na mwonekano unakuwa kama wa kihuni huni. Lakini kama walivyotangulia kusema wanaJF wengine ni kuwa hakuna sehemu rahisi duniani kwenye kutafuta hela. Kuna watu wako Kolwezi, Kasumbalesa, Sumbawanga na sehemu zingine za chaka wana hela kuliko hata hao wa Germany.
 
Bora ukae kimya tu. jiulize swali moja tu, kwanini marekani kuna wageni wengi, kwanini Marekani ni ndoto ya wengi, kwanini balozi zinajaa watu kuomba visa. hilo tu linatosha
Hio ilikuwa zamani ni sawa sawa useme kuwa ni rahisi kutoboa Afrika ya kusini kuliko Botswana kwa mwaka huu wa 2023. Kama haujatembea hauwezi kujua.
 
Hio ilikuwa zamani ni sawa sawa useme kuwa ni rahisi kutoboa Afrika ya kusini kuliko Botswana kwa mwaka huu wa 2023. Kama haujatembea hauwezi kujua.

Mimi naishi Marekani ni marafiki canada Australia na baadhi ya nchi za Euro, kwaiyo tuna share taarifa.
Marekani ni sehemu sahihi kwa mtafutaji
 
Mimi naishi Marekani ni marafiki canada Australia na baadhi ya nchi za Euro, kwaiyo tuna share taarifa.
Marekani ni sehemu sahihi kwa mtafutaji
Mimi nipo ujerumani kama hauna taaluma Marekani pako poa lakini kama una taaluma Ujerumani papo poa sana. Changamoto kubwa ni lUGha lakini ukishaijua mambo yapo poa. Kwa mtu aliyepo marekani anajua kuwa marekani haifikii europe kwa maslahi ya kazi za kitaaluma. I doubt that you are currently in US, labda kama ulikuwa unaishi huko zamani.
 

Kuongea kwa maneno hatuwezi kukuelewa

Sema hivi, kupitia chanzo fulani, Ujerumani ndio nchi nzuri kwa wafanyakazi wenye taalum. alafu fanya na kutupia na kapicha basi.

Inaeleweka kwamba Marekani ndio nchi ya kwanza kimalipo kwa wafanyakazi, ujerumani hata kwenye top 5 countries huwa haipo.
 
kama unabeba box Marekani utapata hela kuliko Ujerumani lakini kama una taaluma ujerumani pako poa sana. Inaonekana haupo Marekani na unafuatilia sana data za internet. USA is over rated na mtu mwenye first hand experience knows that. Wewe leta ushahidi upo Marekani na mimi nitaleta wangu kuwa nipo Ujerumani.
 

Ningekunyamanzia ingekuwa bora zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…