Iwapo tutafanya utafiti asilimia kubwa sana ya watu Duniani,
si Tanzania pekee Duniani kote, ndio ni Dunia yote kabisa wangependa kuishi/kwenda America na kwa sababu za msingi kabisa na zinazoweza kukubalika kwa yyote anaejielewa.
Lakini shida ni kuwa; America si ya kila mtu (Te hee 😀 )
Kuna ambae yupo nyumbani Bongo ama kwingineko,
Hana chochote, hana taarifa sahihi na za kweli, na hana uwezo wa kuweza kwenda America,
Mbung'o huyu ni Bendera fuata upepo lakini ataponda nae kwa kusikiatu pasi na kutafiti.
Lakini kuna ambae yupo nje ya Bongo kanasa sehemu (Ng'ambo ya mauchochoroni) anatamani sana sana angeweza kwenda America lakini nae hawezi yaani kafika na kurudi Bongo hawezi(mazingira yanambana) inaweza kuwa Kisheria au tena Kiuchumi. Afanyeje? Ataponda.
Vilevile kuna mwenzangu na mie ambae 'kaharibu' aidha 'kadunda' mara kadhaa alipoomba Visa ya America,
au tena alikuwepo huko America lakini akafurushwa kwa kukosa uhalali wa kuwepo huko yaani America haimtaki.
Huyu nae atajaribu kusema kaiona America na haipendi America kwa Riwaya na Makala juu,
Ilimradi tu aponde.
Narudia tena Dunia yote inaiota America, America, America.
Lakini America SIO ya kila mtu.
Hata hivyo, kama inavyoweza kuwa sehemu yoyote ile nyingine Duniani,
Hakuna mahali panapokosekana changamoto za hapa na pale lakini kwa ushahidi na taarifa za uhakika hivi tunavyoongea hakuna wa kuifikia America kwa uhakika ya kupiga hatua za kustaajabisha kimaendeleo kwa Wahamiaji.
Swala la msingi zaidi;
Una nini mkononi (unapeleka nini America) na umejiandaaje kuelekea huko kwa maana ya u-me-ji-pa-nga-je?
Sio kukurupuka.
Kingine huko kazikazi, watoto wa mama wakishindwa watatafuta visingizio.
Unataka ndio hivyo, hutaki ndio hivyo.
Chukua hiyo na tafakari.