Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Tayari kile kilichokuwa kinahisiwa kuja kutokea kimeanza kusikika maeneo ya Dodoma na Dar ambapo kundi la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa CHADEMA limejipanga kufungua kesi mbili mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wao wakati wowote wiki ijayo.
Kesi ya kwanza itakuwa ni kesi ya msingi, ambapo wataitaka mahakama ipitie upya hatua zote za CHADEMA zilizotumika kuwavua uanachama kama zilifuata kanuni na taratibu za katiba ya CHADEMA.
Kesi ya pili ni kuweka zuio la mahakama ili kutaka uamuzi wa kuvuliwa uanachama usitekelezwe popote kwanza, ili kupisha shauri la msingi kusikilizwa kwanza.
Tayari vigogo kadhaa wa CCM kisiri wanahusishwa katika kutoa miongozo na kufanikisha mkakati huo. Ofisi ya spika wa bunge nayo inatajwa kuwa inahusika katika kuratibu zoezi hili, na inategemewa kuwa jumatatu ijayo Spika atazungumza bungeni kubariki wabunge wa covid 19 kuendelea kukaa bungeni kwa mtindo wa kuchelewesha (delay tactic). Kauli kama hii inategemewa kutolewa na Spika, "tayari nimepokea barua rasmi kutoka CHADEMA lakini kuna mambo kadhaa yanamchanganyiko hivyo ningehitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuchukua uamuzi, hivyo nitamwandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA ili kuomba ufafanuzi wa barua yake na baada ya hapo ofisi ya spika itakaa upya ili kupitia maudhui ya barua hiyo na kuamua, hivyo basi wabunge wale 19 wataendelea kuwepo bungeni"
Habari za ndani ya Chadema zinasema kuwa uongozi wa chama hicho unazo hizo habari na mawakili wa Chama hicho wako tayari standby wakati wowote kukabiliana na kesi hizo mara tu zitakapofunguliwa.