Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu

Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu

Athari za ujinga huu ndio zinammaliza Samia katika juhudi zake za kuleta maridhiano na Chadema.
Anajivua joho mwenyewe na kukaa bila nguo

Samia amegeuka Jaji? Wapi na wapi! Ngoja waende mahakamani ili tue tujue nani mkweli!
 
Katiba ya chama ya chadema inasema kuwa ,ukikipeleka chana chako mahakamani tayari umejivua ubunge automatic...!

Sasa hao kina mdee wakikipeleka chama Chao mahakami watakuwa wamejivua ubunge moja kwa moja bila kupepesa macho ...
 
Tayari kile kilichokuwa kinahisiwa kuja kutokea kimeanza kusikika maeneo ya Dodoma na Dar ambapo kundi la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa CHADEMA limejipanga kufungua kesi mbili mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wao wakati wowote wiki ijayo.

Kesi ya kwanza itakuwa ni kesi ya msingi, ambapo wataitaka mahakama ipitie upya hatua zote za CHADEMA zilizotumika kuwavua uanachama kama zilifuata kanuni na taratibu za katiba ya CHADEMA.

Kesi ya pili ni kuweka zuio la mahakama ili kutaka uamuzi wa kuvuliwa uanachama usitekelezwe popote kwanza, ili kupisha shauri la msingi kusikilizwa kwanza.

Tayari vigogo kadhaa wa CCM kisiri wanahusishwa katika kutoa miongozo na kufanikisha mkakati huo. Ofisi ya spika wa bunge nayo inatajwa kuwa inahusika katika kuratibu zoezi hili, na inategemewa kuwa jumatatu ijayo Spika atazungumza bungeni kubariki wabunge wa covid 19 kuendelea kukaa bungeni kwa mtindo wa kuchelewesha (delay tactic). Kauli kama hii inategemewa kutolewa na Spika, "tayari nimepokea barua rasmi kutoka CHADEMA lakini kuna mambo kadhaa yanamchanganyiko hivyo ningehitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuchukua uamuzi, hivyo nitamwandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA ili kuomba ufafanuzi wa barua yake na baada ya hapo ofisi ya spika itakaa upya ili kupitia maudhui ya barua hiyo na kuamua, hivyo basi wabunge wale 19 wataendelea kuwepo bungeni"

Habari za ndani ya Chadema zinasema kuwa uongozi wa chama hicho unazo hizo habari na mawakili wa Chama hicho wako tayari standby wakati wowote kukabiliana na kesi hizo mara tu zitakapofunguliwa.
Kwa hiyo Mh.Spika anabariki matumizi mabaya ya pesa za umma?
 
Acha porojo,hujui kuwa Halima ni Mwanasheria kitaaluma?

Unadhani hajui jinsi ya kuulinda ubunge wake?

Kama mlimfukuza kihuni kama alivyosema Mahakama itamoa haki hake

Uanasheria wa Halima kwa sasa ni ceremonial tu, hajawahi kuufanyia kazi popote. Ametoka chuo na kuwa mwanasiasa, hapo alipo kichwa chake kimejaa mambo ya siasa na hana uwezo wa kudeliver chochote kwenye uga wa kisheria.
 
Mahakama ndicho chombo pekee cha utoaji haki ndani ya JMT.
It's very unfortunately katiba ya Chadema, haikitambui hilo!.
P
Kwa hiyo na wewe P ni muumini wa ubadhirifu wa mali za umma?

Ni kwa nini sasa Mzee Mdee asihamie tu CCM na kuachana na CHADEMA.Katika hili suala la Mdee kufukuzwa haki imeonekana kutendeka kwa maana alighushi nyaraka na chama chake hakimtambui.Iwapo CCM wanathamini mchango wa MDEE bado ana nafasi ya kupewa ubunge wa kuteuliwa.
 
Mahakama ndicho chombo pekee cha utoaji haki ndani ya JMT.
It's very unfortunately katiba ya Chadema, haikitambui hilo!.
P

Ww na Halima Mdee ni wanasheria wa nadharia hamjawahi kufanya shughuli yoyote ya kisheria nje ya kile mlichokariri mlipokuwa mnasoma. Mahakama ni chombo cha kutoa haki, hivyo ndio inavyotakiwa iwe, lakini sio ilivyo, na katiba ya cdm ina utaratibu kama ilivyo shughuli za soka ambazo hazipelekwi mahakamani. Ila hata kama katiba ya cdm ingekuwa inataja kwenda mahakamani, bado mahakamani zetu zimethibitika sio sehemu unayoweza kutarajia kupata haki hasa unapokuwa mpinzani.

Haya tuna ushahidi nayo, na aina ya hukumu zilizotolewa kwa kutii maagizo ya viongozi waandamizi wa ccm kwa kofia zao za serikalini. Ni mwendawazimu tu anaweza kuamini kupata haki kwenye mahakama zetu, hasa unapokuwa mpinzani tena kwa kesi inayoihusha serikali na makandokando yake. Isitoshe mahakama zetu ni sehemu unayoweza kuona bila kupata shaka udhaifu wa utendaji wa taasisi zetu za umma. Nenda magereza kulivyojaa watu wenye kesi zilizoshindwa kuamuliwa kwa haki. Kwahiyo itaje mahakama kama sehemu ya kubeba frustration zako, lakini sio sehemu yenye weledi kama unavyohubiri hapa.
 
Kwa hiyo na wewe P ni muumini wa ubadhirifu wa mali za umma?

Ni kwa nini sasa Mzee Mdee asihamie tu CCM na kuachana na CHADEMA.Kati hili suala la Mdee kufukuzwa haki imeonekana kutendeka kwa maana alighushi nyaraka na chama chake hakimtambui.Iwapo CCM wanathamini mchango wa MDEE bado ana nafasi ya kupewa ubunge wa kuteuliwa.

Hilo suala la akina Mdee wala halimuumizi Paskali, yeye anaumizwa na maamuzi ya cdm, kwani hayaendi sawa na matamanio yake. Kwa ujumla cdm inamtesa sana Paskali.
 
Tayari kile kilichokuwa kinahisiwa kuja kutokea kimeanza kusikika maeneo ya Dodoma na Dar ambapo kundi la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa CHADEMA limejipanga kufungua kesi mbili mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wao wakati wowote wiki ijayo.

Kesi ya kwanza itakuwa ni kesi ya msingi, ambapo wataitaka mahakama ipitie upya hatua zote za CHADEMA zilizotumika kuwavua uanachama kama zilifuata kanuni na taratibu za katiba ya CHADEMA.

Kesi ya pili ni kuweka zuio la mahakama ili kutaka uamuzi wa kuvuliwa uanachama usitekelezwe popote kwanza, ili kupisha shauri la msingi kusikilizwa kwanza.

Tayari vigogo kadhaa wa CCM kisiri wanahusishwa katika kutoa miongozo na kufanikisha mkakati huo. Ofisi ya spika wa bunge nayo inatajwa kuwa inahusika katika kuratibu zoezi hili, na inategemewa kuwa jumatatu ijayo Spika atazungumza bungeni kubariki wabunge wa covid 19 kuendelea kukaa bungeni kwa mtindo wa kuchelewesha (delay tactic). Kauli kama hii inategemewa kutolewa na Spika, "tayari nimepokea barua rasmi kutoka CHADEMA lakini kuna mambo kadhaa yanamchanganyiko hivyo ningehitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuchukua uamuzi, hivyo nitamwandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA ili kuomba ufafanuzi wa barua yake na baada ya hapo ofisi ya spika itakaa upya ili kupitia maudhui ya barua hiyo na kuamua, hivyo basi wabunge wale 19 wataendelea kuwepo bungeni"

Habari za ndani ya Chadema zinasema kuwa uongozi wa chama hicho unazo hizo habari na mawakili wa Chama hicho wako tayari standby wakati wowote kukabiliana na kesi hizo mara tu zitakapofunguliwa.
Habari za ndani ya Chadema zinasema kuwa uongozi wa chama hicho unazo hizo habari na mawakili wa Chama hicho wako tayari standby wakati wowote kukabiliana na kesi hizo mara tu zitakapofunguliwa.[emoji1534][emoji1545]
 
Hilo suala la akina Mdee wala halimuumizi Paskali, yeye anaumizwa na maamuzi ya cdm, kwani hayaendi sawa na matamanio yake. Kwa ujumla cdm inamtesa sana Paskali.
Basi akafungue kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraa kuu la chadema hahaha
 
Hivi kwani kuna umuhimu wowote kuitwa kwa jina la covid 19?
Hata kama inatakiwa kutajwa kwa lugha yenye kuwaudhi lakini sijaona mantiki ya kutaja covid 19.
 
CCM ni mabingwa wa propaganda, figisu na fitna. Wamemtuliza mwenyekiti na kahawa ikulu, nyumbu kama kawaida wakashangilia wakidhani wanashinda, watakuja kupigwa na kitu kizito utosini na lawama zitaanza kurudi.
 
CCM wanajimaliza wenyewe.
CCM hawajimalizi,ila wanammalaza Hangaya.Huwezi kusema maridhiano huku mambo yakuwagawa watanzania yakiendelea.
Huo mtego mbaya sana kwa upande mmoja,wanaogopa wakiwatimua tu watasema nani alifoji nyaraka.
 
Ni mwendawazimu pekee ambaye anaweza kwenda mahakamani kwaajili ya kugomea kufukuzwa au kusimamishwa uwanachama wa chama cha siasa.

Hakuna mahakama ambayo ina uwezo wa kumrudishia mtu uwanachama. Mamlaka za juu kabisa za uamuzi juu ya uwanachama huwa zipo ndani ya chama husika, siyo mahakamani.
Tz itawezekana CDM a ccm mnajuana nyinyi
 
Back
Top Bottom