Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu

Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu

Ni mwendawazimu pekee ambaye anaweza kwenda mahakamani kwaajili ya kugomea kufukuzwa au kusimamishwa uwanachama wa chama cha siasa.

Hakuna mahakama ambayo ina uwezo wa kumrudishia mtu uwanachama. Mamlaka za juu kabisa za uamuzi juu ya uwanachama huwa zipo ndani ya chama husika, siyo mahakamani.
Wewe ndio mbumbumbu, mahakama ipo popote na kazi yake ni kutafsiri sheria. Mdee na wenzake watakuwa wabunge wa mahakama na huyo joyce wenu aliyehongwa chama na mwenyekiti haendi bungeni.
 
Chadema kwa sasa mnacheza mziki wa ccm bila wenyewe kujua, kwasasa mmeacha kutetea wananchi mnatetea uamuzi wa kihuni wa mwenyekiti na baraza lake, mpo busy usiku kucha kudeal na hao covid 19 haliyakuwa mmeshawafukuza.

Maamuzi yeyote watakayochukua ni haki yao kama ninyi mlivyopewa haki ya kuwafukuza , acheni wasiwasi .
 
Mahakama ndicho chombo pekee cha utoaji haki ndani ya JMT.
It's very unfortunately katiba ya Chadema, haikitambui hilo!.
P
Chadema wanatambua kwamba mahakama ndo chombo pekee cha utoaji haki ndani ya JMT ila wameamua kufanya mumbo kihuni kihuni hatari.
Duh!
 
Kuna popote nimesema mimi kuwa nina akili kuliko mawakili wa Chadema?. Kusoma sheria sio kuwa Wakili. Kuna wanasheria kibao very bright and brilliant na hawasimami mahakamani!.

The best wa sheria Chadema ni Tundu Lissu, nimemtangulia miaka 2 pale Ilboru. LL.B yangu ni ya UDSM and it's (Hons)!. Sio kila aliyesoma sheria anafanya litigations.

Not always the best runners win the race, or the best fighters win the fight,
this time around, Chadema inakwenda kushikishwa adabu!. Haiwekani kila siku ifanye uhuni iachwe hivi hivi!. Mdee ni Kisiki cha mpingo!.
P


  1. Sakata la wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema ni Chadema wenyewe ndio walilianzisha kwa kugomea nafasi 18 za viti maalum walizopewa na NEC.
  2. Kwa msaada wa kiongozi mmoja mkubwa wa Chadema, Halima Mdee akiwa na Esta Bulaya, wakam convince umuhimu wa nafasi hizo kwa Chadema, akawakubalia kwa shurti wasimtaje.
  3. Halima akawaorganize Wanawake wa Chadema kwa kuanzia na waliokuwa wabunge, wengine wakikubali, wengine walikataa, kwa waliokubali wakaunda a coalition of the willing
  4. Barua bonafide genuine ikaandikwa, mnene akawasainia in return na yeye kuchomekea hapo kakidumu chake, yakaenda NEC, watu wa fursa wakaichangamkia fursa.
  5. Hivyo ni Chadema wenyewe ndio walilianzisha na hizi kati ni Chadema wenyewe wamelimaliza Kwa kikao cha Baraza Kuu kuyabariki maamuzi batili ya CC ya Chadema iliyo wafukuza.
  6. Walipopewa fursa ya kujitetea kwenye kikao cha Baraza Kuu, Halima Mdee akafanya kitendo kingine cha kishujaa kweli kweli kwa kutounguza picha ya Kilichopelekea kwa natumaini mnene yule angewaombea msamaha angalau wabaki wanachama wa kawaida!. Hili halikufanyika hivyo kilichofanywa na Baraza Kuu kuyabariki maamuzi batili ya CC ni uhuni.
  7. Sasa baada ya kuwatimua, ushauri wa bandiko hili bado uko valid, Chadema lazima sasa wautambue uchaguzi, wakubali matokeo, wafanye uteuzi wa wabunge wapya wakaapishwe maisha yaendelee.
  8. Kikwazo ni kimoja, utimuaji uliofanywa na CC ya Chadema ni batili, na baada ya kuonja fursa, jee watakubali matokeo, jee wataukubali ubatili huu au watakwenda mahakamani kutafuta haki yao?.
Jibu litapatikana on Monday.

This is my own recollection.
P.
Duh ndio wewe Pascal ninayekufahamu tangu 2012?
 
Hao wanawake wajinga wasipokuwa makini sasa wanaenda kuwa maadui wa taifa, hizo kodi za watanzania wanazokula bure huko bungeni wanajitafutia laana.
Acha kuweweseka, mmeshawafukuza hao wajinga sasa Taifa gani watakuwa maadui? Kama Taifa la ufipa sawa.
 
Ccm itagaramia mawakili wa hao wamama.

Ila mchuano utazidi ule wa kutafuta bingwa wa kombe la dunia
 
Tayari kile kilichokuwa kinahisiwa kuja kutokea kimeanza kusikika maeneo ya Dodoma na Dar ambapo kundi la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa CHADEMA limejipanga kufungua kesi mbili mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wao wakati wowote wiki ijayo.

Kesi ya kwanza itakuwa ni kesi ya msingi, ambapo wataitaka mahakama ipitie upya hatua zote za CHADEMA zilizotumika kuwavua uanachama kama zilifuata kanuni na taratibu za katiba ya CHADEMA.

Kesi ya pili ni kuweka zuio la mahakama ili kutaka uamuzi wa kuvuliwa uanachama usitekelezwe popote kwanza, ili kupisha shauri la msingi kusikilizwa kwanza.

Tayari vigogo kadhaa wa CCM kisiri wanahusishwa katika kutoa miongozo na kufanikisha mkakati huo. Ofisi ya spika wa bunge nayo inatajwa kuwa inahusika katika kuratibu zoezi hili, na inategemewa kuwa jumatatu ijayo Spika atazungumza bungeni kubariki wabunge wa covid 19 kuendelea kukaa bungeni kwa mtindo wa kuchelewesha (delay tactic). Kauli kama hii inategemewa kutolewa na Spika, "tayari nimepokea barua rasmi kutoka CHADEMA lakini kuna mambo kadhaa yanamchanganyiko hivyo ningehitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuchukua uamuzi, hivyo nitamwandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA ili kuomba ufafanuzi wa barua yake na baada ya hapo ofisi ya spika itakaa upya ili kupitia maudhui ya barua hiyo na kuamua, hivyo basi wabunge wale 19 wataendelea kuwepo bungeni"

Habari za ndani ya Chadema zinasema kuwa uongozi wa chama hicho unazo hizo habari na mawakili wa Chama hicho wako tayari standby wakati wowote kukabiliana na kesi hizo mara tu zitakapofunguliwa.
Msimtishe madame spika

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Paskali! Unamaanisha Mahakama haiwezi kupindua maamuzi ya chama?
Kikao cha Baraza Kuu ni kikao halali na maamuzi yamefikiwa kihalali, ila kilichofanywa na CC ya Chadema sio kikao halali na utimuaji ni utimuaji batili.

Ikithibitishwa kina Halima Mdee na kundi lake ni hawakutendewa haki, mahakama itasitisha uamuzi wa Baraza Kuu kuwatimua, na kuiamuru Chadema kufuata Katiba sheria taratibu na kanuni kuwatimua rasmi.

Kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mwanachama yoyote wa Chadema, akikishataki chama mahakamani, automatically anakuwa amejifuta uanachama wa Chadema.

Hivyo wakienda mahakamani, mahakama itaweka zuio Kwa Bunge kuwavua ubunge, hadi kesi ya msingi isikilizwe na kuamuliwa, that is unazungumzia 2023!.

Uamuzi ikitolewa Chadema iendeshe vikao halali vya mamlaka ya nidhamu na kikao cha Baraza Kuu Chadema kiitishwe tena, that will be 2024!. Uamuzi wa mwisho ukifikiwa in less than 12 months kabla ya uchaguzi unaofuata, kina Halima Mdee na kundi lake wanavuliwa ubunge, ila Chadema haipewi tena fursa ya kupeleka majina mengine!.
P
 
For the sake ya matumbo yao hao covid 19 wafungue tu hiyo kesi

Mtaani pagumu, haswa kama hujajipanga na una lifestyle ya namna fulani.

Petroli tu zaidi ya 3000!!

Hata ningekuwa mimi kama ingenihakikishia uwepo fwa ugali wangu or 2-3year ningefungua tu
 
Hapana , mimi sii muumini wa ubadhirifu, ni muumini wa fursa, zile nafasi 18 za viti maalum ni fursa, Chadema kama chama walizigomea, kina Halima Mdee wakazichangamkia.

Milango iko wazi muda muafaka ukifika watakuja na watapokelewa ila at the moment ni lazima kwanza tushikishane adabu, tusiekeze uhuni!.
P
KUB Mboye alifanya maongezi na Chief Hangaya kabla ya kuwatimua akina Mzee Mdee.Kwa kifupi ni kuwa CHADEMA itateua wabunge wengine kushika nafasi hizo.
Mambo yaliyofanya na shujaa wakati wa uchaguzi mkuu 2020 yamepuuzwa.
 
CCM hawajakoma tu kwenye kesi ya UGAIDI ya Mh. Mbowe eeee !! Hiki chama kina matatizo mengi mno.
 
Back
Top Bottom