Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu

Halima Mdee ajibu maswali yafuatayo.

1. Kikao gani cha Chadema kiliwateua kuwa wabunge wa viti maalum.

2. Kiongozi gani wa Chadema aliandika barua na kujaza fomu za kumtambulisha Halima na wenzake kwa Tume ya Uchaguzi kwamba wameteuliwa kuwa wabunge viti maalum.

Halima Mdee na wenzake wangekuwa WAKWELI basi utetezi wao ungejikita ktk vipengele hivyo muhimu hapo juu.
 
Safi sana tuli miss vituko vya mahakamani dah utamu unarudi huu ndugai atapanda siyo kizimbani,raha sana
 
Katika hao vigogo wa CCM wanaohusishwa na wao wamuhusishe Pius Msekwa katika hili
 
Tayari kile kilichokuwa kinahisiwa kuja kutokea kimeanza kusikika maeneo ya Dodoma na Dar ambapo kundi la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa CHADEMA limejipanga kufungua kesi mbili mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wao wakati wowote wiki ijayo.

Kesi ya kwanza itakuwa ni kesi ya msingi, ambapo wataitaka mahakama ipitie upya hatua zote za CHADEMA zilizotumika kuwavua uanachama kama zilifuata kanuni na taratibu za katiba ya CHADEMA.

Kesi ya pili ni kuweka zuio la mahakama ili kutaka uamuzi wa kuvuliwa uanachama usitekelezwe popote kwanza, ili kupisha shauri la msingi kusikilizwa kwanza.

Tayari vigogo kadhaa wa CCM kisiri wanahusishwa katika kutoa miongozo na kufanikisha mkakati huo. Ofisi ya spika wa bunge nayo inatajwa kuwa inahusika katika kuratibu zoezi hili, na inategemewa kuwa jumatatu ijayo Spika atazungumza bungeni kubariki wabunge wa covid 19 kuendelea kukaa bungeni kwa mtindo wa kuchelewesha (delay tactic). Kauli kama hii inategemewa kutolewa na Spika, "tayari nimepokea barua rasmi kutoka CHADEMA lakini kuna mambo kadhaa yanamchanganyiko hivyo ningehitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuchukua uamuzi, hivyo nitamwandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA ili kuomba ufafanuzi wa barua yake na baada ya hapo ofisi ya spika itakaa upya ili kupitia maudhui ya barua hiyo na kuamua, hivyo basi wabunge wale 19 wataendelea kuwepo bungeni"

Habari za ndani ya Chadema zinasema kuwa uongozi wa chama hicho unazo hizo habari na mawakili wa Chama hicho wako tayari standby wakati wowote kukabiliana na kesi hizo mara tu zitakapofunguliwa.
Sasa ofisi ya spika inahusika vipi?
 
Ni mwendawazimu pekee ambaye anaweza kwenda mahakamani kwaajili ya kugomea kufukuzwa au kusimamishwa uwanachama wa chama cha siasa.

Hakuna mahakama ambayo ina uwezo wa kumrudishia mtu uwanachama. Mamlaka za juu kabisa za uamuzi juu ya uwanachama huwa zipo ndani ya chama husika, siyo mahakamani.
Labda wanaona kwa sababu wapo kwenye msukumo wa watawala basi sheria kwao si kitu.
 
Tayari kile kilichokuwa kinahisiwa kuja kutokea kimeanza kusikika maeneo ya Dodoma na Dar ambapo kundi la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa CHADEMA limejipanga kufungua kesi mbili mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wao wakati wowote wiki ijayo.

Kesi ya kwanza itakuwa ni kesi ya msingi, ambapo wataitaka mahakama ipitie upya hatua zote za CHADEMA zilizotumika kuwavua uanachama kama zilifuata kanuni na taratibu za katiba ya CHADEMA.

Kesi ya pili ni kuweka zuio la mahakama ili kutaka uamuzi wa kuvuliwa uanachama usitekelezwe popote kwanza, ili kupisha shauri la msingi kusikilizwa kwanza.

Tayari vigogo kadhaa wa CCM kisiri wanahusishwa katika kutoa miongozo na kufanikisha mkakati huo. Ofisi ya spika wa bunge nayo inatajwa kuwa inahusika katika kuratibu zoezi hili, na inategemewa kuwa jumatatu ijayo Spika atazungumza bungeni kubariki wabunge wa covid 19 kuendelea kukaa bungeni kwa mtindo wa kuchelewesha (delay tactic). Kauli kama hii inategemewa kutolewa na Spika, "tayari nimepokea barua rasmi kutoka CHADEMA lakini kuna mambo kadhaa yanamchanganyiko hivyo ningehitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuchukua uamuzi, hivyo nitamwandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA ili kuomba ufafanuzi wa barua yake na baada ya hapo ofisi ya spika itakaa upya ili kupitia maudhui ya barua hiyo na kuamua, hivyo basi wabunge wale 19 wataendelea kuwepo bungeni"

Habari za ndani ya Chadema zinasema kuwa uongozi wa chama hicho unazo hizo habari na mawakili wa Chama hicho wako tayari standby wakati wowote kukabiliana na kesi hizo mara tu zitakapofunguliwa.
Yani mke kapata bwana mpya umemfumania, umeamua mfukuza kwa kumwandikia taraka, mke karudi kwa bwana uliyemfumania naye ili waishi wote wewe bado unachukia wakati talaka ushatoa na umewambia ndugu na jamaa na jamii jamani yule si mke wangu jamii umesikia

MY TAKE
Tulia akae na bwana mpya kama umalaya ni tabia yake atachepuka tena usilazimishe bwana mpya amkatae wakati yet ndio kamtoa kwako acha amstili
 
Tayari kile kilichokuwa kinahisiwa kuja kutokea kimeanza kusikika maeneo ya Dodoma na Dar ambapo kundi la wabunge 19 waliovuliwa uanachama wa CHADEMA limejipanga kufungua kesi mbili mahakama kuu kupinga kuvuliwa uanachama wao wakati wowote wiki ijayo.

Kesi ya kwanza itakuwa ni kesi ya msingi, ambapo wataitaka mahakama ipitie upya hatua zote za CHADEMA zilizotumika kuwavua uanachama kama zilifuata kanuni na taratibu za katiba ya CHADEMA.

Kesi ya pili ni kuweka zuio la mahakama ili kutaka uamuzi wa kuvuliwa uanachama usitekelezwe popote kwanza, ili kupisha shauri la msingi kusikilizwa kwanza.
Huu ni "ujambazi" tu unaofanywa mchana kweupe, kuendelea kuwaibia waTanzania kodi zao.

Hawa watu hawana la ziada tena.
Inatakiwa wajitokeze watu (raia) wapeleke shauri hili mahakamani kupinga hawa majambazi kuendelea kunyang'anya pesa ya waTanzania waliyoivujia jasho.
 
. Kauli kama hii inategemewa kutolewa na Spika, "tayari nimepokea barua rasmi kutoka CHADEMA lakini kuna mambo kadhaa yanamchanganyiko hivyo ningehitaji ufafanuzi zaidi kabla ya kuchukua uamuzi, hivyo nitamwandikia barua katibu mkuu wa CHADEMA ili kuomba ufafanuzi wa barua yake na baada ya hapo ofisi ya spika itakaa upya ili kupitia maudhui ya barua hiyo na kuamua, hivyo basi wabunge wale 19 wataendelea kuwepo bungeni"
Duh.

Watu nchi hii wamekuwa mafundi kwelikweli wa kuzua mambo.

Yaani hata yatakayofanyika/semwa siku kadhaa mbele, tayari yamekwishanaswa na kusambazwa kwa walaji?
 
Back
Top Bottom