Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Toka alipooletwa ki mchongo kuwa naibu Spika nilijua mavi matupu
 
Kwa nini usiwe mvumilivu kuvua mbivu na mbichi? Unadhani CC na Baraza kuu ni kikao cha watakatifu wasiokosea? Sasa ni muda wa Dalali DJ kuaibika
 
Mahakama chini ya maelekezo ya CCM.
 
 
Tanzania ina wasomi wa hovyo sana, kuna Mtu anajiita P atakuja na kukwambia mambo ya voices from within, tokea lini nchi ikaendeshwa na voices from within? au utasikia kila kitu kihahusisha KARMA- KARMA ni katiba ya nchi au chama? Alafu anajinasibu ni mawili nguli wa sheria- ni aibu kwa wasomi wa Tanzania.
 
Mahakama zetu zinajidhalilisha sana ndo maana haziaminiki rushwa mbele.
 
OK. Conjurers at work. Let's wait to see.
 
Maigizo hayataisha Tanzania CHADEMA wakomae wao Kama wao ova.
watakomaa nao vipi hapo mpaka kesi ya msingi itolewe maamuzi hivyo wataendelea kuwemo sana mpaka bunge la bajeti litakapohitimishwa.
 
Na mimi najua hivyohivyo..

Kwamba covid19 wamechelewa kwenda mahakamani.. walipaswa waende wakazuie baraza kuu lisijadili uanachama wao na sio sasa hivi wameshatimuliwa..

Lakini nimesikia mahala (za chini ya kapeti) kwamba hata hii kesi mpaka tunaingia siku ya leo ilikuwa haijafunguliwa labda iwe imefunguliwa sasa hivi.
 
Chadema wawaache tu 2025 wanamwagwa
Nadhani issue hii sio suala la 2025 au kesho ni muhimu nchi kuwa na sheria na sheria zisichague wakumuadhibu na yupi wakuachiwa, haki ni muhimu sana tu. Hawa wabunge wana haki kwenda mahakamani kama sheria zinaruhusu lakini swali kukiwa na swala mahakamani hata wakiwa mtumishi wa umma kashitakiwa na akaenda mahakamani je anaruhisiwa kuendelea kufanya kazi au inabidi aachie mpaka hukumu ikitoka? hapa ndio tunatakiwa kuwekwa sawa.

Kwa bunge au CCM wanamaslahi gani na hawa watu 19 kuna fadhila gani zinalipwa. Jambo baya ka kusikitisha ni kuona watunga sheria ndio wanapiga makofi mengi wakijuwa wazi sheria zinapindishwa.

Hii ni sad day katika sheria za nchi hii na zinapoteza credibility ya bunge na nchi. Je kesho mahakama ikisema wamevuliwa uanachama watarudisha malipo yote waliyolipwa wakiwa wabunge?

Kawaida inakuwa wanasimamishwa wakishinda kesi wanalipwa stahiki zao zote. Mimi sina imani na Chadema lakini nakuwa nasikitika nikiona tunakuwa na double standard ikija suala la haki.
 
🤔🤔🤔
 
Kuna mambo ukiwa na akili timamu unaona kabisa yanaweza kufanyika kwenye zile nchi za kijinga tu.kamwe huwezi kuyaona kwenye nchi zenye watu smart wanaojielewa.

Nasikitika kusema nchi nyingi za kundi la kwanza zinapatikana Afrika na hii ikiwa mojawapo.Nchi ambayo mwenye elimu na asiye na elimu wote wanakiwango sawa cha kufikiria.nchi ambayo mwenye madaraka na asiye na madaraka wana kiwango sawa cha maamuzi.Inasikitisha sana.
 
Naendelea kusimamia msimamo wangu wa kutoshangilia kiongozi yeyote anayeingia madarakani haraka haraka wakati sijui muelekeo wake.

Haya wale wa anaupiga mwingi mnasemaje hapa?.

Spika mliyekuwa mnashangilia baada ya Ndugai kupalazwa nje ya box mpo?.

Yaani hii nchi ni kutulia kama umewekwa kwenye jokofu each day!.
 
Mbona siku nyingi tu walishatoka chadema hao.
Nilishauri tangu mwanzo chadema waachane na hao akina mdee wasihangaike nao waendelee na maisha yao.
Lakini hapa shida ni UBUNGE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…