Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Watu wanashangaa nini, mbona hili lilitegemewa. CHADEMA wamefanya kosa kwa maana ya timing.
Na itawagharimu, Wana option moja, compromise na Hawa akina mama.
Hili litakua kosa jingine Kama like la kumzingua Dr. Slaa.
Sijui kwanini Chadema wanaendelea kufanya makosa Kama haya.
Wenye akili walijua itaishia hapa, wamama wale wanaimage ya Chadema unaanzaje kuwazingua?!
Mihemko kama sukuma gang wanavyohemka..

Pili mwenyekiti ni kitengo 😬😬
 
Kwani wakiingia humo bungeni,mkiwa humuwatambui mnaumia nini?
Achaneni nao endeleeni na mambo yenu

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
Wanaoumia ni wananchi wote wanaolipa kodi.kwasababu zinazotumika kuwalipa hao watu ni kodi tunazozilipa wananchi wote wazee kwa vijana.Chadema wanaweza wakaamua kukaa kimya kama hao watu uwepo wao haukihusishi chadema na chadema wakaendelea na mambo yao maana wao hawatoi ata shilingi kwenye kuwahudumia.ila je ni sawa mwananchi kugharamia maslahi ya mtu kwenye taasisi ya umma ambaye uwepo wake umekiuka taratibu.
 
Kuna mambo ukiwa na akili timamu unaona kabisa yanaweza kufanyika kwenye zile nchi za kijinga tu.kamwe huwezi kuyaona kwenye nchi zenye watu smart wanaojielewa.

Nasikitika kusema nchi nyingi za kundi la kwanza zinapatikana Afrika na hii ikiwa mojawapo.Nchi ambayo mwenye elimu na asiye na elimu wote wanakiwango sawa cha kufikiria.nchi ambayo mwenye madaraka na asiye na madaraka wana kiwango sawa cha maamuzi.Inasikitisha sana.
Zile Nchi za kijinga kama Nchi gani?
 
Kwenye kifo cha Magu ulikuwa unademka kwamba ni karma ila hapa hutaki kuamini kma ni karma?
Naomba unipe hiyo quote otherwise utakuwa unaongelea nonsense. Wewe kila habari ni Magufuli, nimeshamtaja hapa? Ungekuwa mama Janeth pengine ningekuelewa
 
Maadam jambo hili limefika mahakamani, ngoja mahakama itoe maamuzi ya mwisho wasije kusema wameonewa.

It is the last kicks of a dying horse.
Hii kesi itachukua miaka mitatu kuisha, ni hadi 2025 july ndio uamuzi utatolewa kuwa chadema wameshinda kesi na wakina halima kufukuzwa
 
CDM mliwatumia watoto wa watu kina mdee kuitukana serekali ya ccm kwa kipind lirefu Leo mnakuja kuwataka kuwafukuza Kam mbwa hpn huo ndio uhun
Mdee kanyaga twende
 
Wengi mpo gizani, kesi hii ikichukuwa muda mrefu ni miezi mitatu tu, muulize ofisa wa mahakama yeyote unayemjuwa.
Sawa mkuu, wewe upo kwenye mwanga. Kwamba figisu za nchi hii ni wewe tu unazijua!
 
Hivi haya maamuzi ya Bunge yana double standards?

Mbona wale wabunge wa CUF walipofukuzwa na Mwenyekiti wanayemtambua wao Lipumba, wabunge wale walifukuzwa mara moja na Bunge hilo??

Mbona Sofia Simba alipofukuzwa na CCM, ilitekelezwa mara moja na Bunge hilo hilo??

Iweje Hawa wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chadema, ambapo vikao vyote 2 vya juu vya chama hicho, kwa maana ya Kamati Kuu na Baraza Kuu, vikisema wazi kuwa hao wabunge, weshafukuzwa na chama chao cha Chadema, kuwepo na kigugumizi cha kuwatimua Bungeni??

Hivi huyo Spika anapata wapi "kiburi" hicho, wakati anajua wazi kuwa Katiba yetu ya Jamhuri, inatamka wazi kuwa kila Mbunge, ni LAZIMA atokane na chama cha siasa??

Hivi huyo Spika Tulia Ackson, haoni kuwa atakuwa anavunja Katiba ya nchi, kwa kuwakumbatia wabunge, ambao hawatokani na chama chochote cha siasa nchini??

Hivi huyo Spika wa Bunge, Tulia Ackson, ambaye ana Shahada ya PhD ya sheria, haoni namna anavyodhalilisha taaluma yake ya sheria, kwa ajili tu ya kuinufaisha CCM?[emoji3064]
Hao wengine unaowataja walienda mahakamani? au kwa kuwa katiba ya chadema haiitambui mahakama basi na nyie hamuitambui?
 
Unapaswa kujua tu kuwa hao wabunge bado wanahitajika huko.
Hiyo kesi yenyewe kuja kuisha 2025.
Wangekuwa hawaitajiki wangeshaondolewa faster tu, kama spika tu aliondolewa faster tu kwa hao Wala isingeshindikana
Mkuu Memento, kwaantiki hiyo unatuambia kuwa hawa ni muhimu sana zaidi ya Spika? Hata huyu aliyepo anaweza kuondolewa na Serikali faster?
 
Serikali inaendeshwa kihuni
CHADEMA, na hasa Mbowe, sasa ni lazima wajue kuwa hakuna kilichobadilika, ila namna tu ya utekelezaji wa hujuma ndiko kulikobadilika.
badala ya kuwaponda vichwa na kuwatupa gerezani, sasa wanaitwa ikulu na kupewa chai na lugha nyororo sana ya kuwatia usingizi.

Mbowe ni lazima aogope sana.
 
CHADEMA, na hasa Mbowe, sasa ni lazima wajue kuwa hakuna kilichobadilika, ila namna tu ya utekelezaji wa hujuma ndiko kulikobadilika.
badala ya kuwaponda vichwa na kuwatupa gerezani, sasa wanaitwa ikulu na kupewa chai na lugha nyororo sana ya kuwatia usingizi.

Mbowe ni lazima aogope sana.
Lissu alishasema Kuwa Chifu Hangaya hana nia ya maridhiano bali analazimishwa na mabeberu.
 
Maadam jambo hili limefika mahakamani, ngoja mahakama itoe maamuzi ya mwisho wasije kusema wameonewa.

It is the last kicks of a dying horse.
Na mahakama itakapoamua kuimaliza hii kesi 2025, sijui itakuwaje mkuu Quinine?
 
Maigizo hayataisha Tanzania CHADEMA wakomae wao Kama wao ova.
Kwamba BUNGE linasema kumfuta mwanachama Uanachama tufuate KATIBA ya Nchi na Si ya CHAMA tena? Ivi mnajua ni Kodi zetu mnapoteza?
 
Back
Top Bottom