Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Wabunge 19 Viti Maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama Kuu

Huwa najiuliza maswali mengi sipati majibu.. hivi CCM inafaidika vp na hao wabunge 19? Kwanini mnahubiri maridhiano wakati nyie hampo tayari? Mnaturudisha nyuma Sana. Achanane na siasa za kukomoana tusonge mbele.
Bunge letu linafuata sheria za jumuia ya madola la vyama vingi. Kama hawatokuwapo bungeni, tanzania itakuwa inakiuka taratibu hizo, na kutakuwa na athari
 
Eleza katiba imevunjwaje? Ibara au kifungu gani cha katiba?........Don't just speak out of nothing...
Kanuni za Chama

6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) (c) (d) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

Hapo tu kuna waliopewa taarifa kwa simu na bila kufafanuliwa makosa yao ili wapate muda wa kutoa utetezi.
Ukiendelea mbele...

6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.

6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au la.

Katika wote hakuna aliyepewa mashitaka kwa maandishi wala nafasi ya kutoa utetezi wala taarifa ya msingi ya mamlaka ya nidhamu. Mpaka hapo mwenendo mzima wa kuwafukuza uanachama ukawa batili.

Ukiwa na swali jingine uliza.
 
Usijifay
Mapambano ya riziki hayajawahi mepesi,nani anaweza kubali Mshahara wa zaidi ya milioni 10 umponyoke kirahisi🤣🤣🤣.Shida ya CDM hawapendi kuambiwa ukweli,Paskali alijaribu kuonesha upungufu wa uamuzi wa CC na Baraza kuu akashambuliwa!
Yeye Mbowe ana usafi gani wa kufukuza wasaliti wakati na yeye 2015 alikisaliti Chama kwa kumuweka Lowasa kuwa mgombea urais wakati walimuweka kwenye list of shame!🤣🤣🤣
Usijifanye mjanja ndugu. Sarakasi hizo zilitarajiwa. Wala suala hilo kuwa hivyo haina maana kuwa Chadema walikosea lolote katika kufikia maamuzi yao.
 
Let's assume kuwa hizi ni kanuni za chama cha siasa kiitwacho "CHADEMA" as far as COVID-19 MPs are concerned...
Kanuni za Chama

6.5.2 Kwa mujibu wa Ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:
(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) (c) (d) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu wa kifungu (a) na (b) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

Kama ndo hizi, then ziko well stipulated na zinaeleweka...
Hapo tu kuna waliopewa taarifa kwa simu na bila kufafanuliwa makosa yao ili wapate muda wa kutoa utetezi.
Ukiendelea mbele...

Wewe unayeandika haya unayathibitishaje? Is it just because umesikia wakisema/yakisemwa? Really?
6.5.6 Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

Likely walipewa. Sisi tunaamini walipewa kwa sbb msingi wa uendeshaji wa chama ni KATIBA na KANUNI za chama chao. Wewe kama unaamini hawakupewa, thibitisha sasa...!
6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.
Waliitwa kwenye CC. "Inasemekana" baadhi walitii na kwenda na "likely" walijitetea. some didn't obey the summon. Vivyo hivyo wote walikuwepo kwenye Baraza Kuu. Aidha walipewa nafasi ya kujijitea huku tukiona kwa macho yetu hatua kwa hatua..

Kwa tuliokuwepo kwenye kikao cha BK, M/kiti wa kikao was very fair enough kwa sababu alifanya yafuatayo:

1. Alisoma agenda kuwahusu. "RUFAA ZA WANACHAMA 19"..

2. Kisha akasoma hatua kwa hatua proceedings toka CC na maamuzi yaliyotolewa + utetezi wao..

3. Rufaa zao zikasomwa na sababu walizitumia kujitetea mbele ya BK ktk rufaa zao. Na kila mmoja akathibitisha juwa hayo ni maelezo yake..

4. Mjadala ukafanyika kwa baadhi ya wajumbe kuchangia hoja hiyo kwa uhuru kabisa kila mmoja aonavyo yeye..

5. Kabla ya maamuzi, M/Kiti wa kikao mara 3 akawapa nafasi ya kusema neno mbele ya wajumbe wa BK aidha wajitetee na kusema lolote wanaloona haliko sawa au kuomba msamaha. Hakuna aliyesimama kusema lolote..!

6. Baada ya hapo, kura za kuunga mkono au kuyakataa maamuzi ya CC ikapigwa. Majority ya wajumbe (95%) wakakubaliana na maamuzi ya CC..

## Unasemaje mpaka hapo..? Hii transparency bado una mashaka nayo tu?
6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kukata rufani au la.
Likely, ndivyo ilivyo...
Katika wote hakuna aliyepewa mashitaka kwa maandishi wala nafasi ya kutoa utetezi wala taarifa ya msingi ya mamlaka ya nidhamu. Mpaka hapo mwenendo mzima wa kuwafukuza uanachama ukawa batili.

Unathibitishaje haya? Au kwa sababu tu umeandika/umesema tu...?
Ukiwa na swali jingine uliza.
Maswali yamo ndani ya maelezo yangu. Yajibu kama unaweza...

Otherwise, kwa maoni yangu, wewe unaandika usichokijua. Hilo ndilo tatizo lako kubwa..!

Pole sana...
 
Hapa ndipo utaona ubaya wa rais kuwa mwenyekiti wa chama.

Rais angeweza kusema kirahisi kabisa kwamba yeye hahusiki na mambo ya muhimili wa bunge, muhimili unaongozwa na Spika.

Lakini, kama mwenyekiti wa chama, ameharibu kabisa utetezi huo.
 
Leo spika wa Bunge ameelezea sakata la wabunge 19 wa viti maalum CHADEMA waliofukuzwa na chama chao. Kwa ufupi, wabunge husika wamefungua kesi mahakamani kupinga maamuzi ya baraza kuu la CHADEMA na Bunge limesema halitaweza kutangaza viti hivyo kuwa wazi kuuheshimu muhimili mwenzake wa mahakama.

=====

Spika amesema taarifa walianza kuiona kwenye mitandao ya kijamii usiku wa tarehe 11 Mei kwamba baraza kuu la CHADEMA limeazimia kukubaliana na uamuzi wa kamati kuu ya CHADEMA kuwafukuza uanachama wabunge 19 kupitia chama hicho.

Tarehe 12 Mei kwa njia ya barua pepe, wabunge hao 19 walimfahamisha spika maamuzi yaliyofikiwa na baraza kuu kwamba si halali, yako kinyume na katiba ya Tanzania na hayakuzingatia haki ya msingi ya kuwasikiliza au kuwaruhusu kujitetea.

Wabunge hao 19 wa CHADEMA wamepeleka kesi mahakama kuu ya Tanzania kupinga uamuzi huo na mwenendo mzima wa maamuzi yaliyofanyika kupitia shauri namba 16 la mwaka 2022 dhidi ya baraza la wadhamini CHADEMA, tume ya Taifa ya uchaguzi na mwanasheia mkuu wa Serikali.

Pia Spika Tulia amesema Mei 12 saa 9:30 alasiri afisa wa CHADEMA alifika bungeni aliyejitambulisha kwa jina la Meshack alifika ofisi ya spika Dar kukabidhi barua kwa spika na aliambiwa asubiri kwani wakati wa Bunge maafisa wote wanakuwa Dodoma, akaondoka baada ya kufanya mawasiliano na viongozi wake.

Tarehe hiyo hiyo Bunge lilipokea barua pepe iliyosainiwa na katibu mkuu wa CHADEMA juu ya maamuzi ya kikao cha baraza kuu juu ya kukataliwa rufaa ya wanachama 19 wa Chadema.

Spika amesema tarehe 13 Mei, barua hiyo iliwasilishwa ofisini kwa Spika kwa mkono na naibu katibu mkuu wa CHADEMA, Singo Kigaila na baadae ikapokea barua hiyohiyo kwa DHL.

Spika amesema Mamlaka ya mwisho ya utoaji haki ni Mahakama katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo katika nchi yenye kuongozwa na sheria na kuheshimiana kati ya mhimili mmoja na mwingine, Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa Mahakama hivyo inalazimika kusubiri mpaka mahakama itapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo.

Spika amesema wabunge husika walimtaarifu mapema kabla hajapokea taarifa yoyote rasmi kutoka CHADEMA, hivyo analazimika kutotangaza nafasi za viti maalum 19 za CHADEMA ziko wazi hadi hapo mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi.

Spika amesema endapo kutakuwa na maswali, msemaji wa jambo husika ni Spika.

Wabunge wamegonga meza kwa wingi kupongeza maamuzi yaliyosomwa na Spika.

Pia, Soma;

=> Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

=> Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

=> Wabunge 19 kufungua kesi, vigogo CCM na ofisi ya Spika wahusishwa katika uratibu!
View attachment 2226708

R
 
Sasa subili bungeni, wanaondolewa kesho, labda Chadema wafanye uzembe tu wa kutopeleka maamuzi ya mahakama kuu usiku huu Dodoma na asubuhi kukabidhi kwa ofisi ya spika.
No sio cdm bali mwanasheria mkuu inapaswa kupeleka maamuzi ya mahakama.
Nimesikiliza press ya Kibatala
 
No sio cdm bali mwanasheria mkuu inapaswa kupeleka maamuzi ya mahakama.
Nimesikiliza press ya Kibatala

Hii Bongo yetu haina uhaba wa sarakasi. Kupata copy ya ruling yenyewe huenda isiwe leo wala kesho!
 
Back
Top Bottom