Wabunge CCM kulishana yamini... Lengo ni Mfumo wa Serikali TATU haupiti !!!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
Alhamisi, Januari 16, 2014 08:04 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

*Lengo ni kuhakikisha mfumo wa kuwa na Serikali Tatu haupiti

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewapanga wabunge na wawakilishi watakaokuwa wajumbe kwenye Bunge la Katiba kukataa pendekezo la Serikali Tatu.

Wameonya kuwa, mpango wa kuvunja Muungano wa Serikali mbili na kuunda tatu ni kinyume cha sera na misingi ya chama hicho pamoja na wosia wa waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai kwa sehemu kubwa wana-CCM hao wameonyesha dhamira ya kuweka msimamo wa pamoja kupinga muundo wa Serikali Tatu.

Vyanzo vya uhakika vimesema kuwa mjumbe mmoja ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) alisimama na kuwataka wanachama wenzao wenye fikara ya kutaka Serikali Tatu wasimame na kukieleza kikao manufaa yake, ili kuwashawishi kama ipo haja ya kuunga mkono.

Taarifa zimesema hakuna Mbunge wala Mwakilishi aliyesimama na kutaja faida ya Serikali Tatu na badala yake wote walionekana kuafiki muundo wa Serikali Mbili.

Wawakilishi watatu walisimama kuchangia mawazo yao wakiwemo Salum Turky, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Hamza Hassan Juma Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtupura na Mwakilishi wa Viti Maalum Ashama Bakari Makame.

Hamza alisema kabla ya kuafiki au kukataa ni vyema rasimu hiyo ikaletwa mbele ya wabunge na wawakilishi, ijadiliwe kifungu kwa kifungu na kuona kama muundo wa Serikali Tatu utakuwa na maslahi zaidi kwa Zanzibar au la kabla ya kuukataa au kukubali.

Akasema ipo haja na ulazima wa rasimu hiyo ya pili kujadiliwa na wawakilishi pamoja na wabunge ikiwamo kufanyiwa semina ili kujua kama mabadiliko hayo yana faida na yataweza kuheshimu na kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

“Niko tayari kuikataa kwa sababu za kisera ikiwa itakosa manufaa kwa Zanzibar, tunahitaji kujijenga kiuchumi na kukwamua wananchi wetu kutoka katika ukosefu wa ajira na kuimarisha huduma za jamii,” alinukuliwa.

Hata hivyo aliposimama Turky, alimtaka Mwenyekiti kuhakikisha mpango huo unawekewa kiapo, ili atakayekwenda kinyume adhurike na kupata laana kwa Mungu.

Turky alisema bila hivyo mapatano yao yatakuwa ni kazi bure, na kwamba mbele ya safari wanaweza kuzungukana na kujikuta mpango wa Serikali Tatu ukipita na kuyaweka rehani Mapinduzi ya Zanzibar.

“Tulishane yamini hapa hapa, atakae kwenda kinyume na Kitabu cha Quraan imdhuru na kupata laana, ndivyo walivyofanya hata wazee wetu wa ASP katika kusimamia na kufanikisha mambo ya msingi,” alisema Mwakilishi huyo wa Mpendae.

Ushauri wake uliungwa mkono na Mwakilishi wa Viti Maalum Asha Bakari Makame, aliyesema ni kweli kuna umuhimu wa jambo hilo kufanyika kabla ya usaliti haujapita miongoni mwao.

“Tusipofanya hivyo tutasalitiana wenyewe kwa wenyewe na kuwapa vicheko maadui wetu, ikiwa faida za Serikali Tatu hazioonekani, tusilitingishe Taifa, likitikisika na kupasuka hakuna wa kuliziba, sote tutaangamia na kutoweka,” alisema.

Wakati hilo likitokea katika kikao hicho cha wabunge na wawakilishi, Umoja wa Vijana wa UV-CCM umetoa msimamo wake mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kusema rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekosa mashiko na haikubaliki, kwani imegusa tunu za Taifa na kutaka kuleta mgawanyiko.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akifungua Mkutano Mkuu maalum wa Mkoa wa Magharibi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere huko Bububu, alisema atakuwa mtu wa mwisho kukubali na kuuafiki mfumo wa Serikali Tatu, akiamini mfumo huo umekosa uimara na umadhubuti.

Vuai alisema nje ya Muungano wa sasa anaamini hata Pemba na Unguja hazitakaa pamoja kama zilivyo, na huo utakuwa ni usaliti wa kuviza mawazo ya waasisi wa Muungano ambao waliuanzisha kwa nia njema iliyoliweka Taifa katika mikono salama kwa miaka 50 iliyopita.

Hata hivyo, Vuai alisema hatma ya kupita au kutopita kwa jambo hilo iko mikononi mwa wabunge na wawakilishi wa CCM ambao ni wengi, hivyo wana kila sababu ya kulipinga wazo hilo ambalo liko kinyumne na sera ya msingi ya CCM.

sura%20ya%20rai.jpg

Hivi hawa watu wapoje jamani? mbona kama kuna kulazimishana!!! Khaa utafikili habari za kutunga.
 
WABUNGE CCM KULISHANA YAMINI *Lengo ni kuhakikisha mfumo wa kuwa na Serikali Tatu haupiti

Hata hivyo, Vuai alisema hatma ya kupita au kutopita kwa jambo hilo iko mikononi mwa wabunge na wawakilishi wa CCM ambao ni wengi, hivyo wana kila sababu ya kulipinga wazo hilo ambalo liko kinyumne na sera ya msingi ya CCM. Chanzo; Gazeti la Rai
 
Hawa watakuwa wanafiki sana, si kila siku wanalalamika kuwa Tanganyika inawanyanyasa? Si wawe na Zanzibar huru sasa?
 
Hii katiba lazima iwe ya kiCCM CCM maana wai ndio wengi hatuwezi kuwalaumu kwa hilo Pengine hapa wapinzani walikosea kucheza karata zao pengine wangesubiri wakawa na wabunge angalau nusu ya wale wa sisiemu lakini wabunge wa sasa ni wachache sana na hawawezi kushindana na CCM ndo maana wameharibu mchakato toka mwanzo kabisa
 
What a bunch of backward thinking morons!Our Country is right on the collapsing state and CCM LUNATICS would rather jump off the cliff and kill themselves than avoiding such a suicide.What a bunch of lemmings!!!
 
WABUNGE CCM KULISHANA YAMINI *Lengo ni kuhakikisha mfumo wa kuwa na Serikali Tatu haupiti
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewapanga wabunge na wawakilishi watakaokuwa wajumbe kwenye Bunge la Katiba kukataa pendekezo la Serikali Tatu.

Wameonya kuwa, mpango wa kuvunja Muungano wa Serikali mbili na kuunda tatu ni kinyume cha sera na misingi ya chama hicho pamoja na wosia wa waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai kwa sehemu kubwa wana-CCM hao wameonyesha dhamira ya kuweka msimamo wa pamoja kupinga muundo wa Serikali Tatu.

Vyanzo vya uhakika vimesema kuwa mjumbe mmoja ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) alisimama na kuwataka wanachama wenzao wenye fikara ya kutaka Serikali Tatu wasimame na kukieleza kikao manufaa yake, ili kuwashawishi kama ipo haja ya kuunga mkono.

Taarifa zimesema hakuna Mbunge wala Mwakilishi aliyesimama na kutaja faida ya Serikali Tatu na badala yake wote walionekana kuafiki muundo wa Serikali Mbili.

Wawakilishi watatu walisimama kuchangia mawazo yao wakiwemo Salum Turky, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Hamza Hassan Juma Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtupura na Mwakilishi wa Viti Maalum Ashama Bakari Makame.

Hamza alisema kabla ya kuafiki au kukataa ni vyema rasimu hiyo ikaletwa mbele ya wabunge na wawakilishi, ijadiliwe kifungu kwa kifungu na kuona kama muundo wa Serikali Tatu utakuwa na maslahi zaidi kwa Zanzibar au la kabla ya kuukataa au kukubali.

Akasema ipo haja na ulazima wa rasimu hiyo ya pili kujadiliwa na wawakilishi pamoja na wabunge ikiwamo kufanyiwa semina ili kujua kama mabadiliko hayo yana faida na yataweza kuheshimu na kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

“Niko tayari kuikataa kwa sababu za kisera ikiwa itakosa manufaa kwa Zanzibar, tunahitaji kujijenga kiuchumi na kukwamua wananchi wetu kutoka katika ukosefu wa ajira na kuimarisha huduma za jamii,” alinukuliwa.

Hata hivyo aliposimama Turky, alimtaka Mwenyekiti kuhakikisha mpango huo unawekewa kiapo, ili atakayekwenda kinyume adhurike na kupata laana kwa Mungu.

Turky alisema bila hivyo mapatano yao yatakuwa ni kazi bure, na kwamba mbele ya safari wanaweza kuzungukana na kujikuta mpango wa Serikali Tatu ukipita na kuyaweka rehani Mapinduzi ya Zanzibar.

“Tulishane yamini hapa hapa, atakae kwenda kinyume na Kitabu cha Quraan imdhuru na kupata laana, ndivyo walivyofanya hata wazee wetu wa ASP katika kusimamia na kufanikisha mambo ya msingi,” alisema Mwakilishi huyo wa Mpendae.

Ushauri wake uliungwa mkono na Mwakilishi wa Viti Maalum Asha Bakari Makame, aliyesema ni kweli kuna umuhimu wa jambo hilo kufanyika kabla ya usaliti haujapita miongoni mwao.

“Tusipofanya hivyo tutasalitiana wenyewe kwa wenyewe na kuwapa vicheko maadui wetu, ikiwa faida za Serikali Tatu hazioonekani, tusilitingishe Taifa, likitikisika na kupasuka hakuna wa kuliziba, sote tutaangamia na kutoweka,” alisema.

Wakati hilo likitokea katika kikao hicho cha wabunge na wawakilishi, Umoja wa Vijana wa UV-CCM umetoa msimamo wake mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kusema rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekosa mashiko na haikubaliki, kwani imegusa tunu za Taifa na kutaka kuleta mgawanyiko.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akifungua Mkutano Mkuu maalum wa Mkoa wa Magharibi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere huko Bububu, alisema atakuwa mtu wa mwisho kukubali na kuuafiki mfumo wa Serikali Tatu, akiamini mfumo huo umekosa uimara na umadhubuti.

Vuai alisema nje ya Muungano wa sasa anaamini hata Pemba na Unguja hazitakaa pamoja kama zilivyo, na huo utakuwa ni usaliti wa kuviza mawazo ya waasisi wa Muungano ambao waliuanzisha kwa nia njema iliyoliweka Taifa katika mikono salama kwa miaka 50 iliyopita.

Hata hivyo, Vuai alisema hatma ya kupita au kutopita kwa jambo hilo iko mikononi mwa wabunge na wawakilishi wa CCM ambao ni wengi, hivyo wana kila sababu ya kulipinga wazo hilo ambalo liko kinyumne na sera ya msingi ya CCM. Chanzo; Gazeti la Rai
Nilikuwa na wasiwasi kidogo na maendeleo ya Zanzibar siku za karibuni lakini nimetulizwa kuwa hali ni shwari kabisa.

CCM wataliwa pesa zao na ya Zanzibar yatatimizwa.
 
Mbona Zanzibar wanakuja juu sana? siwalikuwa wanadai uhuru wao...
sasa uhuru wao utapatikana kama uhuru wa Tanganyika utapatikana vilevile
 
Kazi bure wakilishana yamini kwa serikali 2, wengine watakula yamini kwa 3
 
Idumu serikali ya watu wa TANGANYIKA!!!!!!
Kuipinga hoja ya serikali tatu yawezekana ukawa MNAFIKI,MCHAWI au MWENDAWAZIMU!
 
Dawa ni kuuvunja tu huu muungano, hawa wazenji kila siku haweshi kututukana sisi inakuwaje wanang'ang'ania huu muungano?
 
Nilikuwa na wasiwasi kidogo na maendeleo ya Zanzibar siku za karibuni lakini nimetulizwa kuwa hali ni shwari kabisa.

CCM wataliwa pesa zao na ya Zanzibar yatatimizwa.
Kulishana yamini haitasaidia, enzi za zidumu fikra za mwenyekiti zimeisha, Lazima Tanganyika yetu irudi na wazenji wabaki na zenji yao kama walivyo sasa, halafu sisi wote tukutane kati na serikali ya muungano. Wanaotaka Tanganyika isifufuke ni wanga kama wanaoroga watoto wao wenyewe kwa sababu ya utajiri, washindwe kabisa
 
acha waapizani, ila ikije kwetu tutaikataa tu. kawa watu wametufanya mataahira. hivi vichwa viwili vya nyerere na karume vinaweza vikafikiria kwa niaba ya watu 46,000,000 tena kwa muda wote? Kituko.
 
Mchakato wa Katiba mpya utafia katika Bunge la Katiba kwa kuwa Wabunge wa CCM watapinga muundo wa serikali tatu na watashinda kwa wingi wao! Ikitokea hivyo Watanzania hawatakubali kwa kuwa wameuchoka Muungano wa serikali mbili ambao kero zake haziishi na pia Watanganyika wameshajiandaa kupokea nchi yao! Raisi Kikwete alishawaasa wenziwe kujiandaa kisaikolojia kwa mabadiliko ambayo mengine hayakwepeki lakini wanafanya shingo ngumu!! Tusubiri!!!
 
Haya majamaa majinga sana huwa yanatoa maamuzi kwa interest zao bila kujali mustkhbali wa vizazi vijavyo utazani wao hawana vizazi
 
Mmmmh mara hii Wazanzibari hawaitaki tena Zanzibar yao. Hapo ndipo huwa wananiacha hoi. Kelele nyingi kumbe hamna kitu. Sasa ngoja tuwape Zanzibar yenu muone kama kugharamikia/kuendesha nchi ni sawa na kula Urojo.
 
Bunge la katiba ni sehemu tu ya mchakato. Hatma yake ni pale wananchi watakaposhiriki katika kura ya maoni ndio mzizi wa fitna utakapokatwa na maslahi ya wengi kuzingatiwa.
 
Mlishane tu hizo yamini hata kilo nzimanzima ila wananchi ndio wenye nchi yetu' na tumeamua' serikali tatu
 
I always desire to be wise...I also pray to be wise! Kuna wakati ni rahisi sana kujikuta umepitwa na mambo ukawa kituko cha historia. Historia inaandikwa na matukio kama haya...tutumie busara sio hizo mbinu za kale za kishirikina zisizo na nafasi kwenye modern times. Hoja zijibiwe kwa hoja na sio viroja.
 
Back
Top Bottom