Wabunge CCM kulishana yamini... Lengo ni Mfumo wa Serikali TATU haupiti !!!

Alhamisi, Januari 16, 2014 08:04 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

*Lengo ni kuhakikisha mfumo wa kuwa na Serikali Tatu haupiti

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewapanga wabunge na wawakilishi watakaokuwa wajumbe kwenye Bunge la Katiba kukataa pendekezo la Serikali Tatu.

Wameonya kuwa, mpango wa kuvunja Muungano wa Serikali mbili na kuunda tatu ni kinyume cha sera na misingi ya chama hicho pamoja na wosia wa waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai kwa sehemu kubwa wana-CCM hao wameonyesha dhamira ya kuweka msimamo wa pamoja kupinga muundo wa Serikali Tatu.

Vyanzo vya uhakika vimesema kuwa mjumbe mmoja ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) alisimama na kuwataka wanachama wenzao wenye fikara ya kutaka Serikali Tatu wasimame na kukieleza kikao manufaa yake, ili kuwashawishi kama ipo haja ya kuunga mkono.

Taarifa zimesema hakuna Mbunge wala Mwakilishi aliyesimama na kutaja faida ya Serikali Tatu na badala yake wote walionekana kuafiki muundo wa Serikali Mbili.

Wawakilishi watatu walisimama kuchangia mawazo yao wakiwemo Salum Turky, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Hamza Hassan Juma Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtupura na Mwakilishi wa Viti Maalum Ashama Bakari Makame.

Hamza alisema kabla ya kuafiki au kukataa ni vyema rasimu hiyo ikaletwa mbele ya wabunge na wawakilishi, ijadiliwe kifungu kwa kifungu na kuona kama muundo wa Serikali Tatu utakuwa na maslahi zaidi kwa Zanzibar au la kabla ya kuukataa au kukubali.

Akasema ipo haja na ulazima wa rasimu hiyo ya pili kujadiliwa na wawakilishi pamoja na wabunge ikiwamo kufanyiwa semina ili kujua kama mabadiliko hayo yana faida na yataweza kuheshimu na kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

“Niko tayari kuikataa kwa sababu za kisera ikiwa itakosa manufaa kwa Zanzibar, tunahitaji kujijenga kiuchumi na kukwamua wananchi wetu kutoka katika ukosefu wa ajira na kuimarisha huduma za jamii,” alinukuliwa.

Hata hivyo aliposimama Turky, alimtaka Mwenyekiti kuhakikisha mpango huo unawekewa kiapo, ili atakayekwenda kinyume adhurike na kupata laana kwa Mungu.

Turky alisema bila hivyo mapatano yao yatakuwa ni kazi bure, na kwamba mbele ya safari wanaweza kuzungukana na kujikuta mpango wa Serikali Tatu ukipita na kuyaweka rehani Mapinduzi ya Zanzibar.

“Tulishane yamini hapa hapa, atakae kwenda kinyume na Kitabu cha Quraan imdhuru na kupata laana, ndivyo walivyofanya hata wazee wetu wa ASP katika kusimamia na kufanikisha mambo ya msingi,” alisema Mwakilishi huyo wa Mpendae.

Ushauri wake uliungwa mkono na Mwakilishi wa Viti Maalum Asha Bakari Makame, aliyesema ni kweli kuna umuhimu wa jambo hilo kufanyika kabla ya usaliti haujapita miongoni mwao.

“Tusipofanya hivyo tutasalitiana wenyewe kwa wenyewe na kuwapa vicheko maadui wetu, ikiwa faida za Serikali Tatu hazioonekani, tusilitingishe Taifa, likitikisika na kupasuka hakuna wa kuliziba, sote tutaangamia na kutoweka,” alisema.

Wakati hilo likitokea katika kikao hicho cha wabunge na wawakilishi, Umoja wa Vijana wa UV-CCM umetoa msimamo wake mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kusema rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekosa mashiko na haikubaliki, kwani imegusa tunu za Taifa na kutaka kuleta mgawanyiko.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akifungua Mkutano Mkuu maalum wa Mkoa wa Magharibi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere huko Bububu, alisema atakuwa mtu wa mwisho kukubali na kuuafiki mfumo wa Serikali Tatu, akiamini mfumo huo umekosa uimara na umadhubuti.

Vuai alisema nje ya Muungano wa sasa anaamini hata Pemba na Unguja hazitakaa pamoja kama zilivyo, na huo utakuwa ni usaliti wa kuviza mawazo ya waasisi wa Muungano ambao waliuanzisha kwa nia njema iliyoliweka Taifa katika mikono salama kwa miaka 50 iliyopita.

Hata hivyo, Vuai alisema hatma ya kupita au kutopita kwa jambo hilo iko mikononi mwa wabunge na wawakilishi wa CCM ambao ni wengi, hivyo wana kila sababu ya kulipinga wazo hilo ambalo liko kinyumne na sera ya msingi ya CCM.

sura%20ya%20rai.jpg

acha tuendelee iwe koloni la tanganyika
 
Cha ajabu hao hao wabunge, mawaziri (hata mkuu wao) wazanzibar wanaoshinikizwa kukataa serikali 3 baaya ya mwaka mmoja tuu watasahau kila kitu na kuja kivingine kabisa ( ki-uamsho uamsho!)

Hii si ajabu kwa sababu wanahofia tukiwa na serikali tatu zile nyumba walizogawiwa bure za Oysterbay na Msasani zinaweza kuota mbawa!! Viongozi wana maslahi binafsi makubwa sana na muungano na hivyo wako tayari kufanya kila hila kuwarubuni walalahoi wasiokuwa na maslahi yo yote.
 
[h=1][/h]Alhamisi, Januari 16, 2014 08:04 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mhe hizo mali walizopora serikalini zitarudi tu hata kama ni miaka 20,zibaki serikali 2 au 3 ni kujidanganya tu,watadanganya wananchi kwa muda tu,ni wapi umewai kuona waporaji wakabaki salama mpaka mwisho?
 
Yawezekana maana hata mimi ishu ya serikali tatu inanitia kichefuchefu, I wish it could be one!
 
Hawa watakuwa wanafiki sana, si kila siku wanalalamika kuwa Tanganyika inawanyanyasa? Si wawe na Zanzibar huru sasa?

ni kweli watakua wanafiki kwa kuisaliti nchi yao, basi so kweli kwamba hao jamaa ndio wanaolalika, ispokuwa wanaolalilia Muungano huu ni walala hoi wakawaida sio viongozozi walafi kama hao
 
suala hapa ni rahisi tuu, waikane katibayao mpya, harafu wasubiri katiba mama ya jmt ndipo watunge ya kwao itakayofuta wimbo wao wa taifa, bendera yao, na wawe mkoa ili serikali iwe moja!

Sisi tulikubari kipoteza utaifa sasa ni zamu yao, wapoteze uzanzibari wao na tuwe taifa moja, waache ubinafsi na kuzingatia maslahi ya watu wachache!
 
Yawezekana maana hata mimi ishu ya serikali tatu inanitia kichefuchefu, I wish it could be one!

Kama we ni ke hicho kichefuchefu inaweza kuwa mimba na ikawa mi ishara nzuri ya mtoto Tanganyika kurudi. Sijawahi kuona watu wanafiki kama Wanzibar kama vipi tuwe na serikali moja na sie watanganyika tumechoka na vi malalamiko vyenu.
 
Mliojidanganya CCM italeta katiba mpya mtuambie sasa. Hakuna katiba mpya hapa zaidi ya kuzuga.
 
mtamkumbuka Tundu Lisu aliyekata wabunge hawa waliopo kuingia bunge la katiba maana hawakuchaguliwa kwa ajili ya bunge hilo lakini kingine nikunyima idadi kubwa ya uwakilishi wa Raia wengi kungia bunge la katiba matokeo yake tunapata katiba ya kiccm sasa tutawasubiri kwenye kura za kuipigia katiba tunaipiga chini.
 
wana zanzibar huru, nasi tunataka tanganyika huru waache unafiki!
 
Bunge la katiba ni sehemu tu ya mchakato. Hatma yake ni pale wananchi watakaposhiriki katika kura ya maoni ndio mzizi wa fitna utakapokatwa na maslahi ya wengi kuzingatiwa.

Kura hizo zitahesabiwa na wapigakura wenyewe au watu wa tume? Kama mpigakura mwenyewe atahesabu TANGANYIKA itarudi vinginevyo sijui. CCM ikiamua jambo imeamua..!
 
Naomba niwakumbushe tu kuwa, wanapaswa kuheshimu maamuzi ya wananchi, hii katiba siyo ya ccm, wajitokeze hadharani mbele ya wenye nchi yao kueleza hayo waliyo nayo, kinyume na hapo ni uhaini, waache hofu, wanapaswa kuvuna walichopanda miaka 52 ya uhuru.
 
Ni rahisi ccm kutumia nguvu kwenye bunge la katiba na kufanikiwa ila ni ngumu kuwashauri watanganyika kukataa serikali yao wakati wa kura ya maoni!!!,nadhani ccm lengo lao isiwepo katiba mpya.

Ushauri wangu kwa ccm,wanaweza kutumia nguvu kubwa kwenye kupitisha katiba hii,ila wajue ikipita bila tanganyika wajiandae na anguko 2015,anguko si lazima kutema urais!!,hata kwenye ubunge itakuwa balaa kama wakiitema serikali ya tanganyika,mwamko wa serikali ya tanganyika ni mkubwa ajabu,kamwe hawawezi kupingana nao ni suala la muda tu,nadhani mtu ukiwa kwenye madaraka uwezo wa kuona na kusikia unapungua!!!yetu macho.

mkuu kiche umenena niko simuni kula LIKE. miccm ikichakachua 3 tier gov, watanganyika tutakuja kukutana nao kwenye uchaguzi ujao. na pia wazenji itabidi warekebishe katiba yao. la sivyo patachimbika tanganyika. jmt haiwezi kuendeshwa kwa katiba zinazokinzana.
 
Sijui hata hawa wanasiasa wanataka nini??Ningewashauri tu watuachie wananchi tuamue.
 
Hawa ni vigeu geu na wanafiki wakubwa wanao jali matumbo yao bila kujali maisha ya wananchi maskini, Hawa hawa wawakilishi wakati wa tume ya katiba ilipokwenda kuchukua maoni katika baraza la wawakilishi walitaka serekali tatu tena wote wa ccm na cuf ama kweli hawa ni vigeu geu.
 
Back
Top Bottom