Wabunge CCM kulishana yamini... Lengo ni Mfumo wa Serikali TATU haupiti !!!

Wabunge CCM kulishana yamini... Lengo ni Mfumo wa Serikali TATU haupiti !!!

Siku zote ukikaa na kuwafikiria sana wabunge na viongozi wa CCM utabaki na mshangao wa kutisha ambao hujawahi kuushuhidia kabla hapa Afrika! Hivi kama serikali 3 ni wazo la watanzania wabunge hao wasiozidi 200 pamoja na viongozi wao wanaweza vipi kula yamini kwa ajili ya watanzania wanaotaka serikali 3 zaidi ya milioni 20?!

Kwa nini wasilishane yamini kuhakikisha kuwa kabla ya 2015 ahadi za JK ziwe zimekamilika kwa asilimia angalau 80 tu?! Yaamini haijawahi kuliwa na watu wanafiki na wazandiki! Zanzibar wanataka nchi yao na wameona serikali 3 ndio njia, watanganyika wenye kuitaka Tanganyika yao wameshaamka na sasa wanataka kuiona Tanganyika yao inarudi, wabunge na viongozi wa CCM hata wakilishana yamini mpaka shingoni hawawezi kuzuia wazo ambalo tayari muda wake muafaka umeshafika!

Wanatakiwa kujua hakuna yamini iliyowahi kuzuia mawazo ya watu ambayo muda wake muafaka ulikuwa umeshafika fika, kama jinsi ambavyo halikuwahi kutokea jeshi kubwa lenye vifaa vya kisasa ulimwenguni lililowahi kuzuia mawazo ya kimapinduizi hasa pale mapinduzi yanapokuwa kuwa ndio chaguo pendwa la mwisho la watu hao.
 
Sikwamba wazanzibari hawaitaki zanziba yao la hasha, ni propoganda za magamba wachache na ukitaka kupata ukweli huu waulize mwanasheria mkuu wa Zanziba, Mwasisi wa Muungano Nasoro Moyo, Maalimu Seif na wengineo, wanaotamani Serikali mbili ni wahafina magamba wachache wapenda ukuu kama akina Nahodha na wenzake
 
Mim CCM naishangaa sana... utafikiri familia ya kambale... Haohao CCM Zanzibar chini ya Baraza la Wawakilishi walifanya mabadiliko kwenye Katiba yao ya Zanzibar huku wakijua kabisa mabadiliko na Ibara walizoziongeza zilikuwa zinahatarisha Muungano... Wasiwe wanafiki,,, Kama wanataka Serikali mbili wafanye mabadiliko kwenye Katiba yao ili ieandane na Katiba ya Jamhuri...

Haiwezekani wanataka Serikali mbili, huku wao wenyewe wameshaisigina na kuinajisi Katiba ya Muungano... Kama walikuwa wanabip kwa Watanganyika sasa ndo wanapigiwa... Wasituchanganye!!! Kama Serikali mbili inafaa mabadiliko makubwa waliyoyafanya kwenye Katiba yao yalikuwa ni ya nini kama si kuudhofisha muungano... Kama wanaona Muungano ni muhimu basi suluhisho ni Serikali Tatu, kama wanaona watanganyika watafaidi basi iwe Serikali moja na kama nako kuna tatizo tukubali Serikali ya Majimbo...
 
Kama hawataki serikali tatu wavunje muungano. Halafu hawa ccm wanaangalia maslahi ya chama chao badala ya taifa.

I.D.I.O.T
 
Cha ajabu hao hao wabunge, mawaziri (hata mkuu wao) wazanzibar wanaoshinikizwa kukataa serikali 3 baaya ya mwaka mmoja tuu watasahau kila kitu na kuja kivingine kabisa ( ki-uamsho uamsho!)
 
Ni rahisi ccm kutumia nguvu kwenye bunge la katiba na kufanikiwa ila ni ngumu kuwashauri watanganyika kukataa serikali yao wakati wa kura ya maoni!!!,nadhani ccm lengo lao isiwepo katiba mpya.

Ushauri wangu kwa ccm,wanaweza kutumia nguvu kubwa kwenye kupitisha katiba hii,ila wajue ikipita bila tanganyika wajiandae na anguko 2015,anguko si lazima kutema urais!!,hata kwenye ubunge itakuwa balaa kama wakiitema serikali ya tanganyika,mwamko wa serikali ya tanganyika ni mkubwa ajabu,kamwe hawawezi kupingana nao ni suala la muda tu,nadhani mtu ukiwa kwenye madaraka uwezo wa kuona na kusikia unapungua!!!yetu macho.
 
Wapi uamsho, daini zanzibar yenu mkishindwa hapa tutawatawala milele,kudadadeki
 
sanduku la kura ndo kila kitu.waboreshe daftari la wapiga kura ili mbivu na mbichi zijulikane.
 
Alhamisi, Januari 16, 2014 08:04 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar


*Lengo ni kuhakikisha mfumo wa kuwa na Serikali Tatu haupiti

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewapanga wabunge na wawakilishi watakaokuwa wajumbe kwenye Bunge la Katiba kukataa pendekezo la Serikali Tatu.

Wameonya kuwa, mpango wa kuvunja Muungano wa Serikali mbili na kuunda tatu ni kinyume cha sera na misingi ya chama hicho pamoja na wosia wa waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao kilichoketi chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai kwa sehemu kubwa wana-CCM hao wameonyesha dhamira ya kuweka msimamo wa pamoja kupinga muundo wa Serikali Tatu.

Vyanzo vya uhakika vimesema kuwa mjumbe mmoja ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) alisimama na kuwataka wanachama wenzao wenye fikara ya kutaka Serikali Tatu wasimame na kukieleza kikao manufaa yake, ili kuwashawishi kama ipo haja ya kuunga mkono.

Taarifa zimesema hakuna Mbunge wala Mwakilishi aliyesimama na kutaja faida ya Serikali Tatu na badala yake wote walionekana kuafiki muundo wa Serikali Mbili.

Wawakilishi watatu walisimama kuchangia mawazo yao wakiwemo Salum Turky, Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Hamza Hassan Juma Mwakilishi wa Jimbo la Kwamtupura na Mwakilishi wa Viti Maalum Ashama Bakari Makame.

Hamza alisema kabla ya kuafiki au kukataa ni vyema rasimu hiyo ikaletwa mbele ya wabunge na wawakilishi, ijadiliwe kifungu kwa kifungu na kuona kama muundo wa Serikali Tatu utakuwa na maslahi zaidi kwa Zanzibar au la kabla ya kuukataa au kukubali.

Akasema ipo haja na ulazima wa rasimu hiyo ya pili kujadiliwa na wawakilishi pamoja na wabunge ikiwamo kufanyiwa semina ili kujua kama mabadiliko hayo yana faida na yataweza kuheshimu na kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

“Niko tayari kuikataa kwa sababu za kisera ikiwa itakosa manufaa kwa Zanzibar, tunahitaji kujijenga kiuchumi na kukwamua wananchi wetu kutoka katika ukosefu wa ajira na kuimarisha huduma za jamii,” alinukuliwa.

Hata hivyo aliposimama Turky, alimtaka Mwenyekiti kuhakikisha mpango huo unawekewa kiapo, ili atakayekwenda kinyume adhurike na kupata laana kwa Mungu.

Turky alisema bila hivyo mapatano yao yatakuwa ni kazi bure, na kwamba mbele ya safari wanaweza kuzungukana na kujikuta mpango wa Serikali Tatu ukipita na kuyaweka rehani Mapinduzi ya Zanzibar.

“Tulishane yamini hapa hapa, atakae kwenda kinyume na Kitabu cha Quraan imdhuru na kupata laana, ndivyo walivyofanya hata wazee wetu wa ASP katika kusimamia na kufanikisha mambo ya msingi,” alisema Mwakilishi huyo wa Mpendae.

Ushauri wake uliungwa mkono na Mwakilishi wa Viti Maalum Asha Bakari Makame, aliyesema ni kweli kuna umuhimu wa jambo hilo kufanyika kabla ya usaliti haujapita miongoni mwao.

“Tusipofanya hivyo tutasalitiana wenyewe kwa wenyewe na kuwapa vicheko maadui wetu, ikiwa faida za Serikali Tatu hazioonekani, tusilitingishe Taifa, likitikisika na kupasuka hakuna wa kuliziba, sote tutaangamia na kutoweka,” alisema.

Wakati hilo likitokea katika kikao hicho cha wabunge na wawakilishi, Umoja wa Vijana wa UV-CCM umetoa msimamo wake mbele ya Rais Jakaya Kikwete na kusema rasimu ya pili ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekosa mashiko na haikubaliki, kwani imegusa tunu za Taifa na kutaka kuleta mgawanyiko.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai wakati akifungua Mkutano Mkuu maalum wa Mkoa wa Magharibi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere huko Bububu, alisema atakuwa mtu wa mwisho kukubali na kuuafiki mfumo wa Serikali Tatu, akiamini mfumo huo umekosa uimara na umadhubuti.

Vuai alisema nje ya Muungano wa sasa anaamini hata Pemba na Unguja hazitakaa pamoja kama zilivyo, na huo utakuwa ni usaliti wa kuviza mawazo ya waasisi wa Muungano ambao waliuanzisha kwa nia njema iliyoliweka Taifa katika mikono salama kwa miaka 50 iliyopita.

Hata hivyo, Vuai alisema hatma ya kupita au kutopita kwa jambo hilo iko mikononi mwa wabunge na wawakilishi wa CCM ambao ni wengi, hivyo wana kila sababu ya kulipinga wazo hilo ambalo liko kinyumne na sera ya msingi ya CCM.


sura%20ya%20rai.jpg


Chama chakavu sawa na ukoo wa panya!
Sisi tunajadili katiba kwa maslahi wa WaTZ wote wao wanaangalia maslahi ya chama na matumbo yao tu!
 
sanduku la kura ndo kila kitu.waboreshe daftari la wapiga kura ili mbivu na mbichi zijulikane.
 
kwa hiyo mchakato wa katba mpy si huru ni wa ccm.mhmm tuendako!
 
JK alisema ikishindwa kupita tutarudi kwenye katiba ya zamani ni sawa lakini pia sie watanzania tutataka kumaliza biashara kwa kuidai Tanganyika yetu iwe kwa mtaani,msituni ama kwenye makaratasi
 
awana hoja hawo wakajipange upya then ndo warudi, tanganyika ileeeeeeeeee!!! tunaisubiri kwa amu kubwa sana
 
kuna yamini ya sauti na ile ya kimoyo moyo huku umeuma meno.
 
Ninyi mna matatizo kweli. Mnafikiri Mungu ni CCM?
 
Hii ni demokrasia au ghasia tu. Watu wanajali chama kuliko nchi. Wananchi wasifanye makosa 2015
 
Serikali mbili zpi? Muungano na ZNZ wapi Tanganyika Au ndio 1+1=2? ilitumika La sivyo tupeane Zamu Next 50years tuwe na Tanganyika na Muungano.
 
Hawa wamezowea migogoro isiyokuwa ya lazima. Tukumbuke hata hatua za kuleta maridhiano walipiga kelele hivi hivi mpaka Raia Karume akawa mkali, leo ndio wapo mbele kutetea maridhiano hayo. Ndani ya CCM wapo wengi wenye busara na wanaunga mkono rasimu hii ya katiba. Tuwadharau tu.
 
Bunge la katiba ni sehemu tu ya mchakato. Hatma yake ni pale wananchi watakaposhiriki katika kura ya maoni ndio mzizi wa fitna utakapokatwa na maslahi ya wengi kuzingatiwa.

Mkuu unasemea wanaNCH gani? au ni hawa wanaolishwa Pilau nakuvishwa Kapelo kisha wanamchagua huyo Mwezeshaji wao? Mnaotegemea kuwa CCM wataleta KATIBA 2nayotamani 2tangoja sana!
 
Back
Top Bottom