Wabunge Kenya waanza mikakati ya kujilimbikiza mishahara wananchi nao wagoma!

Wabunge Kenya waanza mikakati ya kujilimbikiza mishahara wananchi nao wagoma!

922982_306641366135003_1111854480_n.jpg



941192_306641482801658_676401481_n.jpg
 
Maandamano ya kupinga nyongeza ya mishahara kwa wabunge wa Kenya yanatarajiwa kuanza leo.Maandamano hayo yataanza katika mji wa Mombasa,pwani ya Kenya.Lakini pia yamepangwa kufanyika katika maeneo mengine nchini.

Ni maandamano yaliyopangwa kufanyika wiki nzima kuteta kuhusu kuongezewa posho kwa wabunge. Chama kikuu cha wafanyakazi nchini Kenya COTU kinaongoza maandamano hayo kikishirikiana na chama cha waalimu pamoja na mashirika mengine.

Wajumbe wa Kenya ni miongoni mwa wajumbe wanaolipwa mishahara ya juu duniani. Wabunge hao wamekataa kwenda mapumzikoni wakitaka suala la mishahara lijadiliwe kwanza. Wanaoandama wanasema wanafanya hivyo kutokana na kuwa wabunge wameonyesha kutojali maslahi ya raia kwa kupitisha ripoti iliyopendekeza kuongezwa kwa mishahara yao.

Tangu wakati huo kumekuwa na hisia mbali mbali huku wabunge wengine wakipinga nyongeza hiyo na wengine kusema wanastahili kupata nyongeza kwa kuwa sasa mishahara yao itakuwa inatozwa kodi.

Source:BBC
 
Wakati huohuo Tanzania akina Nchimbi wanaongelea kuhusu kupiga marufuku maandamano ya aina yoyote ile!
Nchi ya watu wadogo!
 
Na hiyo ndo tofauti kubwa sana kati ya wananchi wa Kenya na Tanzania
 
dah tz hapo mheshimiwa ko ashazuia maandamano kwa mabomu saa nyingi na mjadala ukiendelea bungeni. hivi tz mbona hatujui kusoma na picha hata hatuzioni? nipe macho nione macho eeeee nipe macho nione sawasawaaaa
 
Ndio nacheck hapa Citizen live😱ccupying parliament:-civil society protesting Mps salary demand.
 
Kwa sasa askari wanapakia noah na watoto wao ambao walikuwa katikati ya mlango wa kuingia bunge la kenya.
 
Nimeona citizen ila sasa hao nguruwe wameondolewa kwa kutumia gari ya serikali
Hii nchi ya kenya bana ngoja wale
 
Nimeona citizen ila sasa hao nguruwe wameondolewa kwa kutumia gari ya serikali
Hii nchi ya kenya bana ngoja wale

yap walikuwa wamesambazwa karibia sehemu nying za nairob,wakenya wanajitambua sie bado 2melala.
 
ingekua bongo land makengeza angeseme intelijensia inasema kuna watu ambao watatumia maandamano hayo kulipua makanisa na kudhuru wenzao chezea makengeza weye vipi wale watekaji wa kibanda bado hajawataja au ile jumatatu aijafika?
 
alafu mnataka kusema eti nasi tujilinganishe na hawa, wakimya mpaka waziri anatushangaa!pay1.jpg
 
... Mm ni mzalendo wa nchi yangu TZ, lakini kwa maana ya neno "UZALENDO" wananchi wakenya wametupita sana kwa kutetea maslahi ya nchi...
Hii Elimu ya "Jitambua" ikifanywa kwa umakini inaweza kusaidia wa TZ kujua wajibu wetu...
 
Back
Top Bottom