Watanzani ni watu wa ajabu kwa maana ya ''so special'' mtaendelea kupata tabu mkiwafananisha na watu kama wakenya au mataifa mengine... Hicho ndo kitu kikubwa wanasiasa mnakisahau na kutaka wafanye mambo wanavyotaka wao. tunasahau kuwa tuna utamduni wetu katika kuamua kufanya vitu na si WAJINGA kama mnavyofikiri, ili kuamua hatuhitaji nguvu kiivyooo au maandamano kiivyooo, Ukikaa chini kwa utaratibu watakusikiliza na kukuelewa japo tuna tabia ya kuchukua muda mrefu hadi kufikia kutoa maamuzi ambao faida yake kubwa ni kutoa maamuzi yenye umakini fulani!!
Hao wakenya mnawasifia au kuwatolea mfano wana matatizo kuliko mnayoyasikia kwenye vyombo vya habari kuwa kuna demockrasia kuliko TZ. Fuatilieni hali zao halisi kimaisha ukilinganisha na idadi yao, msipumbazike na taarifa za kwenye makaratasi.... wallahi TUKO huru sana kuliko wao, wana matatizo kuliko sie japo wanzungumza kiingereza kuliko sie kama nacho ni kigezo!lol kwa kifupi tu Kubeba nguruwe na kwenda nae bungeni ukimlisha damu inaonyesha ni jinsi gani ULIVYO CHOKA na maisha na unatafuta haki kwa njia hiyo! itachukua miaka mingi kwa Tz kuwa hivyo...
Sie bado tuna OPTIONS katika kufanya mambo mengi lkn hawa jamaa hakuna, hakuna yaani hata ardhi iko mikononi mwa wenye pesa, unategemea nini kwa kizazi kipya?
TANZANIA ITAENDELEA KUWA TANZANIA na aina yake SPECIAL ya kufanya mabadiliko Kisiasa sio lazima kuwa kama mataifa mengine....