Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 586
- 590
- Thread starter
- #41
Machungu yapi hayo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Machungu yapi hayo?
Interview zao niliziona. Na ujinga uliofanywa na tume pia niliuona.Tusiandikie mate wino ungalipo.
Eleza kwa uwazi wapi uchaguzi ulikuwa na vurugu. Kwa sababu wagombea wote walipiga kura na kuhojiwa na vyombo vya habari.
Kwa mfano Sugu alisema wazi baada ya kupiga kura kuwa mambo yapo shwari na atashinda.
Tundu Lissu alisema hali ni tulivu na mambo yote yapo barabara.
Vivyo hivyo kwa wengine.
Waliokutangulia Wameyasema sana mkuu hii Nchi CCM IMEROGWA haitapata Maendeleo kamweHayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema mwaka 1995 kuwa "Ukipewa kazi ya nchi, lazima ujiheshimu. Huwezi kupewa kazi ya nchi halafu ukaishi kihunihuni." Ni kweli kuwa dunia inaenda kasi na pia wakati ni ukuta; muda ni mchache na mambo ni mengi lakini kama umepewa kazi ya nchi ni lazima ujiheshimu. Ndugu zetu wabunge na watumishi wa umma kuna sauti ya mtu iliayo nyikani. Tafadhaini itengenezeni njia na yanyosheni mapito katika kazi za nchi ili sisi sote tupate kuyaona maendeleo jumuishi ya nchi.View attachment 1847346
Jana tarehe 08/07/2021 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akiwa Sumbawanga mkoani Rukwa alitoa maagizo mawili ambapo agizo moja lilienda kwa wabunge na jingine lilienda kwa watumishi wa umma.
WABUNGE
Kuna wabunge tangu kuahirishwa kwa mkutano wa 3 wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bungeni jijini Dodoma Juni 30, 2021 bado hawajarudi majimboni, wako Dodoma, Dar Es Salaam, Njombe, Kigoma ama wapi jamani? Mimi na wewe hatujui ila sauti iliayo nyikani imetoa maagizo ya Chama kwa kuelekeza "Maagizo kwa Wabunge wote, lazima warudi kwenye majimbo yao kule walikoomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi na wahakikishe wanawapelekea taarifa ya kilichopangwa kwenye bajeti kwa ajili ya majimbo yao."
Sisi wananchi tunawasubiri huku majimboni kwa ajili ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 hususan katika suala la fedha za barabara za vijijini zile milioni 500 kwenye kila jimbo na zimeshathibitishwa. Karibuni na njooni tutatue changamoto na kupata maendeleo kwa sababu kupitia hiyo fedha katika barabara za vijijini kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima kitashushwa, palipopotoka patakuwa pamenyoka na palipoparuza patalainishwa.
WATUMISHI WA UMMA
Ukiwa mtumishi wa umma una wajibu wa kuwa mwadilifu, kuhakisha wananchi wanapokea huduma bora na unakuwa mzalendo kwa taifa (maslahi kwa taifa yanatangulizwa mbele). Kuna mkwamo wa upatikaji wa dawa; sauti iliayo nyikani imesema kwamba itawasiliana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Doroth Gwajima, pamoja na uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) kujua mamilioni ya fedha yanayotolewa kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa dawa yanakwama wapi? “Watueleze (Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) nani anasababisha mkwamo katika upatikanaji wa dawa. Viongozi tuna wajibu wa kufuatilia na kusimamia thamani ya fedha katika kila eneo.” Amesema Ndg. Chongolo.
Sambamba na hilo amewaonya watumishi umma juu ya fedha ya umma kuwa CCM haitacheka na mtu “Tutakuwa wakali, ni lazima tuogope fedha ya umma. Ukizitumia vizuri (fedha za umma) zitakujengea heshima, ukizitumia vibaya zitakuvunjia heshima. Kila mmoja anapaswa kuwa mwadilifu.” na pia akasititiza uwajibikaji “Ni lazima tufanye kazi yenye tija. Wananchi wakiona mambo hayaendi, watatuona sisi (CCM) tunapiga porojo. Hatuko tayari kuitwa wapiga porojo.”
Ndugu zetu wabunge na watumishi wa umma tubuni pale mlipokosea, fanyeni kazi kwa bidii, nyosheni utendaji na kuwa wema katika matendo maana wakati umekaribia kama mlivyoisikia sauti ya mtu anaita jangwani kwa kuwa atakayekuja baada ya huyu ana nguvu kuliko sauti hii yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka ili aipure nafaka; akusanye ngano ghalani na makapi ayachome kwa moto.
Uhakika huo ni dhahania hasi ambayo imejengeka. Kama ambavyo mashabiki wa Simba wanahisi Mzee Mpili ndiye aliyekamilisha ushindi wa Yanga dhidi yao.Interview zao niliziona. Na ujinga uliofanywa na tume pia niliuona.
Sina cha kuhadithiwa kwani kila kitu niliona. Hakuna aliye na uhakika hata mmoja kama kweli alichaguliwa na wananchi bali wote wana uhakika kuwa jiwe aliwachagua.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Siku zetu za kuishi hapa duniani zimehasabiwa.
KabisaSiku zetu za kuishi hapa duniani zimehasabiwa.
Mkuu maendeleo yapo ila kasi inabidi iongezeke kwa kila mmoja; viongozi na wananchi kujua wajibu wetu na kuutekeleza bila kushuritishwa.Waliokutangulia Wameyasema sana mkuu hii Nchi CCM IMEROGWA haitapata Maendeleo kamwe
Ilikuwa wazi mno. Vituko vya tume vilikuwa wazi kabisa. Ilisikitisha sana viongozi kudharau wananchi wake kiasi kile. Ile dharau Mungu atawalipa.Uhakika huo ni dhahania hasi ambayo imejengeka. Kama ambavyo mashabiki wa Simba wanahisi Mzee Mpili ndiye aliyekamilisha ushindi wa Yanga dhidi yao.
Hapana Mkuu. Nia ya dhati ipo ya kuitumikia wananchi, tuwakumbushe pale wanapojisahau.Hakuna mwenye nia njema na wananchi, watu wapo pale ajili ya kupiga pesa.
Tusonge mbele, Kazi Iendelee.Ilikuwa wazi mno. Vituko vya tume vilikuwa wazi kabisa. Ilisikitisha sana viongozi kudharau wananchi wake kiasi kile. Ile dharau Mungu atawalipa.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Kungekuwa na nia nchi ingekuwa mbali sn kwa maendeleo watu wanapiga pesa na maisha yanaenda.Hapana Mkuu. Nia ya dhati ipo ya kuitumikia wananchi, tuwakumbushe pale wanapojisahau.
Waweke wazi hao watu Mkuu.Kungekuwa na nia nchi ingekuwa mbali sn kwa maendeleo watu wanapiga pesa na maisha yanaenda.