Wabunge nchini Marekani wamepiga kura za kumwondoa Rais Biden madarakani kwa tuhuma za Rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kuitajirisha familia yake

Wabunge nchini Marekani wamepiga kura za kumwondoa Rais Biden madarakani kwa tuhuma za Rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kuitajirisha familia yake

Eti impeachment imefanyika bila resolution wala bila taarifa kujulikana kabla. Bunge la Marekani halifanyi kazi kienyeji, haliogopi mtu. Utaratibu unachukua wiki kadhaa watu wanafanya kwa uhuru, ushahidi unatolewa, hapo unakuta directors wa idara kadhaa wanaapishwq kutoa ushahidi. Hapo wangeitwa wahusika wa kupambana na madawa au polisi, wakaitwa watu wa kodi na labda FBI.
Sio kienyeji na ghafla hivi
Na wapo watu unawaona kikasuku wanakubaliana tu kana kwamba ameshapigiwa kura ya kuondolewa Urais.

Huu ndio upotoshaji wa hali ya Juu.

Halafu wamo humu wanaodai haya Unayaona kwenye Nchi zilizoendelea, wakati wao kule wanadai haya yanatokea kwenye Nchi ambazo hazijaendelea.
Uzuzu tu.

Nashikilia pale pale tu, ni upotoshaji.
 
Mkuu,
Nahisi pia lugha ni ngumu nimeshangaa kichwa cha habari na stori iliyoandikwa Fox. Lugha tatizo pia mkuu.
Yawezekana lugha ikawa ngumu. Lakini kwa huyu, hapana, lugha anaijua, ni mpotoshaji tu.

Hatahivyo huyu mjamaa ndivyo alivyo. Huwa anamwaga mada za kusisimua na kutia chumvi alimradi watu(watu wake) waongezee vinyongo vyao. Tizama wapi anatoa likes utaelewa. Eniweyi

Ukweli ni kwamba Kura imepigwa, na kura hiyo ni ya kukubaliana kwa bunge kuanza mchakato wa kufanya uchunguzi na sio kura ya kumuondoa madarakani Raisi kama alivyowasilisha kwenye bandiko kuu.
 
Huku kwetu nchi imejaa panyaroad tu, wale wa ikulu, mashirika ya, umma,wanaovaa suti,na wengine wa huku kitaa, ambao kama mazingira yangekuwa mazuri, huenda wangekuwa watu Bora Sana,
 
Kama ni kweli wapo vizuri, hatulingani nao na wala hatutalingana nao kwenye level ya demokrasia
Umeelewa kilichoandikwa au Kiinglishi kinakuchanganya? Wameandika hivi, wabunge wote wa Republican (wapinzani) 221 wamepiga kura kumu impeachment na wabunge wote wa Democrat (watawala) 212 wamepiga kura kupinga impeachment. Tofauti yake na Tanzania ni ipi? Sio Kila kitu kusifia tu!
 
sasa imewezekanaje apate fursa za kupiga madili ya Rushwa wakati mifumo yao ni ya uwazi na haki?

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Hakuna kilichothibitishwa.

Kura ya bunge (Congress) ni ya kuidhinisha mchakato wa impeachment ufanyike. Ndipo itakapoeleweka kama huo "upigaji" ulifanyika kweli na ki vipi? Bila shaka unaelewa vizuri sana kuwa hayo yanaweza kufanyika tu kwenye nchi yenye mifumo imara ya wazi na haki.

Kwenye nchi zinazoendeshwa kiimla Rais na jamii yake ni "untouchable".
 
Back
Top Bottom