Wabunge ndio maadui Wakwanza wa Maendeleo yetu na wanatunyonya

Wabunge ndio maadui Wakwanza wa Maendeleo yetu na wanatunyonya

Kama hawa ndio vinara wa kuagiza wapigiwe picha za uchi za wanawake watumiwe unategemea kuna mtu mwenye mawazo ya maana hapo? ndiomaana hata hao wanawake kazi yao ni kushinda kwenye kioo tu na kujipura huku wakisubiria posho basi maisha yaende.
 
Hapa KATIBA ndo ibadilishwe, iundwe KATIBA mpya iliyo Wazi.
Haiwezekani hawakatwi contribution popote na kuinua mgongo wanachukua huu ni Wizi na unyonyaji
 
Watanzania. Naomba kwa heshima na Taadhima. Leo hii tufahamu wanaotukwamisha katika maendeleo ni akina nani. Hatuwezi shinda vita vya Umaskini ikiwa Hatujafahamu Maadui zetu ni akina nani.

Tunapaswa pia tufahamu wanaopigana wakiwa upande wetu bega kwa bega ni akina nani. Wanaweza kuwepo watu wa namna hiyo lakini si Wabunge.

Sikiliza haya yanayohusi Wabunge. Halafu tupaze sauti zetu kuwataka waache kutunyonya. Waache kuumiza Watanzania Maskini.

Kwa mtazamo wang.. kingeanzishwa chama ambacho kinajumuisha wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji na wale wote ambao hawajaajiriwa na serikali kikawa kama chama pinzani dhidi ya bunge kikalikosoa bunge na wabunge kwa ujumla wake kama ilivyo vyama Pinzani vya siasa dhidi ya CCM , ilikutetea maslahi ambayo wabunge wanayakalia na kuwakandamiza wananchi ambao sio wabunge. Makato Yao na stahiki zao zikafanana na wananchi wengine
 
Wamekuwa wanatunyonya kimya kimya. Hili la kuweka wazi litawaudhi sana. Tuone watasema nini.

Na kwa katiba iliyopo ni CCM, na siyo wananchi, huamua nani awe mbunge.

Tuwaombe waache kutunyonya kihivyo? Mbona kwa aliyezoea kunyonya ni shida sana kuacha! Kwani tunaweza kuwafanya nini? Hakuna! Power is not in the hands of the people. Ndiyo katiba iliyopo, na hawataki kuibadilisha. Wanaiona ni nzuri sana.
 
Tutawezaje kuendelea kama viongozi wa kisiasa wana uhuru wa kujipangia marupurupu kiasi chochote wapendavyo? Ukiacha hili la wabunge, viongozi wastaafu pia wamejipangia malipo makubwa kupita kiasi. Wamejipangia asilimia 80 ya mshahara wa anayerithi nafasi yao, kila mwezi. Kwa kazi gani?

Ama kweli kikulacho kiko nguoni mwako.
 
Kwa mtazamo wang.. kingeanzishwa chama ambacho kinajumuisha wafanyakazi, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji na wale wote ambao hawajaajiriwa na serikali kikawa kama chama pinzani dhidi ya bunge kikalikosoa bunge na wabunge kwa ujumla wake kama ilivyo vyama Pinzani vya siasa dhidi ya CCM , ilikutetea maslahi ambayo wabunge wanayakalia na kuwakandamiza wananchi ambao sio wabunge. Makato Yao na stahiki zao zikafanana na wananchi wengine
Tatizo ni kwamba nchi hii kundi lolote likiwa organised linatekwa na wanasiasa.
 
Wabunge ni namba moja ila Politicians in general ndio virus wa maendeleo wa Nchi hii akili zao zipo kwenye mishahara minono, posho na wizi wa pesa za Umma.

Nchi hii bila wanasiasa tungekuwa mbali sana
Wanalipana wanavyopenda
 
Bunge la sasa lina wabunge wengi sana. Wapunguzwe kila wilaya iwe ndio jimbo. Wilaya ikiwa kubwa ndio igawanywe.

Mshahara wa wabunge uwe sawa na watumishi wengine wa umma.

Cheo cha waziri mkuu kiondolewe kama kweli tuna practise mfumo wa kuwa na Rais. Makamu wake ndiye awe mtendaji mkuu wa shughuli za kiserikali na kiongozi wa serikali bungeni.

Manaibu waziri wapigwe chini wote. Makatibu wakuu wa wizara wanatosha kuwasaidia mawaziri majukumu.

Wilaya ambazo zinaunda halmashauri hakuna haja ya kuwa na DED, DAS na RC. Vyeo vipungue kupunguza matumizi na kuimarisha utendaji.
 
Tuanze na kupunguza mishahara yao iwe nusu, kisha tuwaambie walipe kodi na PSSSF, na wakimaliza muda wao wasubirie miaka miwili kupewa kiinua mgongo.

Wasiruhusiwe kukopa kutoka mifuko ya PENSION.

Yangu mimi ni hayo tu.

Everyday is Saturday............................... 😎
Hahah nao wakapate Raha ya kuzungushwa pesa zao na PSSSF.
 
Watanzania. Naomba kwa heshima na Taadhima. Leo hii tufahamu wanaotukwamisha katika maendeleo ni akina nani. Hatuwezi shinda vita vya Umaskini ikiwa Hatujafahamu Maadui zetu ni akina nani.

Tunapaswa pia tufahamu wanaopigana wakiwa upande wetu bega kwa bega ni akina nani. Wanaweza kuwepo watu wa namna hiyo lakini si Wabunge.

Sikiliza haya yanayohusi Wabunge. Halafu tupaze sauti zetu kuwataka waache kutunyonya. Waache kuumiza Watanzania Maskini.

Watz peke ndio wabunge wake huwa upande wa siri Kali ktk kumvisha NIRA ya maskai MTU wa hali ya chini huku wakimwimbia mapambio, hii ni ajabu sana.
 
Back
Top Bottom