Wabunge wa CCM 'walioanguka' kura za wajumbe

Wabunge wa CCM 'walioanguka' kura za wajumbe

Katika kile kinachoonekana kama mabadiliko ya upepo wa kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wabunge kadhaa waliokuwa wakitetea nafasi zao wamejikuta wakitemwa na wajumbe wa chama hicho katika kura za maoni zilizofanyika Agosti 4, 2025, katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Ingawa matumaini yao ya kurejea kwenye kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu bado yapo mikononi mwa vikao vya juu vya CCM, uamuzi wa wajumbe unaonesha wazi kuwa baadhi ya majina makubwa huenda yakasalia kuwa historia.

Katika Jimbo la Vunjo, Dr. Charles Kimei ambaye amekuwa mbunge tangu 2020 ameangushwa na Enock Zadock Koola aliyeibuka mshindi kwa kura 1,999 dhidi ya Kimei aliyepata kura 861. Hii ni mara ya pili kwa Koola kushinda kura za maoni katika jimbo hilo, baada ya kufanya hivyo pia mwaka 2020, ingawa hakupitishwa.

Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi amepoteza mbele ya Moris Makoi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Makoi alipata kura 2,148 huku Ndakidemi akijikusanyia kura 627 pekee.
Katika Jimbo la Iringa Mjini, aliyekuwa mbunge Jesca Msambatavangu amejikuta nafasi ya nne kwa kura 408. Mshindi wa kura hizo ni Fadhil Ngajilo aliyepata kura 1,899, akifuatiwa na Wakili Moses (1,523) na Mchungaji Peter Msigwa (477).
Kyerwa, Mbunge Innocent Bilakwate ameangushwa na Khalid Nsekela aliyezoa kura 5,693 sawa na asilimia 71 huku Bilakwate akipata kura 1,567.

Katika Jimbom la Makambako, Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Daniel Chongolo ameibuka mshindi wa kishindo kwa kura 6,151, na kumwacha mbali Deo Sanga (maarufu kama Jah People), aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 15, ambaye alipata kura 470 tu sawa na asilimia 7.1.
Tabora Mjini, Shabani Mrutu ameongoza kwa kura 6,612, akimshinda kwa mbali aliyekuwa mbunge Emmanuel Mwakasaka aliyepata kura 228 pekee. Mwakasaka alizidiwa hata na wapinzani wengine kama Hawa Mwaifunga (326) na Kisamba Tambwe (395).

Geita Mjini, Constantine Kanyasu ambaye amehudumu kwa miaka 10, amepata kura 2,097 na kushindwa na Chacha Wambura aliyepata kura 2,145. Upendo Peneza alipata kura 1,272 na wengine waliambulia makumi ya kura.

Kwa Jimbo jipya la Katoro, aliyekuwa Mbunge wa Busanda, Tumaini Magesa, alihamia huko lakini akashika nafasi ya tatu kwa kura 1,265 nyuma ya Kija Ntemi (2,134) na Ester James (2,075).

Katika jimbo la Namtumbo, aliyekuwa Mbunge Vita Kawawa ameshindwa mbele ya Dkt. Juma Zuberi Homera, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Homera alipata kura 11,836 asilimia 92 huku Kawawa akipata kura 852.

Mtwara Mjini, Joel Arthur Nanauka ameibuka mshindi kwa kura 2,045 dhidi ya Hassan Mtenga Mbunge anayemaliza muda wake aliyepata kura 1,607.
Katika Jimbo la Lindi Mjini, Mbunge anayemaliza muda wake, Hamida Abdalla, ameangushwa na Mohamed Utali, aliyeibuka kidedea kwa kupata kura 1,474 kati ya kura 3,289 zilizopigwa. Hamida alipata kura 876 pekee, ishara ya wazi kuwa wajumbe wameamua kubadili mwelekeo wa uongozi katika eneo hilo.

Nyasa, hali haikuwa tofauti aliyekuwa Mbunge na Naibu Waziri wa zamani, Stella Manyanya, ameangushwa kwa kishindo na John Nchimbi, aliyepata kura 9,157 kati ya kura 10,695 zilizopigwa. Manyanya alipata kura 548 tu, matokeo ambayo ni pigo kubwa kwa mbunge huyo mkongwe aliyedumu kwa vipindi kadhaa ndani ya Bunge.

Katika Jimbo la Muleba Kaskazini, Adonis Bitegeko ameibuka mshindi kwenye kura za maoni za CCM kwa kumbwaga aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Mbunge wa muda mrefu, Dkt. Charles Mwijage. Ushindi huo umeweka historia mpya katika jimbo hilo, na kuongeza idadi ya vigogo waliotemwa kwenye mchakato wa ndani wa chama.

Haya ni baadhi ya majina ya wabunge walioshindwa kura za maoni. Kwa sasa, macho yote yanaelekezwa kwenye vikao vya juu vya CCM, ambavyo vina mamlaka ya mwisho ya kuidhinisha majina ya wagombea.

Hata hivyo, uamuzi wa wajumbe umetuma ujumbe mzito kwamba mabadiliko yanahitajika, na sura mpya zinaungwa mkono. Kwa waliokuwa wabunge waliokataliwa na wanachama wao, matumaini pekee yaliyobaki ni uamuzi wa huruma kutoka juu kama utakuwepo.

Je, vikao vya juu vitarejesha majina yaliyokataliwa na msingi wa chama, au vitaacha sauti ya wajumbe iwe sauti ya wananchi? Macho na masikio sasa yako Dodoma.
Ungeweka kwa mfumo wa pdf kuokoa muda.
 
nauliza matokeo ya bro diego armando maradona wa kusini?
 
WABUNGE WALIOSHINDWA

1. Deo Sanga - Makambako
2. Dr. Charles Kimei - Vunjo
3. Prof. Patrick Ndakidemi - Moshi Vijijini
4. Felister Njau - Moshi Vijijini
5. Ester Matiko - Tarime Mjini
6. Ester Bulaya - Bunda Mjini
7. Innocent Bilakatwe - Karagwe
8. Dr. Medard Kalemani - Chato
9. Mtenga - Mtwara Mjini
10. Cecilia Pareso - Karatu
11. Miraji Mtaturu - Ikungi Mashariki
12. Nustrat Hanje - Ikungi Mashariki
13. John Pallangyo - Arumeru Mashariki
14. Jesca Msambatavangu - Iringa Mjini
15. Dr. Amsabi Mrimi - Serengeti
16. Hawa Mwaifunga - Tabora Mjini
17. Issa Mtemvu - Kibamba
18. Issa Chinguile - Nachingwea
19. Hamida Abdallah - Lindi Mjini
20. Emmanuel Mwakasaka - Tabora Mjini
21. Eng. Stella Manyanya - Nyasa
22. Martin Msuha - Mbinga Vijijini
23. Joseph Kakunda - Sikonge
24. Asa Makanika - Kigoma Kaskazini
25. Constantine Kanyasu - Geita Mjini
26. Hanisi Kigwangala - Nzega Vijijini
27. Godfrey Pinda - Kavuu
Stanslaus Nyongo Naibu Waziri wa Mipango kaliwa kichwa huko Maswa
 
400M wala sio hela ndugu yangu, ndio maana wengine wanalia. Kumbuka kuna ambao wana madeni 😂😂😂😂
Wewe mtu kawekeza mabillion haoni shida yoyote ana kiinua mgongo tayari
 
Unapata kujua kwa kina habari ya kitu. Jifunze kusoma vitu kwa kina ujue chanzo sababu madhara na suluhisho na sio kupitia juu juu inaoenesha chief shule ulifeli sababu ulikua ubapitia definition unalala
Ndio mana wengi wa watu wanamlaumu putin anachofanya pale Ukraine sababu mnajua habari juu juu tu hamusomi vitabu mkajua chanzo cha mgogoro nikuulize bro ivi Ukraine akijiunga na nato then US na wake zake EU wakapeleka ICBM na nuclear pale mpakan warusi watakua na raha ya kuishi kweli wanajua wakijitekenya imekula kwao. Mwisho nakuusia jifunze kusoma vitu kwa kina kabla kutoa hukumu
 
Oya wenzio wanamiliki na mabillion punguza kejeli plus pension wanayopata baada ya kustaafu ubunge huwaambii kitu
Mkuu matumizi ni makubwa zote zimeishia kwenye madeni na kuonga wajumbe Uchaguzi ndani ya CCM ni gharama kubwa sana ili kupita kwenye mchujo zinatumika pesa nyingi sana, Tofauti na Wagombea wa vyama vya upinzani ndiyo Maana Mgombea Ubunge wa CCM akishindwa Ubunge na Upinzani anakua kapata Asala sana tofauti na mpinzani akishindwa Ubunge. Ndiyo Maana mpinzani kutangazwa kashinda Ubunge inakua ngumu sana.
 
Unapata kujua kwa kina habari ya kitu. Jifunze kusoma vitu kwa kina ujue chanzo sababu madhara na suluhisho na sio kupitia juu juu inaoenesha chief shule ulifeli sababu ulikua ubapitia definition unalala
Hadi dakika hii nadhani tayari imeonekana nani alifeli. Kilichokufelisha ilikuwa ni ujuaji
 
Ndio mana wengi wa watu wanamlaumu putin anachofanya pale Ukraine sababu mnajua habari juu juu tu hamusomi vitabu mkajua chanzo cha mgogoro nikuulize bro ivi Ukraine akijiunga na nato then US na wake zake EU wakapeleka ICBM na nuclear pale mpakan warusi watakua na raha ya kuishi kweli wanajua wakijitekenya imekula kwao. Mwisho nakuusia jifunze kusoma vitu kwa kina kabla kutoa hukumu
Wewe ujuaji ndio ulikuangusha. Still bado unaendelea nao
 
Takataka zilizokuepo bungeni msimu ulioisha wanaorudi hawazidi kumi..
 
This is keyboard mistake not mine
Acha kuisingizia key board, huo ni ujinga wako na kujifanya una haraka na ujuaji mwingi ilhali mbele kiza. Ingekuwa ume-type kwa lugha ya kiingereza text correction ingekusaidia. Kadri unavyozidi kujitetea ndio unazidi ku-expose the way kichwani kwako SIFURI
 
Back
Top Bottom