tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Kuna taarifa zimetapakaa hapa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba wabunge wote wa CCM wanaoikosoa serikali hadharani huenda wakaadhibiwa.
Inasemekana moja ya adhabu hizo ni kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi wa mkuu wa 2020 kwa lengo la kuwafutilia mbali katika ulingo wa siasa.
Adhabu ya pili inayopendekezwa ni kuwapoka nafasi za ujumbe katika halmashauri ya taifa ya CCM na ujumbe wa mkutano mkuu ili kuwaweka mbali zaidi na CCM.
Kada mmoja wa CCM aliyepo chamani na serikalini kwa muda mrefu alipoulizwa kuhusu tetesi hiz alijibu: "Ni kweli chama kina taratibu zake za kuisimamia serikali lakini sio kwa kuikosoa serikali hadharani. Hivyo, wana CCM wote wanaokosoa utendaji wa serikali hadharani sharti waadhibiwe...ila kwa sasa siwezi kukuambia aina ya adhabu tutakayowapa."
MAONI YANGU
Ikiwa kweli CCM itawaadhibu hawa wabunge wazalendo walioamua kusimama upande wa wananchi watakuwa wamefanya kosa kubwa sana. Elewa kwamba wana CCM wengi hawapendi uburuzwaji isipokuwa wanaogopa kusema ukweli kwa kuogopa kuadhibiwa na chama na serikali. Sasa endapo CCM na serikali wataamua kuwaadhibu watetezi hawa wa maslahi ya wananchi kwa namna yoyote, watajenga chuki mbaya sana mbele za wananchi.