Tetesi: Wabunge wa CCM wanaoikosoa serikali kuadhibiwa

Tetesi: Wabunge wa CCM wanaoikosoa serikali kuadhibiwa

Hichi chama hakipo kwajili ya kuwasaidia wananchi wahanga wa tetemeko kagera wanalala nje nakuambiwa wajenge nyumba zao wenyewe wakati mashirika yametoa pesa nyingi kwajili ya wahanga hao hapo hapo hichi chama kinawapa wabunge wake milioni kumi kumi kama rushwa tena kwa siri tujiulize je ni watetezi kweli wa wanyonge kama wanavyojinadi au niwanafki?
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi bashe aliwahi kusema hamuungi mkono jmp wakati wa kampeni kwahyo siyo ajabu kiona Leo hii anasimama ni kutoa hoja pinzani
 
Makanjanja wa Tanzania kwa udaku wa uzushi mnajiweza .
 
Sasa wao wanaikosoaje,wapinzani watafanya nini sasa,ssi huku tushazoea kusifia tu hata kama ni kinyes aa huwa ni ndiooooo
 
Hii ni awamu ya ukweli na uwazi wacha wabunge hata wa ccm wafunguke wasikubali kuburuzwa
 
Hao wabunge ni wanafiki. Kama leo umesikiliza mazungumzo ya rais na wahariri utakubaliana na mimi hao ni wabunge maslahi. Hivi inaingia akilini shirika kama NDC, hela zake linaweka CRDB na tena kwa fixed deposit, CEO anapata 10 percent ya faida ya fixed deposit, then serikali inaamua kukopa/kuuza T bills, then bank kutumia hizo hizo za serikali inaenda kuikopesha serikali na serikali inakuja kulipa hizo hela na riba juu yake.
Hizi ngonjera zenu zinachosha masikioni. Huyo CEO kama anachokifanya ni kosa la jinai kwanini msimkamate badala ya kufanya mambo ambayo yana athari kubwa katika uchumi? Msifanye maamuzi kwa kuongozwa na roho mbaya tu!
 
Hivi kumbana waziri atekeleze majukumu yake, au kuisimamia serikali isiharibu uchumi kwa mfano, huko ndiyo kupingana na sera za ccm, basi ni bora tusiwe na CCM kabisa.
Ukiwa wewe hukubaliani na sera ya chama chako ni vizuri zaidi ukajiuzulu katika nafasi hiyo badala ya kuwa chui uliyevaa ngozi ya kondoo.
Chama kitakuamini vipi kwenye mikutano ya ndani kama wewe ni msaliti.
 
Hivi kumbana waziri atekeleze majukumu yake, au kuisimamia serikali isiharibu uchumi kwa mfano, huko ndiyo kupingana na sera za ccm, basi ni bora tusiwe na CCM kabisa.
mkuu, kwa wanaCCM, ni chama kwanza...nchi baadaye! Inasikitisha sana I see.
 
Back
Top Bottom