Tetesi: Wabunge wa CCM wanaoikosoa serikali kuadhibiwa

Tetesi: Wabunge wa CCM wanaoikosoa serikali kuadhibiwa

Ni mbaya sana kutumikia mabwana wawili, by the way katibu Mkuu slaa alipokosoa chama chake wale Jamaa walisemaje vile, walimtukana matusi yote mpaka babu kahama nchi, Leo wanamshabikia bashe kutukana chama chake! Unamtukana dr. Mpango kiasi kile! Ccm mdhibitini huyu faster msimcheleweshe kama mamvi tujifunze kutokana na makosa
Hizo style kwa sasa hazifanyi kazi hata mkiamua kumkomoa atahama chama na ubunge kwake sio issue kwani hana njaa ataishi hata kwa michango ya wapiga kura
 
Swala la chama kuwaadhibu wanachama wanakikosoa chama hadharani .......

Sioni tofauti kati ya CCM Na Chadema.!
 
Kwa hiyo ukiwa mbunge lazima uwe na maneno ya akiba,kwamba ukiikosoa serikali hadharani unaingia matatani,kwa hivyo kuwa mbunge hasa wa ccm unatakiwa ujitie upofu,uone aibu,uwe na maneno ya kusema mengine upige kimya,uwe kama hazikutoshi vile ovyo sana.Hii nchi kuna mashetani kila kona.
Yaani wanataka ukiwa Mbunge wa CCM uwe mjinga mjinga kama Goodlack kombani, CCM hawataki wabunge wakweli wapenda haki na maendeleo bali wanataka wabunge wanafiki wajinga wajinga kama Agnes marwa na wenzao:
 
Hao wabunge ni wanafiki. Kama leo umesikiliza mazungumzo ya rais na wahariri utakubaliana na mimi hao ni wabunge maslahi. Hivi inaingia akilini shirika kama NDC, hela zake linaweka CRDB na tena kwa fixed deposit, CEO anapata 10 percent ya faida ya fixed deposit, then serikali inaamua kukopa/kuuza T bills, then bank kutumia hizo hizo za serikali inaenda kuikopesha serikali na serikali inakuja kulipa hizo hela na riba juu yake.
Sasa serikali ikiziondoa pesa huko ndiyo utakuwa mwisho wa kukosa! ?

By the way, siyo mabank tu yanayonunua Treasury Bills!!
 
Hao wabunge ni wanafiki. Kama leo umesikiliza mazungumzo ya rais na wahariri utakubaliana na mimi hao ni wabunge maslahi. Hivi inaingia akilini shirika kama NDC, hela zake linaweka CRDB na tena kwa fixed deposit, CEO anapata 10 percent ya faida ya fixed deposit, then serikali inaamua kukopa/kuuza T bills, then bank kutumia hizo hizo za serikali inaenda kuikopesha serikali na serikali inakuja kulipa hizo hela na riba juu yake.
Tunauwakika gani na hiyo taarifa nani wa kuhoji kama yaliyosema ni kweli au sikweli
 
Tumbua kabisa itisha uchaguzi upya tu hakuna namna.
 
Kuna taarifa zimetapakaa hapa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba wabunge wote wa CCM wanaoikosoa serikali hadharani huenda wakaadhibiwa.

Inasemekana moja ya adhabu hizo ni kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi wa mkuu wa 2020 kwa lengo la kuwafutilia mbali katika ulingo wa siasa.

Adhabu ya pili inayopendekezwa ni kuwapoka nafasi za ujumbe katika halmashauri ya taifa ya CCM na ujumbe wa mkutano mkuu ili kuwaweka mbali zaidi na CCM.

Kada mmoja wa CCM aliyepo chamani na serikalini kwa muda mrefu alipoulizwa kuhusu tetesi hiz alijibu: "Ni kweli chama kina taratibu zake za kuisimamia serikali lakini sio kwa kuikosoa serikali hadharani. Hivyo, wana CCM wote wanaokosoa utendaji wa serikali hadharani sharti waadhibiwe...ila kwa sasa siwezi kukuambia aina ya adhabu tutakayowapa."

MAONI YANGU
Ikiwa kweli CCM itawaadhibu hawa wabunge wazalendo walioamua kusimama upande wa wananchi watakuwa wamefanya kosa kubwa sana. Elewa kwamba wana CCM wengi hawapendi uburuzwaji isipokuwa wanaogopa kusema ukweli kwa kuogopa kuadhibiwa na chama na serikali. Sasa endapo CCM na serikali wataamua kuwaadhibu watetezi hawa wa maslahi ya wananchi kwa namna yoyote, watajenga chuki mbaya sana mbele za wananchi.

Hii basi itakuwa ni kuwaonea.
Maana Katibu mkuu wa CCM Kinana baada ya ushindi wa CCM alifanya kikao ama semina elekezi na wabunge wote wa chama tawala mjini Dodoma na akasema nami namnukuu:

"Msiogope kukosoa wakati mnaona kuna makosa. Myazungumze wazi bila woga. Na katika maamuzi ya chama msimame pamoja kama wana CCM" Mwisho wa kunukuu!

Hivyo basi kuwaadhibu wabunge wa CCM wanayoyatoa moyoni nikuwaonea.Na si hivyo tu bali pia ni kuikandamiza demokrasia na uhuru wa kujieleza. Hilo wacheni!
 
No UOTE="Ngamanya Kitangalala, post: 18346976, member: 103078"]Kila chama duniani kila taratibu zake
Huwezi kukosoa chama chako hadharani
Kuna carcus ya chama, huko ndio mahala kwa kukosoa
Wanastahiri adhabu[/QUOTE]
No wonder 50 yrs plus chama hiki kimebaki na sifa kuu ya kuwa chama Kikongwe na si kuwakomboa wananchi wake, hata pini na wembe wanaagiza, mosquito net pia ni kwa msaada wa fulani. Sasa angalia wanavyoshika akili za wabunge wake. Very funny ni kwamba wabunge hao hao, hata baada ya kulishwa maneno na hiyo bado wengi wametupwa nje kwenye elections. My advice simamieni mnachoamini hata kama mtadumu kipindi kimoja, in fact wananchi wakikukubali hata ukitemwa kimizengwe utarudi tuu mjengoni kwa mlango mwingine.
 
"EI INCUMBIT PROBATIO QUI DECIT,NON QUI NEGAT"

Mkuu si wote tunajua legal maxim phrase ya criminal law utuandikie Kilatini (Latin)Andika Kibongo bana!
Hata hivyo wacha niwasidie wana JF
Ina maanisha kuwa:
"Mzigo wa UHALISIA wa jambo u juu yake mwenye KUUHAKIKI si yule AKANAYE"
 
Ndiyo sababu wamepewa kufuta jasho cha Milioni kumi kumi
hivi nchi inavyolia ukata kila kukicha dr makufuri anapata wapi guts za kuchota hela za umma na kuwagawia wachumia tumbo wa CCM? ama kweli huyu anahitaji maombezi!
 
kuna mmeanza kusema leo kusema kuadhibiwa??na mpaka leo hakuna kitu,labda muanze kutuambiwa adhabu gani alipewa bashe alipokua anaikosoa serikali katika mjadiliano ya bajeti??
mkuu soma uzi kwanza kabla ya kuchangia...haya ndiyo madhara ya kusoma heading na kuanza kuchangia kiupofu pasipo kuielewa mada.
 
mkuu soma uzi kwanza kabla ya kuchangia...haya ndiyo madhara ya kusoma heading na kuanza kuchangia kiupofu pasipo kuielewa mada.
nmeusoma uzi na nimeuelewa na huu si uzi wa kwanza kuja kwa style hii,hata kipindi cha bajeti uzi kama huu ulikuwepo sioni jipya hapooo
 
Bashe Akija CHADEMA pale Nzega ndio wasahau, CCM haitashinda pale miaka 15
 
Back
Top Bottom