Tetesi: Wabunge wa CCM wanaoikosoa serikali kuadhibiwa

Tetesi: Wabunge wa CCM wanaoikosoa serikali kuadhibiwa

CCM tuna sheria moja tu, ss ni wa kijani na lazma wote tufanane. Sasa hao kina Bashe wataisoma tu hamna namna
Kuna wengine wameji-BRAND wenyewe kwenye majimbo yake na siyo chama.... Ndiyo maana kuna wengine hata wakihama chama, bado wanshinda tu... Tmeshuhudia akina
1. Zitto Kabwe
2. Shibuda alikuwa hivyo
na wengine wengi...
Sasa mkitaka kupoteza majimbo wanyimeni nafasi ya kugombea halafu wakihama ndo mtajuwa
 
Namuamini kwa 100%%%%%%%%%%%. Inamaana wewe bado unamuamini Mbowe? Yaani pamoja na uongo na unafiki wake woote wewe unamuamini??
weka siasa kando dada mudawote najua upo lumumba unalipwa buku zako 7, kuwa na huruma na walalahoi, wao wanaiokosoa serikali sio kwamba wana njaa, tizama chumbuko lao lakini wana huruma na wananchi waliowachagua, wekeni siasa pembeni hapo ndo tutasonga lakini kila kitu mkiingiza siasa, hatutafika popote, ushauri tu nakupa
 
Kuna taarifa zimetapakaa hapa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba wabunge wote wa CCM wanaoikosoa serikali hadharani huenda wakaadhibiwa.

Inasemekana moja ya adhabu hizo ni kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi wa mkuu wa 2020 kwa lengo la kuwafutilia mbali katika ulingo wa siasa.

Adhabu ya pili inayopendekezwa ni kuwapoka nafasi za ujumbe katika halmashauri ya taifa ya CCM na ujumbe wa mkutano mkuu ili kuwaweka mbali zaidi na CCM.

Kada mmoja wa CCM aliyepo chamani na serikalini kwa muda mrefu alipoulizwa kuhusu tetesi hiz alijibu: "Ni kweli chama kina taratibu zake za kuisimamia serikali lakini sio kwa kuikosoa serikali hadharani. Hivyo, wana CCM wote wanaokosoa utendaji wa serikali hadharani sharti waadhibiwe...ila kwa sasa siwezi kukuambia aina ya adhabu tutakayowapa."

MAONI YANGU
Ikiwa kweli CCM itawaadhibu hawa wabunge wazalendo walioamua kusimama upande wa wananchi watakuwa wamefanya kosa kubwa sana. Elewa kwamba wana CCM wengi hawapendi uburuzwaji isipokuwa wanaogopa kusema ukweli kwa kuogopa kuadhibiwa na chama na serikali. Sasa endapo CCM na serikali wataamua kuwaadhibu watetezi hawa wa maslahi ya wananchi kwa namna yoyote, watajenga chuki mbaya sana mbele za wananchi.
CCM hawaachiani maji mezani - Kikwete .
 
Ukiwa wewe hukubaliani na sera ya chama chako ni vizuri zaidi ukajiuzulu katika nafasi hiyo badala ya kuwa chui uliyevaa ngozi ya kondoo.
Chama kitakuamini vipi kwenye mikutano ya ndani kama wewe ni msaliti.
 
Kila chama duniani kila taratibu zake
Huwezi kukosoa chama chako hadharani
Kuna carcus ya chama, huko ndio mahala kwa kukosoa
Wanastahiri adhabu

BADO UNA MENGI YA KUJIFUNZA, NI BORA KUKAA KIMYA KULIKO KUONGEA JAMII IKAJUA UDHAIFU WAKO.
 
Ukiwa wewe hukubaliani na sera ya chama chako ni vizuri zaidi ukajiuzulu katika nafasi hiyo badala ya kuwa chui uliyevaa ngozi ya kondoo.
Chama kitakuamini vipi kwenye mikutano ya ndani kama wewe ni msaliti.
Kumbe SERA za chama cha CCM ni kukandamiza haki na maslahi ya wananchi. Afadhali leo umenijuza mkuu.
 
kuna mmeanza kusema leo kusema kuadhibiwa??na mpaka leo hakuna kitu,labda muanze kutuambiwa adhabu gani alipewa bashe alipokua anaikosoa serikali katika mjadiliano ya bajeti??
 
Hao wabunge ni wanafiki. Kama leo umesikiliza mazungumzo ya rais na wahariri utakubaliana na mimi hao ni wabunge maslahi. Hivi inaingia akilini shirika kama NDC, hela zake linaweka CRDB na tena kwa fixed deposit, CEO anapata 10 percent ya faida ya fixed deposit, then serikali inaamua kukopa/kuuza T bills, then bank kutumia hizo hizo za serikali inaenda kuikopesha serikali na serikali inakuja kulipa hizo hela na riba juu yake.
Haya maajabu sana CEO akiharibu mnahamisha hela na Gavana akiharibu mtahamishia reserve bank ya wapi?

Nyani wakivamia shamba utafyeka mazao? Au utawafyeka nyani?
 
Ni mbaya sana kutumikia mabwana wawili, by the way katibu Mkuu slaa alipokosoa chama chake wale Jamaa walisemaje vile, walimtukana matusi yote mpaka babu kahama nchi, Leo wanamshabikia bashe kutukana chama chake! Unamtukana dr. Mpango kiasi kile! Ccm mdhibitini huyu faster msimcheleweshe kama mamvi tujifunze kutokana na makosa
 
huwezi ukawa mbunge wa ccm halafu ukawatumikia wananchi kwa haki kamwe. kwa ccm chama kwanza kisha nchi....
 
Kuna taarifa zimetapakaa hapa mitaani na kwenye mitandao ya kijamii kwamba wabunge wote wa CCM wanaoikosoa serikali hadharani huenda wakaadhibiwa.

Inasemekana moja ya adhabu hizo ni kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi wa mkuu wa 2020 kwa lengo la kuwafutilia mbali katika ulingo wa siasa.

Adhabu ya pili inayopendekezwa ni kuwapoka nafasi za ujumbe katika halmashauri ya taifa ya CCM na ujumbe wa mkutano mkuu ili kuwaweka mbali zaidi na CCM.

Kada mmoja wa CCM aliyepo chamani na serikalini kwa muda mrefu alipoulizwa kuhusu tetesi hiz alijibu: "Ni kweli chama kina taratibu zake za kuisimamia serikali lakini sio kwa kuikosoa serikali hadharani. Hivyo, wana CCM wote wanaokosoa utendaji wa serikali hadharani sharti waadhibiwe...ila kwa sasa siwezi kukuambia aina ya adhabu tutakayowapa."

MAONI YANGU
Ikiwa kweli CCM itawaadhibu hawa wabunge wazalendo walioamua kusimama upande wa wananchi watakuwa wamefanya kosa kubwa sana. Elewa kwamba wana CCM wengi hawapendi uburuzwaji isipokuwa wanaogopa kusema ukweli kwa kuogopa kuadhibiwa na chama na serikali. Sasa endapo CCM na serikali wataamua kuwaadhibu watetezi hawa wa maslahi ya wananchi kwa namna yoyote, watajenga chuki mbaya sana mbele za wananchi.
uongo mfu wa bawacha
 
Namuamini kwa 100%%%%%%%%%%%. Inamaana wewe bado unamuamini Mbowe? Yaani pamoja na uongo na unafiki wake woote wewe unamuamini??
Kwa hiyo ukiwa mbunge lazima uwe na maneno ya akiba,kwamba ukiikosoa serikali hadharani unaingia matatani,kwa hivyo kuwa mbunge hasa wa ccm unatakiwa ujitie upofu,uone aibu,uwe na maneno ya kusema mengine upige kimya,uwe kama hazikutoshi vile ovyo sana.Hii nchi kuna mashetani kila kona.
 
Karibuni ukawa tujenge nchi ya maziwa na asali
 
Kila chama duniani kila taratibu zake
Huwezi kukosoa chama chako hadharani
Kuna carcus ya chama, huko ndio mahala kwa kukosoa
Wanastahiri adhabu
Yaani hata wakifanya mambo ya ajabu wasikosolewe? Mbona magufuli kasema leo kuna wana CCM wana mambo ya hovyo kuliko hata Wapinzani huko si kukosoana hadharani?
 
Back
Top Bottom