Wabunge wa Kigoma tumieni fursa - Kigoma bado imefungwa

Wabunge wa Kigoma tumieni fursa - Kigoma bado imefungwa

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Wabunge wa Mkoa wetu wanafahamu kutumia fursa za kiuongozi?

OMR ndiyo yenye dhamana na masuala ya mazingira nchini. Sasa Je tumeitumia vema Ofisi ya Mhe Isdory Mpango - Makamu wa Rais katka eneo hili la mazingira??

Je, Mhe Isdory Mpango (Makamu wa Rais) mwenyewe ameelekeza watendaji wake ktk Mkoa Kigoma ili kuneemesha wadau wa mazingira kwenye miradi ya Carbon credit inayotoa bonus ya tzs 87 kwa kila mche wa mti uliopandwa?

Je Waheshimiwa Wabunge wanatambua kuwa Mhe Isdory Mpango - Makamu wa Rais ni fursa, na wanatumia mwanya huo kumkumbusha ktk miradi ya utunzaji mazingira? Tuamke kazi ipate kuendelea!

Note:
Twaweza kuwa na fursa lkn mwisho wa siku tukabaki maskini wa kutupwa kwa kutozitambua na kuzitumia.

Msakila Kabende
Kakonko
 
Back
Top Bottom