Wabunge wa Tanzania wajue sio kila jambo linalohusu usalama wa nchi ni la kutolewa ufafanuzi kwa wanasiasa


Kupinga utawala? Means you go against authority na unataka muachwe mfanye mtakavyo?

Huo ni uhaini tayari.
 
Wewe lazima utakuwa miongoni mwa wale wanaotakiwa wakauze maandazi
 
Mkuu Infantry Soldier, hutokea sana viongozi waovu kujificha ndani ya usalama wa taifa.

Wakiiba watasema ni hela zilizo tumika kwenye mambo ya usalama. Baasi, wamemaliza

Kuna mambo umeandika ni sawa lakin kuna wadau wameweka hapo juu ni sawa pia.
Besaa8 alikomaa juu ya PhD ya magu. Akatoweka. Kama alitoweshwa na usalama ni kwanin? Kutisha wengine kama Ben? Kumlinda mkuu dhidi ya aibu ya kukopi kazi za wengine? Kumpunguzia mkuu na presha ya kufuatilia Ben leo kasema nin, na badala yake ajikite kuendesha nchi?

Maneno ya Ben yalikuwa ya ndani sana ukiwa na akili Huru usingeweza kuya dharau. Na hakukuwa na hoja zozote imara au za kujitosheleza kuzikabili hoja za Ben. Na wabongo tunajuana. Uwezo wetu wengi tunajuana. Na kwa mwanasiasa kama Magu kufanya kazi ile ilikuwa issue. Hapa mim nahitimisha kuwa kwa kinachoitwa usalama wa nchi huenda kweli jamaa alipotwezwA ili 'kumsaidia mkuu '. Na je, kumsaidia mkuu ni kusaidia nchi? Unaweza kusema ndio

Kuna maufisadi mengi ambayo watu wakifuatilia hupata shida. Shida zinaweza kutoka kwa vyombo vya dola au hata vikundi vya kiovu.

Magufuli husemwa juu kivuko kibovu. Mwandish au mtu mwingine akiamua kufuatilia vyombo vya dola vikimvuruga tutasemaje hapo? Viongozi hutumia vyombo vya dola ki ovyo sana. Hutumia kulinda maovu yao. Halafu baadae husingizia usalama wa nchi

Mapungufu ya viongozi hufichwa kwa nguvu kubwa mno. Na wao kwa kujua hilo hujifanyia hata ya ovyo bila kujali. Laiti vyombo vya dola vingekuwa haviwapi kashikashi wanao hoji huenda viongozi wetu wangekuwa makini kwa wayafanyayo. Lakin sasa wana jivurugia vurugia tu

Mwaka huu wataelekeza mabilioni kuzalisha umeme kwa njia ya gesi. Miaka mitatu baadae wataelekeza matrilioni kuzalisha umeme kwa njia ya maji. Na hapo katikat hakuna maelezo yoyote ya kwa nin umeme wa gesi ni kama hatuendelei nao. Wanajua hakuna wa kuuliza. Atayeanza kuuliza uliza anatoweshwa fasta kama Ben.

Na hii tabia huambukiza hata watendaji wa chini serikalin na kwenye taasisi za umma Kama juu hawatoi maelezo yoyote kwanin wa chin watoe.

Mwisho wa siku ofisi za umma zinaendeshwa kama mali binafsi

Acheni kusingizia usalama wa nchi Kuficha madhaifu yenu
 
Umeongea hivyo kwa vile hao 380 wanaodaiwa kupotea sio baba, mama ako na ndugu zako.
Kumbuka kua mnayowafanyia Watanzania ipo siku yatawafika.
Mana saizi mmekamata vyombo vyote vya habari ili uovu wenu usijulikane. Sawa, ila Mungu si dhalimu.
 
Kwenye nchi isiyotofautisha usalama wa taifa na maslahi ya kisiasa ya rais/chama tawala; nchi ambayo teuzi katika vyombo vya dola zinafanywa kisiasa na amri za rais zinatekelezwa bila kuhojiwa, “classified information” hazina tofauti na siri za kimafia.
 
Mtoa huu uzi kwa maandishi yake tu, itoshe kumjua ni mmoja wa waunga mkono wa utekaji na uuwaji wa watu wasiyo na hatia Nchini! Aina ya watu wa hivi, siyo wa kuwafurahia kbsa, Akili zao zimejikita ktk umwagaji damu kwa ghalama yoyote ilimradi ni kuulinda utawala dharimu. Mifano unayoitoa kutoka CHINA ni mwendelezo ule ule wakutuonesha ulivyokatili! China ni Nchi ya kutolea mfano!? Hii Nchi kidemokrasia haiko salama, ugandamizaji na uuwaji kwa wale wanaoikosoa Serikali, ni kipao mbele chao cha kudumu. Swala hapa ni kwamba, Serikali ya CCM, iachane na utawala wa chuma, iache kuua watu hovyo! Siasa za kigaidi zilishapitwa na wakati, wawaachie kazi hiyo Al-shabab, Al-Quida na Boko haram. Ni aibu kubwa kuona Nchi iliyohuru na kihistoria ilikuwa na Rais aliyepinga Dunia nzima mauwaji ya wanadamu kiholela ssa ndiyo inajipanga kuwa Nchi ya umwagaji Damu tena kwa Raia wake wenyewe, hii ni laana kubwa!
 
Infantry soldier ,Una utashi kama wangu,you surpassed tactical points.
Anaelewa atakuwa ameelewa ,naomba uwe unanitagi pia kwenye hizi maada.
Mengine tubishane tu ila kwenye usalama wa Tz Yangu nipo rigid ,
Naipenda Nchi Yangu.
Usalama dhidi ya nani na kwa manufaa ya nani?!
Tz ni ya waTz wote, tukubaliane namna bora ya kuongozana na si kutawalana kikoloni!!. Isije kuwa kwa sababu tu mtu haipendi CCM, basi kawa threat kwa taifa. Hapana
 
Kupinga utawala? Means you go against authority na unataka muachwe mfanye mtakavyo?

Huo ni uhaini tayari.
Kupinga watawala ipo kikatiba. Na ndiyo maana kuna kambi rasmi ya upinzani bungeni !!!. Unaweza ukaipinga serikali na chama tawala, lakini bado ukawa mzalendo wa dhati kwa taifa lako !!
 
 
Mi nashangaa baadhi yenu mmemezeshwa maneno hata ukiulizwa leo una maanisha nini huna hata cha kujieleza..embu tuambie hivi nchi haina sheria zilizotungwa na bunge..? Kama unaambiwa usiandamane kwa sababu kuna viashiria vya uvunjifu wa amani kwanini unalazimisha..
Haya embu tuambie unaupinga utawala huu kwa lipi hasa, tueleze sababu makini za kutetea hoja yako..na hasa kwa jinsi utawala huu unavyojitahidi kupambana na mafisadi
 
Gaidi au mhalifu haitaji kubembelezwa...walipouawa viongozi wa chama na Serikali sikuwaona hapa mkilaani sanasana mlisema acha wakomeshwe ....Jeshi limeenda kuwakomesha wahusika na sasa pako shwari ndio mnaanza kutuletea porojo za haki za binadamu.
Dawa ya terror ni more TERROR ....ndio maana Kibiti,Arusha,Amboni na kwingineko pametulia.
 
Gaidi au mhalifu haitaji kubembelezwa...walipouawa viongozi wa chama na Serikali sikuwaona hapa mkilaani sanasana mlisema acha wakomeshwe ....Jeshi limeenda kuwakomesha wahusika na sasa pako shwari ndio mnaanza kutuletea porojo za haki za binadamu.
Dawa ya terror ni more TERROR ....ndio maana Kibiti,Arusha,Amboni na kwingineko pametulia.
 
Gaidi au mhalifu haitaji kubembelezwa...walipouawa viongozi wa chama na Serikali sikuwaona hapa mkilaani sanasana mlisema acha wakomeshwe ....Jeshi limeenda kuwakomesha wahusika na sasa pako shwari ndio mnaanza kutuletea porojo za haki za binadamu.
Dawa ya terror ni more TERROR ....ndio maana Kibiti,Arusha,Amboni na kwingineko pametulia.
 
Huyu mjinga aliyeandika siku moja mke wake atekwe na apigwe mande mbele yake ndiyo atajua uchungu wa mwana aijuae mzazi
Kwani wale watekaji wa Kibiti walikuwa wanafanyaje?
 
Usinipangie... kwa maana sina mkataba na wewe wala na yeyote wa kusoma ninachoandika!

Jadili mada iliyopo mezani
 
Siku hizi umekua na akili za kipuuzi sana!! Huna hoja, huna mada zenye akili tena!! Umebaki kutetea upumbafu... Kwa kifupi umekua bure kabisa!!

Kwa mamlaka niliyonayo nimeamua kukupuuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…