Mkuu
Infantry Soldier, hutokea sana viongozi waovu kujificha ndani ya usalama wa taifa.
Wakiiba watasema ni hela zilizo tumika kwenye mambo ya usalama. Baasi, wamemaliza
Kuna mambo umeandika ni sawa lakin kuna wadau wameweka hapo juu ni sawa pia.
Besaa8 alikomaa juu ya PhD ya magu. Akatoweka. Kama alitoweshwa na usalama ni kwanin? Kutisha wengine kama Ben? Kumlinda mkuu dhidi ya aibu ya kukopi kazi za wengine? Kumpunguzia mkuu na presha ya kufuatilia Ben leo kasema nin, na badala yake ajikite kuendesha nchi?
Maneno ya Ben yalikuwa ya ndani sana ukiwa na akili Huru usingeweza kuya dharau. Na hakukuwa na hoja zozote imara au za kujitosheleza kuzikabili hoja za Ben. Na wabongo tunajuana. Uwezo wetu wengi tunajuana. Na kwa mwanasiasa kama Magu kufanya kazi ile ilikuwa issue. Hapa mim nahitimisha kuwa kwa kinachoitwa usalama wa nchi huenda kweli jamaa alipotwezwA ili 'kumsaidia mkuu '. Na je, kumsaidia mkuu ni kusaidia nchi? Unaweza kusema ndio
Kuna maufisadi mengi ambayo watu wakifuatilia hupata shida. Shida zinaweza kutoka kwa vyombo vya dola au hata vikundi vya kiovu.
Magufuli husemwa juu kivuko kibovu. Mwandish au mtu mwingine akiamua kufuatilia vyombo vya dola vikimvuruga tutasemaje hapo? Viongozi hutumia vyombo vya dola ki ovyo sana. Hutumia kulinda maovu yao. Halafu baadae husingizia usalama wa nchi
Mapungufu ya viongozi hufichwa kwa nguvu kubwa mno. Na wao kwa kujua hilo hujifanyia hata ya ovyo bila kujali. Laiti vyombo vya dola vingekuwa haviwapi kashikashi wanao hoji huenda viongozi wetu wangekuwa makini kwa wayafanyayo. Lakin sasa wana jivurugia vurugia tu
Mwaka huu wataelekeza mabilioni kuzalisha umeme kwa njia ya gesi. Miaka mitatu baadae wataelekeza matrilioni kuzalisha umeme kwa njia ya maji. Na hapo katikat hakuna maelezo yoyote ya kwa nin umeme wa gesi ni kama hatuendelei nao. Wanajua hakuna wa kuuliza. Atayeanza kuuliza uliza anatoweshwa fasta kama Ben.
Na hii tabia huambukiza hata watendaji wa chini serikalin na kwenye taasisi za umma Kama juu hawatoi maelezo yoyote kwanin wa chin watoe.
Mwisho wa siku ofisi za umma zinaendeshwa kama mali binafsi
Acheni kusingizia usalama wa nchi Kuficha madhaifu yenu