Wabunge wa Tanzania wajue sio kila jambo linalohusu usalama wa nchi ni la kutolewa ufafanuzi kwa wanasiasa

Hivi swala la watu kupotea na kuuwawa ni classfied!? Tunaongea hivyo labda kwa sababu wale walopatwa na maafa hayo si ndugu zako. Lakini ingekuwa ni wapendwa wako sidhani kama ungeliona classfied.
Na vip kama wale waliokuwa wanauwawa kwa kupigwa risasi kila siku wangekuwa ndugu zako?
 
Kwahiyo kupiga watu risasi na kuwaua bila kuthibitisha kwamba wanahusika ndo amani hiyo?!

Hongera kwa kuwa mfuasi mtiifu ambayo baada ya kushindwa kupambana na rushwa imegeuka kuwa ya kufanya mauaji bila kuthibitisha hatia!

Binafsi ningejisikia aibu kuwa mfuasi kindakikindaki wa serikali "iliyochaguliwa" huku ikitekeleza hukumu zake sawa na wanavyofanya Magaidi hatari duniani!

Hata Beberu Kuu Marekani, huwa anakamata Magaidi hatari kabisa, kuwahoji na kuwapeleka Guantanamo ili mradi tu wajiridhishe ikiwa wanahusika na tuhuma tajwa!

Tena basi wanafanya haya kwa watu ambao majority wala sio raia wake!

Na hata walio raia wake; majority wala sio raia wa asili but still they wanafahamu huwezi kukamata mtu na kummiminia mvua ya risasi simply because taarifa za kiusalama zilimtilia shaka mhusika au mhusika alitajwa!!

Na ndio maana haikushangaza kuona kwamba miongoni mwa waliotajwa hawakuwa na hatia na hivyo kuachiliwa huru!

Kinyume chake leo tuna serikali ambayo mtu kutajwa tu inatosha kupewa hukumu ya kifo bila hata ya kufanya intensive investigation!!

Mungu awalaani wote wanaotetea ushenzi na udhalimu kama huu kwa sababu yoyote ile!

Wananchi wanalipa kodi ili majeshi yetu yaweze kulipwa mishahara ili hatimae watumie weledi wao kuhakikisha haki inatendeka!

Unapokuwa na majeshi yanayofanya kazi kwa staili ile ile inayofanywa na Magaidi then hapawezi kuwa na tofauti kati ya Magaidi na askari wanaolipwa ili kulinda Wananchi!!

Kwa hakika nchi inahitaji maombi!
Hao yamkini ni wale unao waona je unajua kwenye operation zao ni wangapi wanauwawa?
Unajua mpaka wampate huyo gaidi ni wangapi wanakuwa wameshapitiwa.na mkono wa moto?
 
UTANGULIZI
=======
Baada ya tukio la September 11 mwaka 2001, aliyekiwa director wa CIA kwa wakati huo aliitwa mbele ya bunge la marekani na kuhojiwa na bunge.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kuwa kuna uhusiano gani wa kiutendaji wa kazi kati ya idara ya ujasusi ya jeshi (Military Intelligence) na CIA katika kuzuia matukio ya uhalifu na kigaidi kutokea ndani ya marekani. CIA director alitoa jibu moja tu kwa kusema "that information is classified" baaaas hakuendelea tena. Not every aspect of state security should be clarified to politicians

MAONI YANGU BINAFSI KUHUSIANA NA SUALA LA KUCHUKUA WATU MATEKA WITH REFERENCE TO CHINA.
=============
Si kila mwenye uraia wa China ni mtu salama kwa maslahi mema na ustawi wa nchi hiyo.

Nchi ya China ina maadui wa ndani pamoja na nje wanaopanga mipango ya kuidhoofisha kila saa na kila dakika. Hivyo ni kazi ya vyombo vya dola kuwatambua na kuwadhoofisha kama sio kuwamaliza kabisa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Huyo mtu adui anaweza kuwa hata ni ndugu yangu mimi au ndugu yako wewe wa karibu lakini mimi na wewe tusiwajue ila wataalam wa mambo ya usalama wa nchi husika wakawajua mpaka njama zao.

Hivyo suala la watu kuchukuliwa mateka na kuhojiwa kwa nchi kama China ni kitu kisichoepukia kwa nchi kutaka kujilinda na kusonga mbele.

Hizo nchi mnazoziona zimeendelea na mnahisi zina viwango vya juu sana vya haki za binadamu na demokrasia kama Marekani, German, Uingereza na hata Japan zipo katika kiwango hicho cha maendeleo si kwa bahati mbaya. Hapana. Idara zao za usalama ni wakali sana. Unafikiri hawafanyiwi hujuma hao jamaa? Unafikiri serikali zao hazina vikosi za kuchukua mateka (abduction squads)??? Wanavyo. Tena wapo very sophisticated, equipped with modern weaponry and techniques.

Nchi ya China ina maadui wanaofanya kazi muda wote kutaka kuihujumu politically, economically hata socially pia (kueneza mienendo itakayoweza kupelekea mmomonyoko wa maadili hata kuua uzalendo miongoni mwa watanzania kama nyimbo za kuua uzalendo kwa vijana zinawezekana ni brainwashing song kwa vijana ili kuhujumu akili zao kwa manufaa ya baadae) na maadui hao wanaweza kuwa ni watu wenye uraia wa China (walio ndani na nje) ama wasio wa China (walio ndani na nje ya nchi) wanaotaka kuwatumia raia wa China kudhoofisha nchi yao pasipo wao raia kujua ama kwa kujua na kuwapa rushwa na wapo ndani pia nje ya nchi ya China.

Kwa hiyo issue ya abduction squads ipo hata marekani na uingereza na ni muhimu sana kwa nchi kujilinda, sembuse China.

Police hawapaswi kuwa wapole. Tofautisheni vituo vya police na nyumba za ibada. Police kuwa wakali inasaidia hata mtu akitaka kutenda kosa lazima awaze mara mbili mbili itakuwaje kama akipelekwa police hivyo ana ahirisha kutenda uhalifu.

Sipo JF kufurahisha. Nipo hapa kufafanua ninayoyajua akilini mwangu.

I STAND TO BE CORRECTED.

KIJANA KUWA MZALENDO, PENDA TANZANIA.

TOFAUTI NI KWAMBA HAKUNA MTU ANAYETAKA KUJUA SIRI ZA SERIKALI ILA WATU WANATAKA HAKI ITENDEKE. KWA MFANO, KAMA SERIKALI INAMTUHUMU BEN SAANANE KWA KUFANYA BIASHARA HARAMU INGESEMA WAZI KWAMBA ANATAFUTWA NA POLISI. NA SIO KITU KIGENI KUSIKIA POLISI WANATOA TANGAZO KWAMBA MTU FULANI ANATAFUTWA.
HIKI NI KISINGIZIO KINACHOTUMIWA NA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KUEPUKA LAWAMA KUTOKA KWA WANANCHI. KITU KINGINE NILITAKA KUONGEZEA NI KWAMBA ZITTO ALIKUWA SPECIFIC KWA KUTAJA MAJINA YA WATU WALIOTOWEKA KAMA BEN SAANANE HALAFU MWIGULU NCHEMBA AKAKIMBIA SWALI KWA KULIJIBU KIUJUMLA BILA HATA KUTAJA MOJA YA MAJINA YA WATU WALIOTAJWA. KWA MFANO, ANGEWEZA KUSEMA KWAMBA BEN SAANANE ANATAFUTWA KWA TUHUMA KADHA WA KADHA, HUKU SIO KUTOA SIRI ZA SERIKALI.
KAMA NINGEKUWA NI ZITTO KABWE NINGEMUULIZA WAZIRI SWALI LA NYONGEZA, JE BEN SAANANE ALIKUWA ANATUHUMIWA KWA KOSA LOLOTE? KAMA NILIVYOTAJA HAPO JUU NI KAWAIDA KWA POLISI DUNIANI KOTE KUTOA MATANGAZO YA WATU WANAOTAFUTWA KWA TUHUMA MBALI MBALI. WATU WANATAKA KUJUA KAMA HAO WATU MAARUFU WALIOTOWEKA WALIKUWA NA TUHUMA ZOZOTE.
 
Hao yamkini ni wale unao waona je unajua kwenye operation zao ni wangapi wanauwawa?
Unajua mpaka wampate huyo gaidi ni wangapi wanakuwa wameshapitiwa.na mkono wa moto?
Kwenye posts zingine nimeeleza bayana kwamba wanaua only when necessary!

Ikiwa shaka ya Zitto (na yangu pia) kuhusu MKIRU ipo sawa basi askari wetu huko MKIRU sio kwamba "waliua" when only it's necessary lakini hiyo ilikuwa ndo hukumu kwa wote waliotuhumiwa!

But all in all, endeleeni kutetea uovu kwa sababu nyie sio yaliyowakuta na kv nafsi zenu zimekosa utu but this's not right!

Mahakama zetu zimejaa kesi kibao zenye miezi na miaka kwa sababu tu upelelezi haujakamilika! Kinyume chake, polisi wale wale ambao wana kesi kadhaa mahakamani ambazo hawajakamilisha upelelezi; huko MKIRU iliwachukua only few weeks kupeleleza na kuwabaini magaidi!!

Only fools can believe that! Unless hao watuhumiwa wawe detained pahala for interrogation, or else, kilichofanyika ikiwa ni vile inavyohisiwa basi kinaweza kufanywa na tawala za kidhalimu peke yake!

Guys... I repeat!! Endeleeni kutetea na kushangilia udhalimu kama huu kwa sababu mnadhani hauwahusu!! Hata UKIMWI wakati unaingia watu walikuwa wanawakejeli wenye UKIMWI na kuwaita MALAYA tu hao but today sidhani kama kuna familia ambayo haijasindikiza "MALAYA" kaburini!
 
Ulishawahi kusikia kesi ya ujajusi inasikilizwa mahakamani hapa Tanzania, let alone Africa? Ina maana hakuna majasusi maadui wanaokamatwa hapa Tanzania? Kama wanakamatwa wanapelekwa wapi?
Why unahoji kuhusu majasusi wakati mada inahusu Washukiwa wa ugaidi?!

But all in all, ni majasusi wa aina gani unaowazungumzia wewe? With unofficial cover or with official cover?!

Kama ni with unofficial cover, labda nikukumbushe ni kiasi cha mwaka mmoja au miwili tu iliyopita kuna Watanzania walikamatwa Malawi kwa tuhuma za ujasusi!!

Kila mwenye kufuatilia alifahamu tukio lile hadi siku mahakama inawaachia huru!

Kwa case ya Majasusi with official cover; in most cases huwezi kuwafikisha mahakamani kwa sababu kwa sababu diplomatic immunity!! Utakachofanya ni kuwatimua tu nchini!

But REMEMBER, hapa tunazungumzia watuhumiwa wa ugaidi na sio Majasusi! Au unataka kuniambia hujawahi kusikia watuhumiwa wa ugaidi wakifikishwa mahakamani hapa Afrika?!
 
Kibiti hakukuwa na ugaidi ila matukio ya mauaji ya watu wasio na hatia kwa hisia za kisiasa na waathirika wakubwa wakiwa viongozi wa chama kinachotawala na watumishi wa hiyo serikali inayotawala.
 
Yaani wewe ni hovyo kabisa, unashabikia mauwaji na utekaji kwa kwa ufuasi wako kwa ccm kwa kujifanya eti ww ni security expert?

Wacheni kuteka na kuuwa watu wasio na hatia yoyote kwa mambo ya kijinga kabisa. You can't sale your toxic rubbish to the people with positve brain. Only ccms, and not all will buy such a negative explanation.
 
UTANGULIZI
=======
Baada ya tukio la September 11 mwaka 2001, aliyekiwa director wa CIA kwa wakati huo aliitwa mbele ya bunge la marekani na kuhojiwa na bunge.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kuwa kuna uhusiano gani wa kiutendaji wa kazi kati ya idara ya ujasusi ya jeshi (Military Intelligence) na CIA katika kuzuia matukio ya uhalifu na kigaidi kutokea ndani ya marekani. CIA director alitoa jibu moja tu kwa kusema "that information is classified" baaaas hakuendelea tena. Not every aspect of state security should be clarified to politicians

MAONI YANGU BINAFSI KUHUSIANA NA SUALA LA KUCHUKUA WATU MATEKA WITH REFERENCE TO CHINA.
=============
Si kila mwenye uraia wa China ni mtu salama kwa maslahi mema na ustawi wa nchi hiyo.

Nchi ya China ina maadui wa ndani pamoja na nje wanaopanga mipango ya kuidhoofisha kila saa na kila dakika. Hivyo ni kazi ya vyombo vya dola kuwatambua na kuwadhoofisha kama sio kuwamaliza kabisa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Huyo mtu adui anaweza kuwa hata ni ndugu yangu mimi au ndugu yako wewe wa karibu lakini mimi na wewe tusiwajue ila wataalam wa mambo ya usalama wa nchi husika wakawajua mpaka njama zao.

Hivyo suala la watu kuchukuliwa mateka na kuhojiwa kwa nchi kama China ni kitu kisichoepukia kwa nchi kutaka kujilinda na kusonga mbele.

Hizo nchi mnazoziona zimeendelea na mnahisi zina viwango vya juu sana vya haki za binadamu na demokrasia kama Marekani, German, Uingereza na hata Japan zipo katika kiwango hicho cha maendeleo si kwa bahati mbaya. Hapana. Idara zao za usalama ni wakali sana. Unafikiri hawafanyiwi hujuma hao jamaa? Unafikiri serikali zao hazina vikosi za kuchukua mateka (abduction squads)??? Wanavyo. Tena wapo very sophisticated, equipped with modern weaponry and techniques.

Nchi ya China ina maadui wanaofanya kazi muda wote kutaka kuihujumu politically, economically hata socially pia (kueneza mienendo itakayoweza kupelekea mmomonyoko wa maadili hata kuua uzalendo miongoni mwa watanzania kama nyimbo za kuua uzalendo kwa vijana zinawezekana ni brainwashing song kwa vijana ili kuhujumu akili zao kwa manufaa ya baadae) na maadui hao wanaweza kuwa ni watu wenye uraia wa China (walio ndani na nje) ama wasio wa China (walio ndani na nje ya nchi) wanaotaka kuwatumia raia wa China kudhoofisha nchi yao pasipo wao raia kujua ama kwa kujua na kuwapa rushwa na wapo ndani pia nje ya nchi ya China.

Kwa hiyo issue ya abduction squads ipo hata marekani na uingereza na ni muhimu sana kwa nchi kujilinda, sembuse China.

Police hawapaswi kuwa wapole. Tofautisheni vituo vya police na nyumba za ibada. Police kuwa wakali inasaidia hata mtu akitaka kutenda kosa lazima awaze mara mbili mbili itakuwaje kama akipelekwa police hivyo ana ahirisha kutenda uhalifu.

Sipo JF kufurahisha. Nipo hapa kufafanua ninayoyajua akilini mwangu.

I STAND TO BE CORRECTED.

KIJANA KUWA MZALENDO, PENDA TANZANIA.
Tatizo ni kutenganisha usalama wa nchi/ raia na usalama wa watawala au chama tawala. Ndiyo maana nchi ulizotaja (ukiondoa china) zina checks and balance. Vyombo vya usalama havina unlimited power kufanya hayo unayoyasema. Wanawajibika kwa aina fulani chini ya wawakilishi wa wananchi (bunge). Ni kweli kuna classified information hawazitoi kwa kila mtu (hata Rais) lakini wakifanya mabaya (au wakiwa na tuhuma) hulazimika kutoa maelezo kwa Kamati husika. Tena tuhuma kama ya kuteka raia wao haina kinga yoyote. Taratibu za raia (wanayepasa kumlinda) ziko wazi - mkamate mpeleke kwenye vyombo vya sheria.
 
TERROR CAN BE USED TO FIGHT TERRORIST THEMSELVES. Ugaidi ndio dawa ya kuwatia adabu magaidi. Wewe baki na mindset yako ya judicial procedures, acha wanausalama wafanye yao. Tulia ulindwe mkuu
Kwahiyo unasema nitulie nilindwe na Serikali ya Magaidi sio? Nilindwe na serikali inayoua raia wake kwa kisingizio cha ugaidi sio? Serikali ambayo mamia ya kesi imeshindwa kuchunguza for months if not years but within few weeks iliweza kuwafahamu Magaidi wa MKIRU na kuwaua?

Ni wapi wamepata uwezo wa ghafla kiasi hicho?!

Hivi nyie watu are you really reasonable au mnaongea tu kwavile yaliyowakuta sio nyinyi?

Mtaendelea ku-justify udhalimu wa serikali hadi lini?

Baada ya Ben Saanane alipotoweka; watetezi wa udhalimu walisema Ben Saanane "amejiteka mwenyewe!"

Siku Tundu Lissu alipomiminiwa risasi; mwanzoni watetezi wa udhalimu walisema sio kweli... ni kiki tu hizo! Ilipothibitika pasipo na shaka yoyote kwamba madhalimu yalitaka kumuua Tundu Lissu; watetezi wao wakabadilisha single na kudai Tundu Lissu ni msaliti!

Few months later; Mwandishi wa Mwananchi akatoweka and presumably murdered!!

Kama kawaida; watetezi wa udhalimu wakajitosa kutetea udhalimu unaotendeka!

Leo hii bila aibu mnatetea watu kupotezwa huku mkiwa hamuishiwi justifications!!

Hivi unaweza kuingia field and within few weeks ukafahamu ni nani na nani gaidi halisi na nani ameingizwa tu mkumboni?

Kama huo uwezo wanao; wanashindwa nini basi kuutumia katika kuwapata wahalifu wengine?!
 
Infantry soldier ,Una utashi kama wangu,you surpassed tactical points.
Anaelewa atakuwa ameelewa ,naomba uwe unanitagi pia kwenye hizi maada.
Mengine tubishane tu ila kwenye usalama wa Tz Yangu nipo rigid ,
Naipenda Nchi Yangu.
TUNACHOKITAFUTA SASA NI UHURU WA MANYANI!
yaani mtu anadai taarifa nyeti kabisa zinaoweza ku compromise usalama wetu kama taifa zizsemwe kwenye magazeti au bungeni kwa kivuli cha demokrasia??huu ni upuuzi!
Kwanza hata tafsiri ya hili demokrasia ya kizungu nahisi ni tofauti na hii tunayohubiriwa!
mtuni hatari kwa usalama, ''unaiondoa hatari isiwepo'' its that simple!watu 53 milioni hawawez ishi kwa tabu eti sababu kuna kundi la watu 1000 ambao ''wakishughulikiwa'' italeta 'kisiasa'!
 
Sio kila upelelezi ni rahisi kufanyika mara moja. It might takes years. Inawezekana amekimbia nchi ama magaidi wamemteka. Ndio maana IGP anasema mtu yeyote mwenye taarifa zitakazoweza kuisaidia police apeleke
hahahaahha eti mwenye taarifa
 
Yaani wewe ni hovyo kabisa, unashabikia mauwaji na utekaji kwa kwa ufuasi wako kwa ccm kwa kujifanya eti ww ni security expert?

Wacheni kuteka na kuuwa watu wasio na hatia yoyote kwa mambo ya kijinga kabisa. You can't sale your toxic rubbish to the people with positve brain. Only ccms, and not all will buy such a negative explanation.
[emoji1] [emoji1] wasio na hatia.. ila waliokuwa wana uwawa na wasio na hatia walikuwa na hatia.!!
 
Serikali ya kidhalimu na iliyojaa uovu mara zote wao na mawakala wao lazima watafute sababu za kuhalalisha udhalimu na uovu wao!!!

Tundu Lissu ambae mlimmiminia risasi na kutaka kumuua ni gaidi?

Mwandishi wa Mwananchi ambae possibly nae amemiminiwa risasi ni gaidi?

Ben Saanane asiyefahamika aliko na bila shaka nae huenda amemiminiwa risasi ni gaidi?!

Ushetani na damu ya mwanadamu ni chanda na pete kwa sababu makafara ndio ada ya madhalimu ya Kiafrika!! Ni kutokana na ukweli huo ndio maana mnapokosa damu sahihi hamuoni taabu hata kutafuta damu popote pale zilipo kama mlivyopata kufuta damu hadi kwa wasafiri wa daladala na kutandika risasi za kukata kona!!!

Kila mwenye akili timamu anafahamu magaidi ni washenzi na pia wana mioyo ya kishetani iliyojaa uovu utamanio damu za wanadamu!! Ni kutokana na hilo ndio maana hawaoni taabu kuua watu bila kujali wahusika wana hatia au hapana! Wanachotaka wao ni DAMU, basi!

Hivyo ndivyo ambavyo nafsi za kishetani na mawakala wao wangpenda kuona!!!

Kinyume chake, ni serikali ya kidhalimu na iliyojaa roho za kishetani peke yake ndizo zinaweza kufanya mambo yake kwa mtindo ule ule unaofanywa na magaidi wapenda damu bila kujali ikiwa wahusika wana hatia au hapana!!!!

Ni matunda ya kutopewa na udhalimu na roho za kishetani ndio maana pale mawakala wenu wa kutoa roho wanapokosa mtu sahihi wa kumtoa roho, hawaoni taabu kuua hata wao kwa wao kama ambavyo Wakala mmoja wa mauaji alipomchomolea bastola Nape Nnauye na kutaka kumtoa roho wakati ni "mtoto wao!"
Huyo mtu adui anaweza kuwa
hata ni ndugu yangu mimi au
ndugu yako wewe wa karibu
lakini mimi na wewe tusiwajue
ila wataalam wa mambo ya
usalama wa nchi husika
wakawajua mpaka njama zao
 
Huyo mtu adui anaweza kuwa
hata ni ndugu yangu mimi au
ndugu yako wewe wa karibu
lakini mimi na wewe tusiwajue
ila wataalam wa mambo ya
usalama wa nchi husika
wakawajua mpaka njama zao
Wahalifu wengine wote wanashindwa kuwabaini lakini from nowhere, huko MKIRU wakaweza kuwabaini within few weeks if not days!!

Hata Zombe na wenzake walivyopeleka watu Magwepande na kuwamiminia risasi to death na wenyewe si walituambia hivyo hivyo... majambazi!
 
kwamfano wanasiasa waliopigwa risasi/kupotezwa walikua na madhara gani kwa taifampaka watekwe au kushambuliwa?
mtu kusema tutashitakiwa kufuatia uvunjifu wa mikataba hovyo na mwingine kusema ana 'phd feki' ni makosa yanayo hatarisha amani ya taifa?
Hukuambiwa huyo aliyepigwa risasi alikua anaangaika usiku kucha kutafuta nyaraka muhim za serikali ili aendelee kuropoka na kufurahisha mabwana zake?Kuna taarifa ni confidential na public na zote ziko kwa maslai ya umma.Yeye confidential news alikua anazitoa public tena kwa dharau na kejeli kwa maslai ya nani?Huyo mpuuzi ingekua ni China au Urusi angekua kashanyongwa au kutiwa sumu.
 
Mawazo ya hovyo kabisa haya!

Yaani watu kama akina Ben Saanane hawajulikani walipo kwa takribani miezi 18 sasa; wewe unataka kuaminisha watu kwamba mambo kama hayo yanatokea kwa ajili ya usalama wa taifa?!

Mwandishi wa Mwananchi nae unaenda mwezi wa 4 sasa with unknown whereabouts; halafu unataka kuaminisha watu kwamba, hayo hayapaswi kuhojiwa kwa ajili ya usalama wa taifa!!

Kwa mfano, unaweza kueleza ni aina ipi ya security threat iliyosabishwa na mtu kama Ben Saanane kwa kuhoji PhD ya Mkuu wa nchi?!

Ikiwa Waandishi wa Habari wanaruhusiwa kwenda hadi uwanja wa vita kuripoti vita; ni hatari ipi ya kiusalama ambayo ingesababishwa na Ripota wa Mwananchi kwa kutaka kufuatilia kilichokuwa kinaendelea Kibiti?!

By the way, kila mmoja anafahamu Magaidi wakubwa kabisa waliokuwa wanahatarisha usalama wa Marekani walikuwa wanakamatwa na kupelekwa Guantanamo!

Unaweza kutueleza hapa hao wahatarishaji wakubwa wa usalama wa Tanzania wamezuiwa gereza lipi kwa miezi yote hii?!

Btw, hivi unafahamu tofauti kati ya kulinda taarifa za siri za kiusalama (classified info) na kuficha maovu yaliyofanywa na watu walio kwenye system?

All in all, yote yana mwisho haya na endeleeni kutetea udhalimu kwavile hayajawakuta!

Na uzuri ni kwamba, majority ya watetezi wa udhalimu unaoendelea wala hampo kwenye inner circle, na kwa maana nyingine; hata nyie hampo salama!!

Ikiwa hata Nape ameshawahi kutolewa bastola hadharani; seuze nyie ambao wengine hata kula yenu ni shida!!

Wengine mkikesha kuangalia filamu na tathimlia za kivita na kijasusi kutoka Hollywood, mnadhani tayari ndo mmeshakuwa wataalamu na wachambuzi wa masuala ya kijeshi na kijasusi!
Ukiacha reference za jf,unauthibitisho upi kuwa kuhoji PhD ndiko kulikomfanya Ben apotee?
 
Hukuambiwa huyo aliyepigwa risasi alikua anaangaika usiku kucha kutafuta nyaraka muhim za serikali ili aendelee kuropoka na kufurahisha mabwana zake?Kuna taarifa ni confidential na public na zote ziko kwa maslai ya umma.Yeye confidential news alikua anazitoa public tena kwa dharau na kejeli kwa maslai ya nani?Huyo mpuuzi ingekua ni China au Urusi angekua kashanyongwa au kutiwa sumu.
mkaamua kumtandika risasi duh
 
UTANGULIZI
=======
Baada ya tukio la September 11 mwaka 2001, aliyekiwa director wa CIA kwa wakati huo aliitwa mbele ya bunge la marekani na kuhojiwa na bunge.

Moja kati ya maswali aliyoulizwa ni kuwa kuna uhusiano gani wa kiutendaji wa kazi kati ya idara ya ujasusi ya jeshi (Military Intelligence) na CIA katika kuzuia matukio ya uhalifu na kigaidi kutokea ndani ya marekani. CIA director alitoa jibu moja tu kwa kusema "that information is classified" baaaas hakuendelea tena. Not every aspect of state security should be clarified to politicians

MAONI YANGU BINAFSI KUHUSIANA NA SUALA LA KUCHUKUA WATU MATEKA WITH REFERENCE TO CHINA.
=============
Si kila mwenye uraia wa China ni mtu salama kwa maslahi mema na ustawi wa nchi hiyo.

Nchi ya China ina maadui wa ndani pamoja na nje wanaopanga mipango ya kuidhoofisha kila saa na kila dakika. Hivyo ni kazi ya vyombo vya dola kuwatambua na kuwadhoofisha kama sio kuwamaliza kabisa kabla hawajaleta madhara makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Huyo mtu adui anaweza kuwa hata ni ndugu yangu mimi au ndugu yako wewe wa karibu lakini mimi na wewe tusiwajue ila wataalam wa mambo ya usalama wa nchi husika wakawajua mpaka njama zao.

Hivyo suala la watu kuchukuliwa mateka na kuhojiwa kwa nchi kama China ni kitu kisichoepukia kwa nchi kutaka kujilinda na kusonga mbele.

Hizo nchi mnazoziona zimeendelea na mnahisi zina viwango vya juu sana vya haki za binadamu na demokrasia kama Marekani, German, Uingereza na hata Japan zipo katika kiwango hicho cha maendeleo si kwa bahati mbaya. Hapana. Idara zao za usalama ni wakali sana. Unafikiri hawafanyiwi hujuma hao jamaa? Unafikiri serikali zao hazina vikosi za kuchukua mateka (abduction squads)??? Wanavyo. Tena wapo very sophisticated, equipped with modern weaponry and techniques.

Nchi ya China ina maadui wanaofanya kazi muda wote kutaka kuihujumu politically, economically hata socially pia (kueneza mienendo itakayoweza kupelekea mmomonyoko wa maadili hata kuua uzalendo miongoni mwa watanzania kama nyimbo za kuua uzalendo kwa vijana zinawezekana ni brainwashing song kwa vijana ili kuhujumu akili zao kwa manufaa ya baadae) na maadui hao wanaweza kuwa ni watu wenye uraia wa China (walio ndani na nje) ama wasio wa China (walio ndani na nje ya nchi) wanaotaka kuwatumia raia wa China kudhoofisha nchi yao pasipo wao raia kujua ama kwa kujua na kuwapa rushwa na wapo ndani pia nje ya nchi ya China.

Kwa hiyo issue ya abduction squads ipo hata marekani na uingereza na ni muhimu sana kwa nchi kujilinda, sembuse China.

Police hawapaswi kuwa wapole. Tofautisheni vituo vya police na nyumba za ibada. Police kuwa wakali inasaidia hata mtu akitaka kutenda kosa lazima awaze mara mbili mbili itakuwaje kama akipelekwa police hivyo ana ahirisha kutenda uhalifu.

Sipo JF kufurahisha. Nipo hapa kufafanua ninayoyajua akilini mwangu.

I STAND TO BE CORRECTED.

KIJANA KUWA MZALENDO, PENDA TANZANIA.
Asante, kumbe JF bado ina watu makini! Maana sasa hivi imevamiwa na waimba taarabu na mateka wa wanasiasa uchwara
 
Back
Top Bottom