Mawazo ya hovyo kabisa haya!
Yaani watu kama akina Ben Saanane hawajulikani walipo kwa takribani miezi 18 sasa; wewe unataka kuaminisha watu kwamba mambo kama hayo yanatokea kwa ajili ya usalama wa taifa?!
Mwandishi wa Mwananchi nae unaenda mwezi wa 4 sasa with unknown whereabouts; halafu unataka kuaminisha watu kwamba, hayo hayapaswi kuhojiwa kwa ajili ya usalama wa taifa!!
Kwa mfano, unaweza kueleza ni aina ipi ya security threat iliyosabishwa na mtu kama Ben Saanane kwa kuhoji PhD ya Mkuu wa nchi?!
Ikiwa Waandishi wa Habari wanaruhusiwa kwenda hadi uwanja wa vita kuripoti vita; ni hatari ipi ya kiusalama ambayo ingesababishwa na Ripota wa Mwananchi kwa kutaka kufuatilia kilichokuwa kinaendelea Kibiti?!
By the way, kila mmoja anafahamu Magaidi wakubwa kabisa waliokuwa wanahatarisha usalama wa Marekani walikuwa wanakamatwa na kupelekwa Guantanamo!
Unaweza kutueleza hapa hao wahatarishaji wakubwa wa usalama wa Tanzania wamezuiwa gereza lipi kwa miezi yote hii?!
Btw, hivi unafahamu tofauti kati ya kulinda taarifa za siri za kiusalama (classified info) na kuficha maovu yaliyofanywa na watu walio kwenye system?
All in all, yote yana mwisho haya na endeleeni kutetea udhalimu kwavile hayajawakuta!
Na uzuri ni kwamba, majority ya watetezi wa udhalimu unaoendelea wala hampo kwenye inner circle, na kwa maana nyingine; hata nyie hampo salama!!
Ikiwa hata Nape ameshawahi kutolewa bastola hadharani; seuze nyie ambao wengine hata kula yenu ni shida!!
Wengine mkikesha kuangalia filamu na tathimlia za kivita na kijasusi kutoka Hollywood, mnadhani tayari ndo mmeshakuwa wataalamu na wachambuzi wa masuala ya kijeshi na kijasusi!