Wabunge walifanyiwa Presentation wakasema safi. Rais Samia sasa kaingia line

Wabunge walifanyiwa Presentation wakasema safi. Rais Samia sasa kaingia line

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Kwanza niulize; Wapi wabunge walikokwenda wasiombe rushwa? Hata kwenye taasisi za serikali ni hivyo hivyo! Mbumbumbu hawa ndo iwe kigezo cha kuwekeza Bagamoyo? NO!

Bandari ya Bagamoyo ilibuniwa kuanzia ikulu ya Kikwete. Hakukuwa na faida yoyote ya nchi ila familia yake na baadhi ya wanasiasa, ambao walishajipangia shares kwenye makampuni. Ndio maana tulisikia spika akizungumzia shares hadi kwenye shirika la reli. Ikumbukwe pia hakuna nchi Afrika hii ambako wachina wamewekeza bila kuiliza. Kwa kuwa tumeonesha urafi mkubwa kwa kusukumwa na hao walioipania siku nyingi, tutalizwa tu!

Huu ni muendelezo wa wizi na udhaifu wa marais wetu tangu enzi za mwinyi na mkataba tata wa Loliondo ambao hataki kuusema ktk kitabu chake. Mkapa kaja na Netgroup solution ikatwaa Tanesco, SA ikatwaa ATC, enzi za Kikwete ikawa ndo kabisa! IPTL, TRL na wahindi, chenji ya rada, escrow, etc. Leo hii huyu atakwepaje kupigwa? Hizi elimu zetu za hapa na pale uelewa unakuwa ni mdogo sana kujua kinachoendelea duniani.

Wenye uelewa ndo wanapotosha kabisa! Mtu kama Zitto mchumi uchwara wa Bungeni anajidai eti Oman na China tuna udugu, Foolish! Kwani nchi hii imetawaliwa na mataifa mangapi miaka ya nyuma, mbona hakuna walichotusaidia, itakuwa Oman waliotuuza kama watumwa!
 
Hapo wanapanga maslahi yao na firstguy anajificha ila ni mipango ya interest zao wapwani kwa hasara ya taifa.
 
Kipindi Magu anaijenga chato mlimpigia makofi na kushangilia juu.

Now mambo yanageuka mnalialia.

Acheni utoto na upuuzi nyie MATAGA.
Unasema maneno yanayozungumzwa mtaani, lakini unaripuka kama anayetoka usingizini.
 
Mkuu mimi ni nani niweze kukupinga? umeongea jinsi uhalisia ulivyo......ngoja tusubiri hapa wademkaji wa mradi wa bagamoyo walete kejeli na matusi...
 
Kwa Uchunguzi wako nimependa hio literature review jinsi awamu za nyuma zilivyotupiga ila umesahau awamu ya Tano, au Awamu hio hatukupigwa (kwa kuepuka kwako hio awamu naona kama upo bias) ingawa nakubaliana na wewe hii mikataba tusiende kichwa kichwa tumeibiwa sana na tutaendelea kuibiwa kama kutakuwa hakuna transparency....
 
Huu ni muendelezo wa wizi na udhaifu wa marais wetu tangu enzi za mwinyi
Wewe nani atakusikiliza ?? Unapunguza siku zako za kuishi kwa kupoteza energy yako muhimu.

Nani atachukuwa utopolo huu?

Niko Bagamoyo eneo itakapo jengwa bandari nafanya site clearance.
 
Bandari ITAJENGWA mtake msitake..


PERIOD!

#KaziInaendelea
#NchiKwanza
 
Nisaidieni mnipe somo, faida na hasara za bandari ya Bagamoyo.
 
Hii inafanana na fedha za covid dunia nzima wanasiasa wanazipiga na kuzila hela za covid si kenya si marekani.
 
Mama chapa kazi kwa maendeleo ya nchi Nyumbu pekee walio na mawazo Kama ya Kayafa wanatapatap Kama kima
 
Nisaidieni mnipe somo, faida na hasara za bandari ya Bagamoyo.
Faida:
1. Ni mradi utakaosaidia wanasiasa kupata shares na utajili wa kudumu kwa familia zao
2. Angalau itarudisha urafiki na wachina na waarabu wa oman, ambao walituuza utumwa siku nyingi
3. Pembe za ndovu zitapita kwa urahisi kuelekea china
4. Rais Samia ataweza kuwa na vitega uchumi bara kama wenzake waliostaafu
+5. Ngazi ya kwenda Mbinguni itakuwa ndani ya bandari na kuongeza baraka za nchi kuendelea

Hasara:
1. Bandari ya Dar itafungwa
2. Bandari ya Tanga itafungwa
3. Nchi nzima itakuwa ktk madeni ya kudumu
 
Mkuu mimi ni nani niweze kukupinga? umeongea jinsi uhalisia ulivyo......ngoja tusubiri hapa wademkaji wa mradi wa bagamoyo walete kejeli na matusi...
Kweli JF ina wademkaji!! Nadhani ni tatizo la kuongezeka kwa wasio na ajira. Kuna watu wanaandika mambo ya mbinguni wakiamini yamekuja na Samia.
 
Mkuu hamia Somalia nchi hii haikufai tena.
Mimi nilishapanga kuhama lakini dunia hii mwafrika ana heshima afrika tu! Ukienda US ujiandae kukabwa shingo hadi kufa!

Kwa hili la Bagamoyo, tunaliunga mkono. Tatizo tuelezwe uhusiano wa mradi na nchi ni upi?
 
Back
Top Bottom