Kwanza niulize; Wapi wabunge walikokwenda wasiombe rushwa? Hata kwenye taasisi za serikali ni hivyo hivyo! Mbumbumbu hawa ndo iwe kigezo cha kuwekeza Bagamoyo? NO!
Bandari ya Bagamoyo ilibuniwa kuanzia ikulu ya Kikwete. Hakukuwa na faida yoyote ya nchi ila familia yake na baadhi ya wanasiasa, ambao walishajipangia shares kwenye makampuni. Ndio maana tulisikia spika akizungumzia shares hadi kwenye shirika la reli. Ikumbukwe pia hakuna nchi Afrika hii ambako wachina wamewekeza bila kuiliza. Kwa kuwa tumeonesha urafi mkubwa kwa kusukumwa na hao walioipania siku nyingi, tutalizwa tu!
Huu ni muendelezo wa wizi na udhaifu wa marais wetu tangu enzi za mwinyi na mkataba tata wa Loliondo ambao hataki kuusema ktk kitabu chake. Mkapa kaja na Netgroup solution ikatwaa Tanesco, SA ikatwaa ATC, enzi za Kikwete ikawa ndo kabisa! IPTL, TRL na wahindi, chenji ya rada, escrow, etc. Leo hii huyu atakwepaje kupigwa? Hizi elimu zetu za hapa na pale uelewa unakuwa ni mdogo sana kujua kinachoendelea duniani.
Wenye uelewa ndo wanapotosha kabisa! Mtu kama Zitto mchumi uchwara wa Bungeni anajidai eti Oman na China tuna udugu, Foolish! Kwani nchi hii imetawaliwa na mataifa mangapi miaka ya nyuma, mbona hakuna walichotusaidia, itakuwa Oman waliotuuza kama watumwa!