Wabunge waliochaguliwa na wananchi wana uwezo mkubwa wa kuleta chachu ya maendeleo

Wabunge waliochaguliwa na wananchi wana uwezo mkubwa wa kuleta chachu ya maendeleo

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Januari imefika taarifa iliyoko ni kuwa watoto wetu wengi wanaoanza kidato cha kwanza hawana madarasa ya kusomea. Hili ni swala la kila mzazi na mwananchi. Hatujui nani katika hawa watoto atakuja kuboresha sera za nchi sisi tukiwa ni wazee.

Watanzania walioko Ughaibuni wangetumika kusaidia tatizo hili. Kila mtu awasiliane na mbunge wa jimbo lake kuona jinsi watakavyochanga. Hata kama kila mtu akileta €20 mbona watu 20 wanamaliza madarasa mawili.

Tatizo hapa ni kuwa, hata wale waliofuatilia uchaguzi mitandaoni. Wale viongozi walioonyesha uwezo wa kuleta mabadiliko siyo walioko madarakani. Hata wale walipita kura za maoni pia si walio rudi. Wabunge tulionao ni wale waliopendwa na NEC CCM.

Tutaletaje umoja wa kitaifa hapa ili watoto wetu wasome na ndugu zetu wasio na 5,000 ya mchango wasiwekwe ndani.
 
Wabunge wakatwe mishahara hadi ifikie sawa na ile ya walimu. Makato yajenge madarasa. Ujenzi ukiisha warudishiwe mshahara wao waliozoea
 
Wabungwe wakatwe mishahara hadi ifikie sawa na ile ya walimu.. makato yajenge madarasa.. ujenzi ukiisha warudishiwe mshahara wao waliozoea
Wabunge wengine hata kuitisha mikutano ya hadhara wanashindwa kwani waliowakataa ni wengi lakini wamepata ubunge kwa maajabu.
 
Sawa, tumekusikia. Tupo tunaijenga Chato kwanza. Leo tunazindua VETA.
 
Wabungwe wakatwe mishahara hadi ifikie sawa na ile ya walimu. Makato yajenge madarasa. Ujenzi ukiisha warudishiwe mshahara wao waliozoea
Hivi kwa nn wabunge wengi hawachangii maendeleo ya wananchi waliowachagua?
 
Back
Top Bottom