Pre GE2025 Wabunge waliojiongezea mshahara hawajamchangia Rais Samia fomu. Walimu wanao lipwa pesa ya pipi wanamchangia fomu

Pre GE2025 Wabunge waliojiongezea mshahara hawajamchangia Rais Samia fomu. Walimu wanao lipwa pesa ya pipi wanamchangia fomu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama ni ujinga /upumbavu ni wa watanzania wote.

Ikiwa walimu ndio sababu ya CCM kuendelea kuwa madarakani, je msiokuwa walimu mmechukua hatua gani??


Ikiwa hata yakiitishwa maandamano Kila Mtu anajifungia kwake anabaki kuia kelele JF tu


Sasa na wewe si kenge tu na upumbavu wako, unakimbia mvua unaingia kwenye dimbwi
 
Bila shaka kuwatukana walimu ni kujitukana wenyewe


Maana kama umefundishwa na wajinga/wapumbavu basi wewe ndio utakuwa mjinga na mpunbavu zaidi na ndio maana mnalalamikia matokeo ya tatizo huku mnaacha vyanzo vya tatizo

Raisi kamchagua mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi, unadhani mkurugenzi anaweza kumtosa boss au chama chake?

Mara ngapi watu wanakamata kura feki siku za uchaguzi? Huwa wanakamatwa nazo walimu?


Shida kubwa ni Katiba, Katiba ikiwa nzuri hata watumishi wa umma wanaweza kuzuiliwa kusimamia uchaguzi
 
Aina nne za mifumo ya kuendesha nchi
===
Serikali ya kibepari Umma wa kijamaa

Serikali ya kibepari Umma wa kibepari

Serikali ya kijamaa Umma wa kijamaa

Serikali ya kijamaa Umma wa kibepari
===
Najaribu kujiuliza hawa walimu wanataka kuuaminisha Ulimwenguni kuwa nchi yetu inaendeshwa kwa mfumo upi?
 
Walimu wanafanya hivyo katika misingi ya kuamini ndio njia pekee ya wao kupata masilahi zaidi, Kugoma hawawezi kabisa na haiwezi tokea kamwe. Wanachangishana fomu wakiamini hivyo kitu ambacho hakipo na wala hakitatokea sana sana wangoje pesa zao za kustafu watakazo lipwa.
Nchi hii kila sekta imejaza mitakataka tu! Ma mwalimu nayo hayajitambui!
 
Haa Haa Walimu Tena Wameshikwa Pabaya Kuhusu Fomu Ya Rais
 
Achana na propaganda za kitoto!

Hakuna mwalim aliefanya hivyo!!

Walikusanya walimu wao wa mchongo Ili kuwakilisha walimu halisi Kwa mtaji wa kisiasa!!

Nadhani ieleweke hivyo!!
Kulaumu Mwalimu wa Mkarama primary school Kwa ujinga wa viongozi wa Chama cha walimu ni kuwaonea. Hapa nilipo kuna walimu zaidi ya 300 lakini Hakuna hata mmoja aliyetoa hata 100. Hao ni viongozi wa CWT waliopachikwa na CCM baada ya kuwaondoa kina Maganga kwenye nafasi na kuweka misukule wao wasiojitambua. Ndo maana kuna watu hata akipata ajali akatoka salama anamshukuru Mama Kizimkazi. Ameanza kutukuzwa zaidi ya Mungu na yeye anaona Sawa tu.
 
Mimi mwalimu niko huku namanyele kumbe nimemchangia Rais kuchukua fomu.... Nilikua sujui km nimemchangia hela rais! Km nimemchangia rais bila mm kujua basi haya ni maajabu ya dunia...
Hela za Chama chenu mnazokatwa Kila mwezi zimemegwa amepelekewa mama yenu.
 
Zile ni Drama. Hakuna mwalimu Tanzania aliyemchangia Samia Pesa ili achukie form ya Urais. Mi Mwalimu mbona sijamchangia?
 
Back
Top Bottom