kekule benzene
JF-Expert Member
- Sep 28, 2016
- 1,444
- 3,576
Nchi hii kila sekta imejaza mitakataka tu! Ma mwalimu nayo hayajitambui!Walimu wanafanya hivyo katika misingi ya kuamini ndio njia pekee ya wao kupata masilahi zaidi, Kugoma hawawezi kabisa na haiwezi tokea kamwe. Wanachangishana fomu wakiamini hivyo kitu ambacho hakipo na wala hakitatokea sana sana wangoje pesa zao za kustafu watakazo lipwa.
Kulaumu Mwalimu wa Mkarama primary school Kwa ujinga wa viongozi wa Chama cha walimu ni kuwaonea. Hapa nilipo kuna walimu zaidi ya 300 lakini Hakuna hata mmoja aliyetoa hata 100. Hao ni viongozi wa CWT waliopachikwa na CCM baada ya kuwaondoa kina Maganga kwenye nafasi na kuweka misukule wao wasiojitambua. Ndo maana kuna watu hata akipata ajali akatoka salama anamshukuru Mama Kizimkazi. Ameanza kutukuzwa zaidi ya Mungu na yeye anaona Sawa tu.Achana na propaganda za kitoto!
Hakuna mwalim aliefanya hivyo!!
Walikusanya walimu wao wa mchongo Ili kuwakilisha walimu halisi Kwa mtaji wa kisiasa!!
Nadhani ieleweke hivyo!!
Hela za Chama chenu mnazokatwa Kila mwezi zimemegwa amepelekewa mama yenu.Mimi mwalimu niko huku namanyele kumbe nimemchangia Rais kuchukua fomu.... Nilikua sujui km nimemchangia hela rais! Km nimemchangia rais bila mm kujua basi haya ni maajabu ya dunia...