Wabunge walipe kodi, wabunge kutolipa kodi ni rushwa inayotolewa na Serikali

Wabunge walipe kodi, wabunge kutolipa kodi ni rushwa inayotolewa na Serikali

Wabunge bila aibu wanasifia wananchi kulipishwa kodi lukuki huku wakijua kwamba wao kama kupe wanaishi na kuneemeka kwa kodi zetu na jasho letu wananchi.
Yaani haya yote bila mwendazake tusingefika huku. Bahati mbaya hata Mama naye ana mwelekeo huo huo
 
Mshahara wa wabunge ni hela ya kodi, sasa kwa nini walipe kodi? Ni sawa na kumpa hela mwanao na halafu unamwambia akugawie hela ulizompa. Kama unahitaji hela mpe kidogo, nyingine ubaki nazo.
Mbona watumishi wa umma wanakatwa kodi kwenye mishahara yao inayotokana na kodi.

Wewe mzenji naona umeanza kuchanganyikiwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Naunga mkono hoja wakatwe kodi sio mshahara tu iwe mpaka marupurupu kama wanavyofanya kwa sekta binafsi.

Pia na huduma walipie kama watumishi wa kaiwada ila kadi zao ndio ziwe na VIP mfano huduma za afya, walipie kutokana na mapato yao.

Pia pensheni yao itokane na mishahara yao na marupurupu yao kama watumishi wengine wa umma.
 
Kodi wanalipa ila ni kidogo sana kutoka kwenye mishahara yao..ila hela nyingi imejazwa kwenye posho na marupurupu ambayo kwa mujibu wa sheria hayakatwi kodi.

#MaendeleoHayanaChama
Sasa si kwa mujibu wa sheria. Mi nilidhani wanafanya fraud
 
Mbona watumishi wa umma wanakatwa kodi kwenye mishahara yao inayotokana na kodi.

Wewe mzenji naona umeanza kuchanganyikiwa.

#MaendeleoHayanaChama

Ni ujinga pia. Mshahara unaolipwa na kodi kukatwa kodi. Afadhali hapa mngekata huo mshahara ili kodi mbaki nazo.
 
Wabunge walipe kodi. Katika nchi nyingi ulipaji wa kodi ni majawapo katika sifa kuu kwa wagombeaji wa ubunge kuwa nayo ili wakidhi kuchaguliwa.

Ni wazi kuwa kwa Wabunge wetu hawa kwa kutolipa kutolipa kodi wanakosa uhalali wa kuikosoa serikali pamoja na jukumu la kuhimiza ulipaji wa kodi.

Sasa hivi tunawaona wabunge wanavyoisifia Serikali kwa kuwatoza kodi kibao wananchi wanaowawakilisha kama chanzo kikuu cha mapato.

Swali linalonisumbua kama mwananchi ni sababu zipi zilipelekea hawa wawakilishi wetu wenye kipato na marupurupu maradufu kutolipa kodi.

Kila mbunge anayesimama bungeni cha kwanza kinachotoka kinywani kwake ni shukhrani kwa serikali na sifa pekee kwa kingozi Mkuu wa serikali.

Je bunge letu ni rubber stamp ya serikali na Rais wa nchi? Je kutolipa kodi ni mojawapo katika utekelezaji wa state sponsored corruption?

Hata wakitumia lugha gani katika utetezi ukweli utabaki pale pale; kwa kutolipa kodi wabunge wetu wanakula rushwa inayotolewa na serikali.
Naunga hoja.

bu msikilize Mzee Fumbua macho kwenye hii video Bishop Aungustine Mpemba.
 
Naona mnaona kodi tu kumbe maeneo mengi kodi inapotea.

Mimi ninachojua kuwa wabunge hawapo hata kwenye mifuko ya hifadhi ya Jamii

Hii ni changamoto kubwa ndio maana hawawezi kukiongelea Kikokotoo

Hawa ilitakiwa wakishaingia kwenye ajira wawe kama waajiriwa hata mishahara yao jipange na Bodi ya mishahara

Hizi Pension zao hazina formula wala HAKUNA mtu au mkampuni inayoweza kulipa hizo pension zao wanazolipwa

Haya mambo Mwigulu alitakiwa aiweke kama vyanzo vipya kabisa vya mapato nchini sio mitozo tu kuongezeka kila uchao wakati wengine ni free-laider ety kwasababu ni wanasiasa
Kwenye kikokotoo tumepigwa na kitu kizito wananchi wenzangu.

Kweli Ajuza wa miaka 60, umpe 33% ya M 100? sawa na M 33 kwa M 100, atafanyia kitu gani hiyo pesa kwa jinsi thamani ya pesa ilivyoshuka hivi tokana na mfumuko wa bei za bidhaa kuwa juu?

Kwa umri huo life span ya huyo Mstaafu ni bahati nasibu kutokana na akili kutumika sana na uwezekano wa kupata magonjwa kama kansa, BP ni kawaida sana sababu seli za kinga za afya ya mwili hupungua uwezo.

Kwanini huyo Mstaafu asife mapema kwa mazingira hayo?
 
Mshahara wa wabunge ni hela ya kodi, sasa kwa nini walipe kodi? Ni sawa na kumpa hela mwanao na halafu unamwambia akugawie hela ulizompa. Kama unahitaji hela mpe kidogo, nyingine ubaki nazo.
We mpumbavu mtumishi gani wa serikali asiyelipwa hela ya kodi?

Au unadhani serikali inapata wapi hayo malipo ya mishahara bila ya kukata kodi kila mwananchi?

Ficha upumbavu wako kwanza [emoji34]
 
Kila mbunge anayesimama kuchangia bajeti anaanza kwa kumshukuru na kumpongeza rais[emoji53][emoji28][emoji316]
 
Wabunge walipe kodi. Katika nchi nyingi ulipaji wa kodi ni majawapo katika sifa kuu kwa wagombeaji wa ubunge kuwa nayo ili wakidhi kuchaguliwa.

Ni wazi kuwa kwa Wabunge wetu hawa kwa kutolipa kutolipa kodi wanakosa uhalali wa kuikosoa serikali pamoja na jukumu la kuhimiza ulipaji wa kodi.

Sasa hivi tunawaona wabunge wanavyoisifia Serikali kwa kuwatoza kodi kibao wananchi wanaowawakilisha kama chanzo kikuu cha mapato.

Swali linalonisumbua kama mwananchi ni sababu zipi zilipelekea hawa wawakilishi wetu wenye kipato na marupurupu maradufu kutolipa kodi.

Kila mbunge anayesimama bungeni cha kwanza kinachotoka kinywani kwake ni shukhrani kwa serikali na sifa pekee kwa kingozi Mkuu wa serikali.

Je bunge letu ni rubber stamp ya serikali na Rais wa nchi? Je kutolipa kodi ni mojawapo katika utekelezaji wa state sponsored corruption?

Hata wakitumia lugha gani katika utetezi ukweli utabaki pale pale; kwa kutolipa kodi wabunge wetu wanakula rushwa inayotolewa na serikali.
Ndo KATIBA mpya inaandikwa hivyo, Marekani tunaowaita mabeberu mbona Rais analipa Kodi?

Uingereza wanalipa Kodi.

Pia wanalipwa kiduchu makusudi Ili Wazalendo pekee ndo waingie mjengoni.

Na Ukiwa na biashara unakabidhi, sio hapa Wamiliki wa vituo vya mafuta na waagizaji mafuta ndo wabunge na mawaziri.

Hiyo ni roho mbaya.
 
Kwa maana nyingine ni kwamba bungeni wamejaa wawakilishi wa serikali ya CCM na kwa hila serikali hiyo hiyo ndiyo ilihakikisha wanachaguliwa mwaka 2010.

Bungeni kwa sasa hatuna hoja mbadala wala kauli mbadala na kwa kauli zaoo wenyewe bungeni kwa sasa wanaitetea serikali kuliko hata wakati wa chama kimoja.

Bunge la sasa halina tofauti na kikao cha mkutano mkuu wa CCM na hili lilipangwa kwa makusudi liwe hivyo. Vikao vya bunge havina tofauti na timu ya kampeni.

Wabunge bila aibu wanasifia wananchi kulipishwa kodi lukuki huku wakijua kwamba wao kama kupe wanaishi na kuneemeka kwa kodi zetu na jasho letu wananchi.

Kila wanachomiliki hao wabunge kimetokana na kodi zetu na imefikia mpaka wanamsifia waziri wa fedha kwa kuwa mbunifu katika kutukamua hadi tunatoka damu.

Kweli Tanzania itaendelea kujengwa na wenye moyo huku ikitafunwa na wenye meno. Kwa ubinafsi wa Wabunge wetu unaotisha wanadiriki hadi kutunga sheria zisizowabana wao.
Yule marehemu wa Chato ndio alitaka bunge hili tulilo nalo, hii ndio legacy yake kwa wasiojuwa maana ya legacy.

Mbunge wa Ukonga Jerry Slaa aliliongea hili bungeni yule punguwani wa Kongwa alimshughurikia kwelikweli na kumfikisha kwenye kamati ya maadili.

Watanzania hatuko serious, Jerry Slaa alipolifikisha jambo hili bungeni hakupata sapoti ya umma.

Kwahiyo tukae kitako kwa kutulia tumezidi ukondoo.
 
Hii akili sijui wanaitoa wapi,ni ukosa akili kujifanya unaongea kwa uchungu kuhusu bajeti wakati wewe hulipi kodi
 
Kodi wanalipa ila ni kidogo sana kutoka kwenye mishahara yao..ila hela nyingi imejazwa kwenye posho na marupurupu ambayo kwa mujibu wa sheria hayakatwi kodi.

#MaendeleoHayanaChama
Hayo marupurupu na posho zilipangwa na nani kama siyo wao wenyewe?Ndiyo mambo ya kula kwa urefu Wa kamba?
 
Hili ni la msingi sana. Lkn likiibuliwa linapotezewa kiaina.
 
Back
Top Bottom