Mshahara unaodaiwa wanapata wengi wa Wabunge hawa wala rushwa ni chini ya Tsh. 3,000,000/= kwa mwezi lakini jumla hela wanazosukumiziwa mifukoni kila mwezi ikikaribia Tsh. 20,000,000/= kwa mwezi kutokana na posho na malipo mengine mengi tu.
Tunapoambiwa wanalipa kodi ni makato kwenye mshahara wa hizo milioni tatu lakini katika malipo ya milioni ishirini wanazojaziwa mifukoni kila mwezi hawalipi hata senti tano. Cha ajabu Mama ntilie mwenye kipato kisichofika hata laki moja analipishwa kodi.
Wananchi wapigwa butwaa wakimshangaa Waziri wa fedha kwa mbwembwe kuwahimiza hadi vijana wa miaka 18 kulipa kodi na bunge zima kulipuka kwa shangwe, vigelegele, ugongaji wa meza na ukataji wa mauno juu ya meza wakimpongeza Waziri kwa ubunifu.
Tumelogwa...