Wabunge Wanapokosa hoja za kisiasa wanakimbilia vifungu vya misahafu. Ongezeni ufahamu wa siasa

Wabunge Wanapokosa hoja za kisiasa wanakimbilia vifungu vya misahafu. Ongezeni ufahamu wa siasa

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Umekuwa mtindo wa kudumu ukisikiliza Bunge unaishia kuambiwa Biblia inasema hivi, Kuruani inasema hivi. Hakuna maneno ya watu mashuhuri au hoja zenye mashiko kisiasa. Hii ni dalili ya kuwa na wanasiasa waliofilisika kisiasa na wanahangika sana na elimu ya dini.

Safari hii Spika kaangukia pua kwa kutoa maneno ambayo hayajawahi kuandikwa ktk Biblia. Amejaribu kunyanyuka kwa kuombewa msamaha na ofisi ya Bunge, bado ameangukia kisogo kwa kukosea maelezo ya Biblia, na hapo ni baada ya kujivunia ushiriki wake ktk kanisa. Tuelewe nini kichwani mwake? Tuna mfumo mbovu na tunapata wabunge wabovu na hatimaye spika mbovu.
 
Walikuwa na hasira na gwajima za waziwazi.ukiwafuatilia wote pale waliotaja vifungu vya biblia vyote vinaupande wake wa pili kama jibu lao.mfano aliyesema vita vyetu si vya nyama nivya rohoni.akaendelea kwamba,tunaweza kuchanja kama itakuwa ni sumu kwa vile cc niwa Mungu havitatudhulu.jibu lake ni kwamba Mungu hadhihakiwi.huwezi kujitupa gholofani ukisema Mungu ataniokoa.mwingine akasema tutii mamlaka ilipo.biblia inasema mamlaka iliyowekwa na Mungu na inayomtii Mungu ,sio hii mamlaka inayobambikizia watu kesi,matozo wakati maisha ya watanzania yapo chini.kiujumla walikuja na jazba na wakawa wamepotea kwenye mada husika.jpili tutawafundisha biblia inasemaje na ninani anafaa kuwa kuhani wa Mungu
 
..nakuunga mkono kwa 100%.

..kuna tatizo kubwa sana la wanasiasa na viongozi kukosa hoja na kuamua kushawishi kupitia misahafu.

..hali hiyo inatokana na wanasiasa na viongozi wetu kutofanya utafiti, au kutojisomea, kabla ya kuwasilisha maoni yao.
 
Tukubali tu kwamba tuna viongozi wadhaifu kwa ufahamu. Sasa angalia Spika! Eti alijivunia kuwa ni mshiriki mzuri huko kwenye kanisa lake, halafu anakosea kiasi kile na kusemekana ni ulimu kukosa mfupa. Alipoandika je? Tatizo akikaa pale anajiona anafahamu sana kuliko wa-TZ waliokaa nyumbani na maofisini.
 
Tuna genge la wahuni,chakubanga bungeni,hawana kitu kipya zaidi ya kubadirika kulingana na upepo ulivyo,hii yote ni sababu ya uchu wa madaraka na kutosimamia nafsi zao na kutojiamini kwa kuogopa kufukuzwa chamani,so wamejaa unafiki mtupu.
 
Back
Top Bottom