Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wabunge wanne kati ya 17 waliolazwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) wameruhusiwa baada ya afya zao kuimarika, huku wengine wakiendelea na matibabu.
Majeruhi hao walipata ajali juzi eneo la Mbande wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma wakienda Mombasa, Kenya kwenye mashindano ya 14 ya Mabunge ya Afrika Mashariki.
Akizungumza na Nipashe jana, Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura wa BMH, Dk. Winnie Msangi, alisema wabunge hao waliruhusiwa baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari bingwa hospitalini hapo na afya zao kuonekana kuimarika.
Dk. Msangi alisema majeruhi wengine waliosalia wanaendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa madaktari, ili kuhakikisha afya zao zinaimarika na kuendelea na shughuli zao za kila siku.
Pia, Soma: Dodoma: Basi lililobeba Wabunge wa Tanzania lagonga Lori na kuwajeruhi Wabunge 23