Tetesi: Wabunge wanne, kuhama vyama vyao

Tetesi: Wabunge wanne, kuhama vyama vyao

Nelson Masaduki

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Posts
346
Reaction score
380
Nyalandu ameweka sytle ya kuhama vyama.

Tetesi kutoka ndani ya chama fulani ni kwamba kuna wabunge wanne ambao watahama chama chao. Wengine walionekana jijini Dar es Salaam walipokuwa wakitoka katika kikao chao cha siri.

Pamoja na kwamba maamuzi ya mwisho yatatolewa hivi karibuni kuhusu namna ya kujitangaza kuhama chama chao, bado kuna shinikizo kuwa wajitangaze kwa wakati mmoja ila wapo wanaotamani kila mtu akajitangazie jimboni kwake.

Wakihama, watarejea tena kugombea kupitia chama watakachokwenda. Watu wanaamka, na wanafanya msimu wa kampeni kuanza. Kila wanapojiengua tume ya uchaguzi inabidi kutangaza utaratibu wa uchaguzi.

Tuendelee kusubiri.
Mungu ibariki Tanzania
 
Ni wa chama tawala au ni wa upinzani wanaotafuta kutumiwa na chama tawala?
 
Maadamu vikao vya siri vinafanyikia Dar basi hao ni wabunge wa chama kileeeee...!ila vikao vingefanyikia Arusha ningejua ni wa chama chenye nchi ndio wanao hama.
 
Tume ya utumishi wa umma na ile ya utawala bora watuambie kama alichokifanya Kitila Mkumbo ni sahihi kwa mtumishi wa umma kuvaa sare za chama na kujitangaza hadharani kujihusisha na siasa za chama hicho huku bado ni Katibu Mkuu wa wizara. Hii nchi tuliikuta ikiwa na kanuni na taratibu na miiko ya utumishi wa umma, tusiharibu.
 
wale wanaohama wakusanyane woote, tuwe na press moja, halafu tunapokezana tu, wa upande huu wanakwenda upende mwingine wanapokelewa, and viseversa, hizi mambo zinakula muda wa wavuja jasho jamani kuwajadili wanasiasa tuu.
 
Tume ya utumishi wa umma na ile ya utawala bora watuambie kama alichokifanya Kitila Mkumbo ni sahihi kwa mtumishi wa umma kuvaa sare za chama na kujitangaza hadharani kujihusisha na siasa za chama hicho huku bado ni Katibu Mkuu wa wizara. Hii nchi tuliikuta ikiwa na kanuni na taratibu na miiko ya utumishi wa umma, tusiharibu.
Mkuu, that will never happen may be over your dead body.
Dola inashikwa na waleee ambao ndo wanaunda tume unazozitaja.Nani hataki kibarua chake.
Kitila is a political hypocrite like many other politicians you know.
 
Back
Top Bottom