Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Dickson Ng'hily

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
451
Reaction score
485
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, pamoja na mambo mengine..Wataka Umri wa mgombea uraisi upunguzwe tka miaka 40 hadi 35...Wataka Mawaziri wateuliwe nje ya wabunge...Uteuzi wa viongozi wa juu uthibitizhwe na Bunge...Idadi ya Wizara ijulikane kikatiba na ziwe chache...

Wataka matokeo ya rais yapingwe mahakamani...Muungano wa kimkataba (treaty-based union)...Rais wa Zanzibar awe Makamu wa rais...Majina matatu ya jaji mkuu yapendekezwe kwa rais kwa uteuzi na jaji athibitishe na Bunge na Rais asiwe na mamlaka ya kuwaondoa mpaka ridhaa ya wabunge, Hapa inahusu pia uteuzi wa CDF,IGP, Mkuu wa TISS, Magereza, Uhamiaji nk....

Wataka pia ubunge na udiwani uwe na kikomo...Viti maalumu vifute na badala yake majibo yawe ni wilaya na kuwe na mgombea ubunge na mgombea mwenza wake..Kama mgombea ni mwanaumwe, mgombea mwenza awe mwanamke na akichaguliwa mmoja wote wameshinda kama kwa rais...Uraisi uwe wa Kipindi kimoja cha miaka 7.....

Pia uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship)...Kuwe na tume kikatiba itakayo shunghulikia kero za Muungano...Chiligati ataka Articles of Unioni zirejee kama ilivyokuwa mwanzo mambo 11...Mafuta gesi visiwe vya Muungano (hapa ni wabunge wa CCM na CUF bara na Visiwani waliungana)....Ubunge na Udiwani uwe na kikomo cha vipindi viwil (Miaka mitano kila kipindi)....Na mambo mengine mengi...
Source Mimi Mweneyewe Bungeni Dodoma leo...
 
Maoni ya kipumbavu na kijuha na kama wabunge wa Chadema mmeshiriki maoni haya ya kuweka kipindi cha rais kiwe kimoja1 kwa miaka 7 basi mjue na nyie mmekuwa mafaalla pia na kama mnataka rais wa Zanzibar awe makamu wa rais basi na huo ni ufalllla.
 
Uraisi miaka saba? Hata kama ni kipindi kimoja siungi mkono hoja hiyo hata kidogo.
Miaka mitano mitano kwa mihula miwili bado inafaa sana.
Viti maalum kuondolewa naunga mkono hoja hiyo lakini mgombea ubunge kuwa na mgombea mwenza siungi mkono. Wazo langu wilaya ziwe majimbo ya uchaguzi na kuwe na wagombea wanaume na wanawake. Ukiweka mgombea mwenza itasababisha wagombea wabovu kuchaguliwa kwa kubebwa na wale wazuri.
 
dah bunge hili hili la ccmoko au lingine? maana makinda,sita,lowasa n.k watafanya kaz gan tangu 1976 wapo bungen wawaachie vjana wapo weng mtaan na wao wajenge taifa lao kila cku majna hayo hayo.
 
Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.

1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengata sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.

2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!

3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?
 
Maoni ya kipumbavu na kijuha na kama wabunge wa Chadema mmeshiriki maoni haya ya kuweka kipindi cha rais kiwe kimoja1 kwa miaka 7 basi mjue na nyie mmekuwa mafaalla pia na kama mnataka rais wa Zanzibar awe makamu wa rais basi na huo ni ufalllla.
Sina tatizo na pendekeza la Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais, sioni sababu ya kuwa na gharama kubwa ya kuwa na makamu wa Rais na bado kuwe na Rais wa Zanzibar. Wakati Rais wa muungano anapokuwa hayupo basi Rais wa Zanzibar aongoze. Lakini pia itabidi katiba iseme kama itakuwaje pale atakapotokea kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano ni wa kutoka Zanzibar.

Lakini suala ambalo nalipinga kwa nguvu zote hapa ni hilo la Rais kuongoza nchi kwa miaka saba mfululizo. Hapo kwa kweli wamechemka, bora hata wangepunguza hata hiyo miaka mitano. Maana ikitokea mna Rais mbovu kusubiri miaka mitano ni migumu kweli. Bora iwe hata miaka minne kila mhula badala ya mitano.

Na la mwisho, kwenye umri, nadhani wanamtengenezea njia Zitto, its no wonder kwamba yeye ndo amependekeza hilo. Lakini taasisi ya urais ni taasis nyeti na inayohitaji mtu mwenye akili iliyokomaa, nafikiri badala ya kupunguza walipaswa kuongeza, angalau iende 45 na si kushusha. Tunataka Rais ambaye ataweza kujiheshimu na si Rais ambaye anaingia Ikulu huku anatafuta dogodogo. Tunataka Rais ambaye atakuwa na uwezo wa kupima kauli zake kabla ya kuzitamka hadharani.
 
Maoni ya kipumbavu na kijuha na kama wabunge wa Chadema mmeshiriki maoni haya ya kuweka kipindi cha rais kiwe kimoja1 kwa miaka 7 basi mjue na nyie mmekuwa mafaalla pia na kama mnataka rais wa Zanzibar awe makamu wa rais basi na huo ni ufalllla.
Duuu wamekuuzi kweli.......
 
Hili la urais kuwa miaka 35 linalenga zaidi kuisambaratisha CDM, kwani Mh.Zitto lazima atalianzisha tu hapo 2015.
 
Miaka 7 ya nini?Ikiwezekana iwe miaka 4 tu na kikomo iwe vipindi 2 tu.Hata hivyo, naona mawazo ya upinzani kuhusu katiba mpya yamezingatiwa.
 
-Nakubaliana na suala la kushusha umri wa Urais.Inawezekana kuna uwezekano wa kupata wenye uwezo wa kuwa Rais

-Nakubaliana na hoja ya kuwa na approval ya uteuzi wa CDF,Chief Justice,IGP,AG na CAG
-Pia tufikirie kuwa na bicameral parliamentary system.Kama ni uwakilishi tuachane na ukuu wa wilaya na mkoa kwa kufanya decentralization

-Hapo kwa serikali tatu tungekuwa na federal system ambayo inakidhi hoja yangu hapo juu ya decentralization

-Nashindwa kuelewa ni kwa nini wabunge hawajaongelea kuhusu impeachment ya Rais.

Pia ningependekeza vipindi vya urais viwe miaka 4 kwa two terms.Miaka 7 ni hqtari hasa kwa mazingira haya ya wimbi la ufisadi na kutowajibika.Pia impeachment process haijarahisishwa.Napinga vikali hili la miaka 7

-Pia hapo kwenye bicamneral parliament.Bunge la law chamber liwe miaka 3 kwa vipindi viwili na chaguzi zifanyike kwa kupishana na uchaguzi wa Rais uwe baada ya uchaguzi wa Bunge na magavana
 
mawazo mengine hayafai, naona wabunge wetu wamekosa kazi sasa, rais wa zanzibar awe makamu wa rais???? halafu rais miaka saba?? duh kwa hiyo kama akiboronga tumsubiri miaka saba???
 
Yaani WaTZ tuna maajabu mengi sana. Kila kukicha kunatokea kioja kingine!
Nchini kuna matatizo zaidi ya milioni. Wabunge wanaona Umri wa Rais ukipunguzwa kuwa miaka 35 ndiyo kitu muhimu zaidi, ama kweli sikio la kufa halisikii dawa!! Halafu muhula mmoja uwe miaka 7, miwili 14. Tukipata bahati mbaya ya kupata Rais bomu, basi tunaye kwa miaka 14!
 
Yote ni sawa lakini umri wa urais ni kijana mno bado ana mambo mengi,urais miaka saba sijaikubali hata kidogo,ikitokea mkapata rais bomu mtateseka kwa miaka saba? No hiyo haikubaliki kabisa.
 
Kusema kipindi cha urais kiwe ni miaka 7 ni ujuha uliopitiliza, najua hayo yatakuwa ni magamba tu.

Pili umri kupunguzwa naona siyo mbaya. Ukomo wa ubunge na udiwani sioni kama una tija.

Kuwa na mgonbea mwenza kwa ubunge nao ni ujuha uliopitiza.

Kufuta viti maalumu fifty fifty, ila maoni yangu viti hivi vipunguzwe kutoka idadi iliyopo saizi maana wengi ya viti maalumu wamekuwa kama visusio vya wakuu.

Kuhusu jaji mkuu naunga mkono hoja ila kuwe na vigezo kabisa ili kuepuka masuala mengi hasa udini unadaiwa kukubuhuvsiku hizi.

Uteuzi wa CDF na wenzake naunga mkono hoja.
 
Hatutaki mapendekezo yao walikuwa wapi siku zote, hizi ni njama za kutaka kuhodhi maoni ya katiba waache wananchi watoe maoni yao/yetu
 
Pasiwe na mgombea mwenza kiti cha urais. Kwani mwenza ni mke au mume wa rais. Acheni dharau
 
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, pamoja na mambo mengine..Wataka Umri wa mgombea uraisi upunguzwe tka miaka 40 hadi 35...Wataka Mawaziri wateuliwe nje ya wabunge...Uteuzi wa viongozi wa juu uthibitizhwe na Bunge...Idadi ya Wizara ijulikane kikatiba na ziwe chache...

Wataka matokeo ya rais yapingwe mahakamani...Muungano wa kimkataba (treaty-based union)...Rais wa Zanzibar awe Makamu wa rais...Majina matatu ya jaji mkuu yapendekezwe kwa rais kwa uteuzi na jaji athibitishe na Bunge na Rais asiwe na mamlaka ya kuwaondoa mpaka ridhaa ya wabunge, Hapa inahusu pia uteuzi wa CDF,IGP, Mkuu wa TISS, Magereza, Uhamiaji nk....

Wataka pia ubunge na udiwani uwe na kikomo...Viti maalumu vifute na badala yake majibo yawe ni wilaya na kuwe na mgombea ubunge na mgombea mwenza wake..Kama mgombea ni mwanaumwe, mgombea mwenza awe mwanamke na akichaguliwa mmoja wote wameshinda kama kwa rais...Uraisi uwe wa Kipindi kimoja cha miaka 7.....

Pia uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship)...Kuwe na tume kikatiba itakayo shunghulikia kero za Muungano...Chiligati ataka Articles of Unioni zirejee kama ilivyokuwa mwanzo mambo 11...Mafuta gesi visiwe vya Muungano (hapa ni wabunge wa CCM na CUF bara na Visiwani waliungana)....Ubunge na Udiwani uwe na kikomo cha vipindi viwil (Miaka mitano kila kipindi)....Na mambo mengine mengi...
Source Mimi Mweneyewe Bungeni Dodoma leo...

Asante kwa kutujuza, ila haya mambo kwa nini yanajadiliwa bungeni wakati tuko kwenye Mchakato Wa kuandika katiba mpya?

Ina maana CCM ikipitisha haya itakuwa imetudharau wananchi!
 
Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.

1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengata sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.

2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!

3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?

Nimependa point zako tatu zina mashiko maana 7 years ili iweje, hapo 35yrs - Raisi naungana na wewe maana institutions nyingi hazijakaa vyema kila siku wanakuja na vitu vipya sasa kama hajaonja mikikimikiki inakuwa ngumu kuimudu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kumbe wanamwandaaa zzk awe rais au uvurugaji wa siasa za maji taka
 
Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.

1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengata sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.

2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!

3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?

nakuunga mkono mkuu!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom