Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Eti mgombea mwenza....haya mambo ya kubalance gender ndo yaliyotuletea yule mama 'supika'.
 
Mawazo mengine bwana ya ajabu sana. Eti miaka saba urais!!! imagine huyu Aliy..ndo angekuwa anaongoza miaka saba! Najua wazo ili ni la copy and paste. Nchi kama hii ambayo chaguzi zake na mchunjo wa kupata viongozi bado ni utata, ukimweka kichaa ikulu itakuwaje? maana kwa mfumo huu tulionao nawaona vichaa wakielekea ikulu!
 
Kwakuwa tunakubaliana kwamba ujana unakomea kwenye umri wa miaka 35 basi nakubaliana na hoja ya kupunguza umri wa mgombea uraisi ili wale tuliovuka ujana tupate haki ya kugombea uraisi badala ya kutulazimisha kuwa wapiga kura tu katika kipindi cha mpito kuelekea miaka 40.
Ila sasa twende mbele some extra miles tuweke vigezo mahsusi kwa mgombea uraisi na mojawapo na ya lazima iwe ni uadilifu wake usiwe wa kutiliwa shaka hata kidogo.
 
Hili la urais kuwa miaka 35 linalenga zaidi kuisambaratisha CDM, kwani Mh.Zitto lazima atalianzisha tu hapo 2015.

Hii inadhihirisha ni jinsi gani bunge limechangia kuzamisha hii nchi. Wanawaza vyeo tu na sio ustawi wa jamii nzima ya Tanzania. Hilo la miaka 35 liko wazi mno ni kitu gani kinatafutwa hapo. Ni mkakati wa kusambaratisha upinzani. Lakini kama ambavyo tumeona mara nyingi wakubwa hawa wamekuwa wanafanya maamuzi bila kupima madhara yatokanayo na maamuzi yao. Hili la miaka 35 litaleta madhara makubwa way beyond CHADEMA. Itakula kila upande.
 
Kwakuwa tunakubaliana kwamba ujana unakomea kwenye umri wa miaka 35 basi nakubaliana na hoja ya kupunguza umri wa mgombea uraisi ili wale tuliovuka ujana tupate haki ya kugombea uraisi badala ya kutulazimisha kuwa wapiga kura tu katika kipindi cha mpito kuelekea miaka 40.
Ila sasa twende mbele some extra miles tuweke vigezo mahsusi kwa mgombea uraisi na mojawapo na ya lazima iwe ni uadilifu wake usiwe wa kutiliwa shaka hata kidogo.

Kamanda Tupo ukurasa mmoja.Nakumbuka hii mada ya umri ililetwa hapa mwaka jana na nilisema age group ya 35-40 imekua deprived off haki yao ya kikatiba.Imebaki haki ya kupiga kura tu.

Pia niliongelea umuhimu wa vigezo vya kibaiolojia na kisaikolojia vya kuweka limit ya urais.Kuanzia miaka 80 and above iwe no.Tuangalie diminishing criteria katika reasoning capacity and tough/prudent desicion making capability.

Tuweke uadilifu na sifa nyingine mbele kwa kulenga maadili ya uongozi
 
Lengo la kutaka mgombea ubunge kuwa na mgombea mwenza ni nini hasa? Je mgombea anaposhinda huyo mwenza nae atahudumiwa kwa kodi hii hii? Au itakuaje? Ila kufanya wilaya kuwa majimbo ya uchaguzi ni bora zaidi maana itapumguza idadi ya wabunge na hivyo kupunguza gharama.

Ukitakafari kwa kina, 'mbunge mwenza' technically ni viti maalum. Wanachofanya hawa walafi wa vyeo kupumbaza watu kuwa wanataka kufuta viti maalum lakini wanarudisha kwa 'jina' la mgombea mwenza. This is 'structural unemployment' Mbunge mwenza maana yake nini hasa?

Kama sikosei sasa tuna Wilaya 133 (naomba nisahihishwe), kwa maana hiyo tutakuwa na wabunge 266 (133 x 2=266). Hapa kila mtu atakuwa mbunge kamili kwa maana ya malipo/posho etc.

Tujiulize, kama tuna uwezo wa kuhudumia (posho etc) wabunge 266 kwa nini tusitenge majimbo 266 ili kila mmoja akagembee kwenye jimbo badala ya huu UKUPE? Kuna Wilaya nyingine ambazo ni kubwa sana - kioneo na hata kwa idadi ya watu. Mfano Kinondoni ni Wilaya, kuna watu wangapi Kinondoni? Kwanini tusiwe na formula ya kugawa majimbo ili kuhakikisha uwiano mzuri katika representation?
 
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, pamoja na mambo mengine..Wataka Umri wa mgombea uraisi upunguzwe tka miaka 40 hadi 35...Wataka Mawaziri wateuliwe nje ya wabunge...Uteuzi wa viongozi wa juu uthibitizhwe na Bunge...Idadi ya Wizara ijulikane kikatiba na ziwe chache...

Wataka matokeo ya rais yapingwe mahakamani...Muungano wa kimkataba (treaty-based union)...Rais wa Zanzibar awe Makamu wa rais...Majina matatu ya jaji mkuu yapendekezwe kwa rais kwa uteuzi na jaji athibitishe na Bunge na Rais asiwe na mamlaka ya kuwaondoa mpaka ridhaa ya wabunge, Hapa inahusu pia uteuzi wa CDF,IGP, Mkuu wa TISS, Magereza, Uhamiaji nk....

Wataka pia ubunge na udiwani uwe na kikomo...Viti maalumu vifute na badala yake majibo yawe ni wilaya na kuwe na mgombea ubunge na mgombea mwenza wake..Kama mgombea ni mwanaumwe, mgombea mwenza awe mwanamke na akichaguliwa mmoja wote wameshinda kama kwa rais...Uraisi uwe wa Kipindi kimoja cha miaka 7.....

Pia uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship)...Kuwe na tume kikatiba itakayo shunghulikia kero za Muungano...Chiligati ataka Articles of Unioni zirejee kama ilivyokuwa mwanzo mambo 11...Mafuta gesi visiwe vya Muungano (hapa ni wabunge wa CCM na CUF bara na Visiwani waliungana)....Ubunge na Udiwani uwe na kikomo cha vipindi viwil (Miaka mitano kila kipindi)....Na mambo mengine mengi...
Source Mimi Mweneyewe Bungeni Dodoma leo...

Mawazo mengine yote naweza kukubaliana nayo lakini hapo kwenye RED kuna siri kubwa imefichika.

Mosi, wanataka rais awe na kipindi kimoja tu cha miaka 7 na wakati huo huo wanahubiri uraia wa nchi mbili. Hapo ni kupalilia ufisadi wa rais na washirika wake (kama ilivyo sasa) ili sasa baada ya kufisadi na kukwapua mabilioni yetu wakimbie zao ughaibuni ambako watakuwa na uraia wa pili tayari.

Pili, ubunge na udiwani kuwa na kikomo ni vema kabisa lakini kituko ni hoja ya wabunge wenza na kutaka majimbo yafutwe tubaki na wilaya. Kwa utajiri gani tulionao wa kulipa miposho kwa wabunge wawiliwawili? Yaani tunarundika wabunge kibao wa nini? Watu sasa tunataka bunge dogo, la hoja na lenye mamlaka ya kuisimamia na kuihenyesha serikali. Kwa sasa pamoja na wingi wao hakuna wanachofanya.Ni porojo tupu.

Mfano kwa sasa tuna Wilaya zaidi ya 120, kwa hoja ya wabunge ya kutaka majimbo yafutwe tubaki na Wilaya zenye wabunge wawili kila moja maana yake tuwe na wabunge 240 na zaidi, wote wa nini? Bunge la sasa lina wabunge zaidi ya 300 lakini tunachoshuhudia ni Wabunge active wasiozidi hata 50,Kwa nini tusisisitize kubaki na mbunge mmoja na mwenza wake kutoka kila mkoa? Ili walau tuwe na wabunge 70-80
 
pamoja na kwamba yataongelewa mengi juu ya maoni haya, na kwa kuwa kila mmoja wetu hupenda kuskia kile anachotegemea kusikia, na ikiwa tofauti ndio mtafaruku kama huu huwa unatokea.

kwa mimi binafsi sioni kama kuna shida yoyote kwa raisi akiwa madarakani kwa miaka 7, maana ni michache zaidi kwa nchi yenye demokrasia changa kama tanzania kuliko miaka 10 ya utawala uliogawanyika katika vipindi viwili. kwa demokrasia tulioifikia sasa bado inampa nafasi ndogo mno raisi alieko madarakani kuachia ngazi baada ya awamu yake ya kwanza, na hii husababisha mmatumizi makubwa ya pesa za serikali kumwezesha aendelee kwa kipindi kijacho hata ikibidi kwa matumizi ya rushwa au mabavu. kwaiyo miaka 7 afu anag'atuka inatosha kabisa

pili'kipindi cha miaka mitano cha awamu ni kipindi kifupi sana kwa raisi alielo madarakani kufanya mabadiliko makubwa ya kisera na kiuchumi. mabadiliko ya kiuchumi na hali ya maisha ya raia hayawezi kubadilika katika kiwango cha kuwa noticed kwa muda wa miaka mitanoN hivyo ni vyema pia kama akiongezewa miaka miwili ili malengo ya kukuza uchumi yaweze kuonekana.

tatu, kipindi cha miaka saba cha utawala wa raisi husika kitakuwa na chaguzi mbili za wabunge wenye awamu za miaka mitano, nikiwa na maana awamu ya kwanza ni ile itakayofanyika katika uchaguzi mkuu wa raisi na wabunge na awamu ya pili ya wabunge ni pale ambapo raisi atakuwa amemaliza miaka yake mitano na kubakiza miwili. mantiki ya hii ni kwamba kwanza kitawapa wananchi fursa ya kubadili wabunge katika awamu moja ya uongozi kama wakibaini sera za raisi hazitekelezeki kwa uzembe au udhaifu wa mmbunge wao, pia itampa raisi nafasi ya kufanya kazi na bunge tofauti tofauti lenye ari na uzoefu tofauti sio kama sasa wabunge wamekuwa wale wale (mabadiliko kidogo tu) kwa awamu zote za uongozi
 
Hoja zako dhaifu pia! Point no.1 wewe unaamini mpaka leo rasi kuwa mtoto basi atapelekeshwa? Vipi KIM wa North Korea? Na kama una hofu ya ujana wake may be kwenye uwizi pia chaka, hao wazee marais ndio tunaowaona daily wanapelekeshwa Africa na sehem kubwa ya dunia..kwani marais wa sasa wengi si wazee na mbona vibaraka/wezi wa kupelekeshwa kama unavyodai juu hapo??

Nashukuru ume-point out Kim Jon-un wa North Korea. Huyu dogo is busy playing with toys. Wanaoendesha nchi ni wengine kabisa. Na pia wanaofaidi nchi ni wengine. Kim hana mbele wala nyuma zaidi ya kupiga makofi, na kusubiri appointment ya kwenda kwa kinyozi to maintan his punk-style.

Kwa Tanzania, I am yet to see a 35 yrs chap mwenye uwezo kukataa offer ya suti.
 
Sasa nimenusa na kutambua kiburi na kiherehere cha ZZK kinatoka wapi!
 
Ukitakafari kwa kina, 'mbunge mwenza' technically ni viti maalum. Wanachofanya hawa walafi wa vyeo kupumbaza watu kuwa wanataka kufuta viti maalum lakini wanarudisha kwa 'jina' la mgombea mwenza. This is 'structural unemployment' Mbunge mwenza maana yake nini hasa?

Kama sikosei sasa tuna Wilaya 133 (naomba nisahihishwe), kwa maana hiyo tutakuwa na wabunge 266 (133 x 2=266). Hapa kila mtu atakuwa mbunge kamili kwa maana ya malipo/posho etc.

Tujiulize, kama tuna uwezo wa kuhudumia (posho etc) wabunge 266 kwa nini tusitenge majimbo 266 ili kila mmoja akagembee kwenye jimbo badala ya huu UKUPE? Kuna Wilaya nyingine ambazo ni kubwa sana - kioneo na hata kwa idadi ya watu. Mfano Kinondoni ni Wilaya, kuna watu wangapi Kinondoni? Kwanini tusiwe na formula ya kugawa majimbo ili kuhakikisha uwiano mzuri katika representation?

Nakubaliana na wewe kuhusu kugawa upya majimbo kwa kuzingatia idadi ya watu. Wilaya zenye watu wengi zaidi ndio ziwe na jimbo zaidi ya moja nyingine zibaki kama jimbo moja tu. Hilo suala la wagombea wenza wasituletee halina maana yoyote. Kwanza hata hivyo viti maalum havina maana yoyote! Vifutiliwe mbali! Sio mambo ya kutupa sie kazi ya kulipa vilaza kodi zetu badala ya hizo pesa kufanya shughuli za kimaendeleo. Hiyo mishahara na posho za viti maalum bora zingekuwa zinajenga nyumba za waalimu au kununua madawati watoto wasikae chini.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Uraisi miaka saba? Hata kama ni kipindi kimoja siungi mkono hoja hiyo hata kidogo.
Miaka mitano mitano kwa mihula miwili bado inafaa sana.
Viti maalum kuondolewa naunga mkono hoja hiyo lakini mgombea ubunge kuwa na mgombea mwenza siungi mkono. Wazo langu wilaya ziwe majimbo ya uchaguzi na kuwe na wagombea wanaume na wanawake. Ukiweka mgombea mwenza itasababisha wagombea wabovu kuchaguliwa kwa kubebwa na wale wazuri.

Kwahali tuliyonayo sasa ingekuwa hata 4 kama marekani kwani huyu jamaa mwakani inagekuwa mwisho.
au wangeweka option ya kuchagua kati ya 3-7, akiwa mbovu bunge limtoe hata kwa mitatu!
 
pamoja na kwamba yataongelewa mengi juu ya maoni haya, na kwa kuwa kila mmoja wetu hupenda kuskia kile anachotegemea kusikia, na ikiwa tofauti ndio mtafaruku kama huu huwa unatokea.

kwa mimi binafsi sioni kama kuna shida yoyote kwa raisi akiwa madarakani kwa miaka 7, maana ni michache zaidi kwa nchi yenye demokrasia changa kama tanzania kuliko miaka 10 ya utawala uliogawanyika katika vipindi viwili. kwa demokrasia tulioifikia sasa bado inampa nafasi ndogo mno raisi alieko madarakani kuachia ngazi baada ya awamu yake ya kwanza, na hii husababisha mmatumizi makubwa ya pesa za serikali kumwezesha aendelee kwa kipindi kijacho hata ikibidi kwa matumizi ya rushwa au mabavu. kwaiyo miaka 7 afu anag'atuka inatosha kabisa

pili'kipindi cha miaka mitano cha awamu ni kipindi kifupi sana kwa raisi alielo madarakani kufanya mabadiliko makubwa ya kisera na kiuchumi. mabadiliko ya kiuchumi na hali ya maisha ya raia hayawezi kubadilika katika kiwango cha kuwa noticed kwa muda wa miaka mitanoN hivyo ni vyema pia kama akiongezewa miaka miwili ili malengo ya kukuza uchumi yaweze kuonekana.

tatu, kipindi cha miaka saba cha utawala wa raisi husika kitakuwa na chaguzi mbili za wabunge wenye awamu za miaka mitano, nikiwa na maana awamu ya kwanza ni ile itakayofanyika katika uchaguzi mkuu wa raisi na wabunge na awamu ya pili ya wabunge ni pale ambapo raisi atakuwa amemaliza miaka yake mitano na kubakiza miwili. mantiki ya hii ni kwamba kwanza kitawapa wananchi fursa ya kubadili wabunge katika awamu moja ya uongozi kama wakibaini sera za raisi hazitekelezeki kwa uzembe au udhaifu wa mmbunge wao, pia itampa raisi nafasi ya kufanya kazi na bunge tofauti tofauti lenye ari na uzoefu tofauti sio kama sasa wabunge wamekuwa wale wale (mabadiliko kidogo tu) kwa awamu zote za uongozi

Ndugu yangu sijui hesabu zako umezipigaje, unaposema wabunge watachaguliwa pamoja na rais na kisha uchaguzi mwengine wa wabunge tu wakati rais akifikisha miaka mi5 awa watakakaa kwa muda gani? Maana baada ya miaka miwili lazima uchaguzi wa rais ufanyike sasa wabunge wa miaka miwili wa nini? kwangu mimi naona mfumo wa sasa uendelee na miaka 35 ya urais sina tatizo nayo lkn ubunge mwenza ni kupoteza pesa za walipa kodi bure.
 
Hayo ya miaka 7 ni danganya toto, kinachotafutwa hapo ni miaka 35. Penda msipende miaka ya urais itabadilishwa.
 
Hii habari mbona haieleweki, si kuna warioba anakusanya maoni ya katiba? Sasa hao wabunge vipi tena? au ndo walikuwa wanatoa maoni kwa warioba?
 
35 year kwa rais ni vema naunga mkono, na kwa wale wanao sema rais lazima awe na umri mkubwa ndio amepita mikikimiki mingi si kweli kunauwezekano kuna mtoto wa umri wa miaka 5 amepita kwenye dhahama ya maisha kuzidi rais aliye madarakani.

pili mnapaswa kufahamu kuwa rais ni institution na si mtu mmoja kama mnavyo fikiria so hakuna haja ya kuweka watu kwa umri mkubwa, wakati wajua mtu anavyo zidi kuwa mkubwa uwezo wake wa kufikiri na kutunza kumbukumbu unapungua.
 
Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.

1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengata sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.

2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!

3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?

ZZK hahahahaha ni hatari kabisaaa
 
Kwa tulipofikia tutangaze tenda wazungu waje kututawala kwa mkataba tumeshindwa tumejaribu hatuwezi tumelala

HILI NI WAZO ZURI SANA. Hasa hilo la kutangaza tenda. Nina mtoto wa miaka 35. Pamoja na kisomo chake na uwezo wake angeamua kugombea uraisi 2015 atakapokuwa na miaka 37 nitakuwa wa kwanza kumpigia kura ya NO. Kwa nchi zetu hizi mgombea uraisi asiwe chini ya miaka 45.
 
Back
Top Bottom