Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Napinga vifuavyo....----....

1: Rais ibakie 40 yrs plus other qualifications...

2. Futa viti maalum.... NA HAKUNA MGOMBEA MWENZA HATUFANYI BIASHARA AU HARUSI.... KWANI MAKAMU WA RAIS ANA KAZI...?? ni mzigo tu kwa wananchi...

3: Vipindi vya ubunge na urais viwe miaka 5 mitano... yaani ukishatumikia for 10yrs ONDOKA UNATAKA NINI.... ??

4. 35 yrs bado kwa urais ... bado bado.... Zitto asipenyeze his tactics & hizi ni bills na zikipita zisipite kumfavour a SINGLE GUY...
 
Hili la kipindi cha rais 7 years mmmh!!!!!!!!!!

Naunga mkono hoja ya 35 years...................... ZZK for presidency!!!!!!!!!!!!!!
 
maoni yamejaa ubinafsi si kwa maslahi ya taifa,ndio maana tunapinga wabunge kuwemo kwenye bunge la katiba kwani wataenda kutetea maslahi yao badala ya kutetea maslahi ya taifa

teh,teh, wameona moto wa vitu maalumu unawaka kuliko walivyotegemea wameamua kupendekeza makamu mbunge ili waendelee kuwepo. Pumbaf zao! Kazi zao zipi zaidi ya kula kodi zetu na kupitisha sheria za kutuachia 4 percent kwenye madini? Misamaha kwenye mafuta, vifaa na kila kitu kiendacho migodini? Kupitisha ununuzi wa vifaa second hand ili watuletee fourth hand? Hii katiba itakuwa hovyo kwa vyovyote vile.
 
uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa lazima uwe sawa. kwa vile wananchi wanaweza kuchagua kiongozi wao akiwa na miaka kumi na minane. basi pia awe na uwezo wa kuchaguliwa akiwa na umri huo. ikiwa atagombea nafasi yyte hata urais.

wananchi wana haki ya kuamua. kama wamchague wa umri gani, wa miaka mia kama bbi kidude au kumi nane. huenda ikatokea tukawa na vijana ambao sisi sote tukaamini ana uwezo na sifa za kuwa rais wetu. ila umri ati iwe kikwazo. tupanueni demokrasia pana. kuweka umri miaka 35 au 18 haimaanishi kua watanzania watachagua umri tu pasipo kuangalia misingi mengine, ikiwemo busara na hekima pamoja na uwezo wake wa nafasi anayoitaka kutuwakilisha

nnawataka watanzania wenzangu tuwe wana demokrasia wa kweli. umri tusikifanye kizingiti
 
Wabunge wote ni wanfiki na wabinafsi tena kama Zitto, Shibuda na wabunge wa CCM hawa jamaa wana upunguani uliokithiri.
 
hata kama baadhi ya yaliopendekezwa kimtazamo ni pumba, hatuna budi kuheshimu mawazo yao nasi kuchangia yetu kwa kutoa hoja nzuri hapo tutajenga demokrasia ya kweli,
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Asante kwa kutujuza, ila haya mambo kwa nini yanajadiliwa bungeni wakati tuko kwenye Mchakato Wa kuandika katiba mpya?

Ina maana CCM ikipitisha haya itakuwa imetudharau wananchi!

Mkuu.
Mimi nimeshangazwa na mambo machache.
1. Kwanini wabunge wafanywe so special kufuatwa bungeni wakati walitakiwa kutoa maoni yao mbele ya walio wachagua kwenye majimbo yao, wilaya zao, au mikoa yao?!

2. Kama wananchi ndio wamewachagua wawakilishi wao (wabunge) kuna mantiki gani ya kuwapa nafasi ya kipekee wabunge bila kuchanganya mawazo yao naya wananchi wao?! Yaani kama kamati ya kukusanya maoni imepita Lushoto basi mawazo ya wananchi wa Lushoto yaungane naya wabunge wao.

Kinacho nipa mashaka ni kwamba maoni ya wabunge yanaweza kupewa uzito mkubwa kuliko maoni ya wananchi kwa kisa tu kuwa yamejadiliwa na wabunge ambao ki mantiki wao ndio wanafanya bunge kuwa mhimili wa serikali.
 
Hili la kipindi cha rais 7 years mmmh!!!!!!!!!!

Naunga mkono hoja ya 35 years...................... ZZK for presidency!!!!!!!!!!!!!!
Ssa nimeamini hii story nilisikia mahali kumbe ndio maana Mnyika anachafuliwa watu wanalenga 2022
 
Nimesoma gazeti la Mwananchi kuna mbunge mmoja kijana kasema wanaotaka umri wa urais uwe miaka 45 hawana hoja hii imekaaje?
 
Tujiandae kumpokea Zitto Kabwe.
 
Hiyo ya miaka 35 isije kuwa ni sababu ya ZZK kutaka nae achukue form!ni kweli anakuwa amekomaa kiasi hicho cha kuchukua ofiki kubwa kuliko zote?ni mtazamo tu nafikiri 40 inafaa si 35,bado anakuwa hajawa a subira,busara zinazostahili na uvumilivu wa ki-rais....maoni yangu tu
 
:whistle:Kikubwa ninachokiona kwa wabunge ni kuwa yapo mambo ya msingi waliyoyataja kama vile idadi ya wizara, uteuzi na mamlaka ya rais lazima yapimwe siyo kumwacha afanye atakavyo. Lakini viwepo vigezo vya nani awe mbunge kwa maana ya uwezo na upeo maana hii ndo inapelekea kuwa na bunge la kijinga lisiloweza hata kusoma na kuelewa muswada kisha kuburuzwa tu. Hakuna haja ya mgombea mwenza wa ubunge, nini maana yake?:target:
 
Wakuu.
Habari hii nimeichota kwenye gazeti la Tanzaniadaima la leo 3 Nov,2012.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ametaka umri wa kugombea urais ushushwe kutoka miaka 40 hadi kufikia 35.

Zitto ambaye amekuwa akihusishwa na harakati za kuusaka urais mwaka 2015, huku kigezo cha umri kikitajwa kuwa kikwazo, alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa maoni yake kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyofika jana mjini hapa kukusanya maoni ya wabunge.

Akitoa maoni yake, Zitto alisema ni ushamba kwa nchi kama Tanzania kuweka umri mkubwa kama sifa ya kugombea urais.

“Umri wa kugombea urais, Rwanda wenzetu wanaruhusu miaka 35, Burundi miaka 35, Kenya miaka 35, Marekani miaka 35, Afrika Kusini miaka 35…Sisi ni ushamba tu, hakuna sababu ya kuweka umri mkubwa,” alisema Zitto ambaye wakati akianza kuchangia alitania akisema kuwa itakapofika mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 39.

Mbali na Zitto, wengine waliounga mkono hoja hiyo ni pamoja na Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy (CCM), Mbunge wa Tarime, Chacha Nyambari Nyangwine (CCM), Mbunge wa Nzega, Dk. Khamis Kigwangwala (CCM), Mbunge wa Viti Maalumu, Dk. Prudenciana Kikwembe (CCM) na Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agripina Buyogera (NCCR-Mageuzi).

Kwa upande wake, Keissy alipendekeza umri wa kugombea urais iwe kati ya miaka 35-40 kwani umri huo ni watu wenye nguvu.

“Hii nchi ni kubwa sana… ina milima na mabonde, tunataka rais ambaye ataweza kutembea nchi nzima na mabonde yake, hatutaki kusikia rais ambaye baada ya siku mbili tukasikia ameenda India, Pakistan kutibiwa,” alisema.

Nyangwine alipendekeza miaka 35 na kuendelea na kuongeza kuwa, hali hiyo itatoa nafasi kwa vijana kushiriki, huku Dk. Kigwangala akisema haoni sababu ya umri kuwa zaidi ya miaka 35 kwa mtu kuwa rais.

Zitto amekuwa akitajwa kuusaka urais 2015, huku akipigania sifa ya umri kwa mtu kuwa nafasi hiyo ipunguzwe kutoka miaka 40 kwa mujibu wa katiba ya sasa hadi 35.

Tayari mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini amewahi kukaririwa mara kadhaa akisema kuwa hana mpango wa kugombea tena ubunge ifikapo mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.

Mbali na hoja hiyo ya umri wa urais, nyingine ambayo ilionekana kuwagusa wabunge wengi ni ile ya Muungano.

Wabunge wengi hasa wa kutoka Zanzibar, walionekana kutotaka Muungano uvunjwe, badala yake walipendekeza kuwe na muundo mwingine tofauti na wa sasa.

Walipendekeza mifumo mitatu ya muundo wa Muungano. Muundo wa kwanza ni ule wa serikali tatu, muungano wa mkataba na tatu muungano wa kuwa na rais mmoja na mawaziri wakuu wawili; mmoja kutoka Tanzania bara na mwingine Zanzibar.

Wabunge waliopendekeza mfumo wa serikali tatu ni pamoja na Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa (CUF), ambaye alitaka pia uongozi uwe wa mkataba baada ya ule wa serikali mbili.

“Mfumo wa sasa umeleta matatizo sana, mimi napendekeza iwepo Serikali ya Bara ambayo sijui mtaamua kuiita Mzizima au lolote na ile ya Zanzibar, na Rais wa Muungano achaguliwe na wananchi wote kulingana na mzunguko wa kubadilishana,” alisema mbunge huyo.

Baadhi ya wabunge waliopendekeza muundo wa serikali tatu na ule wa mkataba ni pamoja na Mbunge wa Tumbe, Rashid Ali Abdallah (CUF), Mussa Kombo (Chake Chake), na Kombo Hamis Kombo (Magogoni) ambao wote ni wabunge wa CUF.

Wengine ni wabunge wa viti maalumu, Easter Bulaya na Diana Chilolo, wote kutoka CCM.

Kwa upande wa wabunge waliokuwa wakiunga mkono mfumo wa serikali mbili, wengi wao walionekana kuwa ni wa CCM.

Miongoni mwao ni pamoja na Mbunge wa Manyoni Mashariki John Chiligati (CCM), Mbunge wa Bunda, Steven Wassira (CCM), Mbunge wa Dole, Silvester Mabumba (CCM), Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Zakhia Meghji, Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba (CCM) na wengine. Hata hivyo, wabunge hao waliokuwa wakitetea muundo wa serikali mbili walipendekeza uwepo utaratibu wa kushughulikia kero zinazowakabili Wazanzibari, huku wakitaka iundwe tume ya kushughulikia kero hizo.

Wengine walipendekeza Zanzibar iachwe huru katika masuala ya mafuta, bandari pamoja na kutaka isaidiwe kiuchumi.

Katika hilo, Chilligati alisema; “Kama muungano ungekuwa ni sumu inayojaribiwa, tungethubutu kuuvunja kwa muda kidogo, kule Zanzibar Watanzania elfu 15, na Wanzanzibari walioko bara laki 2.5 waonje adha ya kutafuta hati ya kusafiria au waambiwe wahame, tungejaribu kufanya hivyo.”

Alikosoa mfumo wa serikali tatu, Chiligati alisema unaongeza gharama kwa sababu utahitaji Baraza la Mawaziri na rais mwingine, na kwamba Tanganyika iliyokufa itabidi ifufuliwe.

Mbali na hilo, suala la mgombea binafsi nalo lilichukua nafasi kubwa katika maoni waliyokuwa wakichangia wabunge hao.

Wabunge wengi walipendekeza Katiba ijayo itamke wazi juu ya mgombea binafsi, ikiwa ni pamoja na uwepo wa Mahakama ya Katiba.

Aidha, wabunge wengi walitaka viti maalumu viondolewe na kupendekeza mfumo mwingine wa kuwanyanyua wanawake, ikiwa ni pamoja ule wa kutaka mbunge anayesimama katika jimbo asimame na mgombea mwenza mwanamke na atakapopita, mgombea mwenza naye atakuwa mbunge.

Suala la ukubwa wa madaraka ya rais nalo lilionekana kuwagusa wabunge wengi, ambao karibu wote waliochangia wakiwamo wachache wa CCM, walitaka yapunguzwe.

Pia walitaka utaratibu wa mawaziri kutokana na wabunge, ufutwe na kupendekeza mawaziri wateuliwe nje ya Bunge na wawe wataalamu wa wizara husika.

Kuhusu suala la mihimili mitatu, yaani Serikali, Bunge na Mahakama, wabunge wengi waliotoa maoni walitaka Katiba ijayo itamke wazi kuwa ni kosa kuingiliana na mihimili mingine.

Kwa upande wa wahujumu uchumi, baadhi ya wabunge waliotoa maoni walitaka watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo wanyongwe.

Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema hakuna sababu ya kulinda haki ya mhujumu uchumi ambaye amepewa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kununulia dawa na badala yake anaweka fedha mfukoni halafu unalinda haki ya mtu mmoja.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ambaye alipata wakati mgumu, alisema kabla ya kuanza kukusanya maoni kwa wabunge alipata woga.
 
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, pamoja na mambo mengine..Wataka Umri wa mgombea uraisi upunguzwe tka miaka 40 hadi 35...Wataka Mawaziri wateuliwe nje ya wabunge...Uteuzi wa viongozi wa juu uthibitizhwe na Bunge...Idadi ya Wizara ijulikane kikatiba na ziwe chache...

Wataka matokeo ya rais yapingwe mahakamani...Muungano wa kimkataba (treaty-based union)...Rais wa Zanzibar awe Makamu wa rais...Majina matatu ya jaji mkuu yapendekezwe kwa rais kwa uteuzi na jaji athibitishe na Bunge na Rais asiwe na mamlaka ya kuwaondoa mpaka ridhaa ya wabunge, Hapa inahusu pia uteuzi wa CDF,IGP, Mkuu wa TISS, Magereza, Uhamiaji nk....

Wataka pia ubunge na udiwani uwe na kikomo...Viti maalumu vifute na badala yake majibo yawe ni wilaya na kuwe na mgombea ubunge na mgombea mwenza wake..Kama mgombea ni mwanaumwe, mgombea mwenza awe mwanamke na akichaguliwa mmoja wote wameshinda kama kwa rais...Uraisi uwe wa Kipindi kimoja cha miaka 7.....

Pia uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship)...Kuwe na tume kikatiba itakayo shunghulikia kero za Muungano...Chiligati ataka Articles of Unioni zirejee kama ilivyokuwa mwanzo mambo 11...Mafuta gesi visiwe vya Muungano (hapa ni wabunge wa CCM na CUF bara na Visiwani waliungana)....Ubunge na Udiwani uwe na kikomo cha vipindi viwil (Miaka mitano kila kipindi)....Na mambo mengine mengi...
Source Mimi Mweneyewe Bungeni Dodoma leo...

Nilazima watanzania wajuwe kumpa nchi kijana nikutaka mlipuko wa kisiasa. Nikweli vijana ni taifa la kesho lakini kumpa kijana taifa hili ni hatari sana. Mim nikijana nina miaka 30. Lakini napinga kumpa kijana wa 35 hii nchi ni tamaa na wazee wasikubali. 35 bado kijana hajatulia sasa tusitake kuijaribu aman yetu tusubiri 40. Tufundishwe na wazee wetu then watatupa nchi.
 
Raisi akiwa na miaka 35, atakapoacha uraisi hata kama ni kwa miaka 10 atakuwa na miaka 45. Je na uchumi huu tutaweza kumtunza rais mstaafu mwenye miaka 45? Mimi naona rais awe ma miaka 55 na kuendelea.











Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.

1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengatamani sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.


2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!

3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
walimsahau DPP huyu naye lazima awe approved na bunge maana anamadaraka makubwa sana. vipindi vya urais vibaki kama vilivyo au tuige marekani kufanya after 4 years hii ya saba siielewi. Chiligati namuunga mkono kuwa article of the union zirudi za kwanza kwani zitaipa zbar hadhi yake.
 
Another silly season bungeni. Miaka 5 tu imetuchosha.....iyo 7 itakuwaje???? Yesu na maria!!!
 
1. Mwanasheria mkuu athibitishwe na jopo la wanasheria/chama cha wanasheria na sio bunge. Hii ni mihimili miwili tofauti.
2.Jamani umri wa uraisi inatakiwa uwe uleule sababu a)Hii si nafasi ya kufanyia masihara tunahitaj mtu ambaye ana experienc na utendaji kaz serikalin, vjana tulionao weng ni malimbukeni tu.
3.Kuhusu kipind cha uongoz wa rais kiwe vilevile.Ikiwa hvyo watu wakipata watakuwa wanajinufaisha wenyewe.
4. Mbunge mmoja anatosha kabisa.
 
Back
Top Bottom