Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Wabunge wataka Umri wa kugombea Urais uwe 35; Zitto asema umri mkubwa ni ushamba

Hizi hoja walichangia Asubuhi au Jioni?

Kama ni jioni, mmhh! Maana huwa vikao wanakula kwanza mambo yao ya kuvuruga ubongo, wanafikiria Anticlockwise.

Hapo kuna hoja za kipuuzi.
1. Kupunguza umri wa Raisi.
2. Kipindi cha raisi kuwa kimoja cha 7yrs.
3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza, huu ni upuuzi uliokithiri.
 
Hatutaki mapendekezo yao walikuwa wapi siku zote, hizi ni njama za kutaka kuhodhi maoni ya katiba waache wananchi watoe maoni yao/yetu

Nakuunga mkono mkuu, hizi ni njama za ccm kuuteka mchakato wa kutoa maoni. kwa staili hizi itakuwa ngumu sana hii nchi kuendelea.
 
Lengo la kutaka mgombea ubunge kuwa na mgombea mwenza ni nini hasa? Je mgombea anaposhinda huyo mwenza nae atahudumiwa kwa kodi hii hii? Au itakuaje? Ila kufanya wilaya kuwa majimbo ya uchaguzi ni bora zaidi maana itapumguza idadi ya wabunge na hivyo kupunguza gharama.
 
Hili la urais kuwa miaka 35 linalenga zaidi kuisambaratisha CDM, kwani Mh.Zitto lazima atalianzisha tu hapo 2015.

sio zitto tu januari makamba je atatulia ipite kimya hiyo bahati? hata mimi nitagombea kupitia vile vyama vyetu vya dharura na nyongeza mfano cck!
 
Hatutaki mapendekezo yao walikuwa wapi siku zote, hizi ni njama za kutaka kuhodhi maoni ya katiba waache wananchi watoe maoni yao/yetu

ndugu yangu wabunge nao ni wananchi na raia wa tz wenye haki kikatiba kutoa maoni yao ila hawana nafasi ya kutulazimisha maoni yao ndio yawe maoni ya wananchi wote!
 
-Nakubaliana na suala la kushusha umri wa Urais.Inawezekana kuna uwezekano wa kupata wenye uwezo wa kuwa Rais

-Nakubaliana na hoja ya kuwa na approval ya uteuzi wa CDF,Chief Justice,IGP,AG na CAG
-Pia tufikirie kuwa na bicameral parliamentary system.Kama ni uwakilishi tuachane na ukuu wa wilaya na mkoa kwa kufanya decentralization

-Hapo kwa serikali tatu tungekuwa na federal system ambayo inakidhi hoja yangu hapo juu ya decentralization

-Nashindwa kuelewa ni kwa nini wabunge hawajaongelea kuhusu impeachment ya Rais.

Pia ningependekeza vipindi vya urais viwe miaka 4 kwa twi terms

-Pia hapo kwenye bicamneral parliament.Bunge la law chamber liwe miaka 3 kwa vipindi viwili na chaguzi zifanyike kwa kupishana na uchaguzi wa Rais uwe baada ya uchaguzi wa Bunge na magavana

sikubaliani na wewe kwenye swala la umri wa raisi. Tunahitaji mtu aliyepevuka vya kutosha. Miaka 35 bado sana!
Binafsi nataka muungano uvunjwe. Kwahiyo hoja ya rais wa z'bar kuwa makamu wa rais inakufa!
 
Kwa tulipofikia tutangaze tenda wazungu waje kututawala kwa mkataba tumeshindwa tumejaribu hatuwezi tumelala

unaweza ukakoma yote ndugu yangu ila usije ukakoma kufikiri juu ya mema kwa taifa hili maana bado una ya nafasi kuleta mabadiliko chanya yenye manufaa na mustakabali mwema kwa taifa, wadhungu ni kina na hasa hata tuweke/tutangaze zabuni kwao wapo wabongo wakikabidhiwa hii nchi ndani ya miaka mitano ya kwanza taifa litakaa kwenye mstari!
 
sikubaliani na wewe kwenye swala la umri wa raisi. Tunahitaji mtu aliyepevuka vya kutosha. Miaka 35 bado sana!
Binafsi nataka muungano uvunjwe. Kwahiyo hoja ya rais wa z'bar kuwa makamu wa rais inakufa!

Mimi nataka ushushwe.Mataifa mengi yanatambua mtu mwenye miaka 35 anaweza kuwa Rais.Sisi kwa nini tunaweka vizuizi? je watanzania tunachelewa kukomaa?Mbona umri wa ukomavu kisheria katika kufanya maamuzi na kupiga kura ni miaka 18 kama ilivyo kwa nchi nyingine?

Mbona Nyerere alikua Rais akiwa under 40?

Nakubali kuna watu walikua marais wakiwa under 40 lakini walifanikiwa kuongoza kwa weledi na kuna wengine waliofeli vibaya.

Come on Filipo!
 
Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.

1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengata sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.

2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!

3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?

Hoja zako dhaifu pia! Point no.1 wewe unaamini mpaka leo rasi kuwa mtoto basi atapelekeshwa? Vipi KIM wa North Korea? Na kama una hofu ya ujana wake may be kwenye uwizi pia chaka, hao wazee marais ndio tunaowaona daily wanapelekeshwa Africa na sehem kubwa ya dunia..kwani marais wa sasa wengi si wazee na mbona vibaraka/wezi wa kupelekeshwa kama unavyodai juu hapo??
 
sio zitto tu januari makamba je atatulia ipite kimya hiyo bahati? hata mimi nitagombea kupitia vile vyama vyetu vya dharura na nyongeza mfano cck!

Daah, u made my day, vyama vya dharura na nyongeza!

Ila wabunge wetu sijui wameacha wapi vichwa. Urais miaka 7! Ubunge mwenza khaa! Urais miaka 35, please no.
 
hv haya mambo ya ujinsia yanakujae?, siku hz kila kitu wanaweka ujinsia, mi sikatai mambo ya ujinsia ila nakataa na napingana na wale ambao wanadhani kuweka usawa kijinsia ni kwa kulazimisha jinsia fulani iingie kwa upendeleo bungeni, tumeona wanawake wameingizwa ila impact yake ndo tumeona wao wenyewe wameomba waondolewe maana hivyo viti maalum ndo vimewashushia heshima kabisa.SASA ETI WANATAKA KUFUTA VITI MAALUM LAKINI WANAPENDEKEZA WABUNGE WAWE NA WAGOMBEA WENZA WA JINSIA TOFAUTI WAKATI NI KITU KILEKILE, WACHA WATU WACHUANE KWA SERA SIYO KWA JINSIA ZAO BANA
 
Hizi hoja walichangia Asubuhi au Jioni?

Kama ni jioni, mmhh! Maana huwa vikao wanakula kwanza mambo yao ya kuvuruga ubongo, wanafikiria Anticlockwise.

Hapo kuna hoja za kipuuzi.
1. Kupunguza umri wa Raisi.
2. Kipindi cha raisi kuwa kimoja cha 7yrs.
3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza, huu ni upuuzi uliokithiri.
Nyerere alichukua nchi akiwa na umri gani? Na mbona leo anaitwa mpaka baba wa taifa kwa performance yake? Zinduka usifate mkumbo.
 
sikubaliani na wewe kwenye swala la umri wa raisi. Tunahitaji mtu aliyepevuka vya kutosha. Miaka 35 bado sana!
Binafsi nataka muungano uvunjwe. Kwahiyo hoja ya rais wa z'bar kuwa makamu wa rais inakufa!

kama kupevuka kunapimwa kwa umri huu ni wakati wa kuwazungumzia kina mzee makamba, malecela na mtei kuwa wagombea urais!
na huyu aliyetambulika kama rais kijana aliyotutenda tumeyaona na bado anaendelea kutuumiza!
kwetu sisi kama taifa tunahitaji sifa ya ziada kwa rais ajae na hakika umri si suala la msingi ikiwa tutaweka vigezo vingine vya msingi tutakuta umri unajinyambua wenyewe,mfano tukihitaji sifa kiongozi ziwe
1.uadilifu usio na shaka. (lazima kutakuwepo maeneo ya kupima kwa hakika ktk cv ya muhusika)
2.uzoefu katika uongozi. (lazima tutahitaji walau tuone utumishi ktk uongozi wenye ufanisi kabla ya kugombea nafasi ya urais kwa mfano tunaweza kusema muhusika awe kwenye uongozi walau kwa awamu mbili za miaka mitano)
3.elimu, uelewa na ujuzi wa mambo.
 
Hapa hakuna kumuandalia Zitto urais kwani haka katotot katalizika taifa kaburini, hivi matatizo ya wakina ponda na farid wa uamsho zitto atayaweza kweli? Mikopo vyuo vikuu huyu mtoto atayaweza kweli? Msimamo wake juu ya muungano ukoje? Je msimamo wake kuhusu ufisadi wa rafiki zake wakina Rostam ukoje? Vip kuhusu Jack zoka ataweza kweli kumuwajibisha?

Zitto bado ni punguani na juha mkubwa mithili ya uyoga na marikebu na kamwe hawezi kuongoza nchii na CHADEMA mkifanya ufallla kumuweka mimi kura yangu nitampa Lipumba au Lowasa..

CHADEMA acheni upumbavu na ungese kumuweka Zitto awe Rais.
 
kama kupevuka kunapimwa kwa umri huu ni wakati wa kuwazungumzia kina mzee makamba, malecela na mtei kuwa wagombea urais!
na huyu aliyetambulika kama rais kijana aliyotutenda tumeyaona na bado anaendelea kutuumiza!
kwetu sisi kama taifa tunahitaji sifa ya ziada kwa rais ajae na hakika umri si suala la msingi ikiwa tutaweka vigezo vingine vya msingi tutakuta umri unajinyambua wenyewe,mfano tukihitaji sifa kiongozi ziwe
1.uadilifu usio na shaka. (lazima kutakuwepo maeneo ya kupima kwa hakika ktk cv ya muhusika)
2.uzoefu katika uongozi. (lazima tutahitaji walau tuone utumishi ktk uongozi wenye ufanisi kabla ya kugombea nafasi ya urais kwa mfano tunaweza kusema muhusika awe kwenye uongozi walau kwa awamu mbili za miaka mitano)
3.elimu, uelewa na ujuzi wa mambo.

Cha ajabu hayo hawajayajadili mkuu na ndiyo maana wamesahau impreachment kwa Rais na inabidi turahisishe hii process kwa kuzingatia wingi wa uwakilishi wa moja kwa moja kwa wananchi
 
Penye miaka saba hapo nimechukia sana. Yaani mnakuwa na rais km kikwete alafu mnasubiri miaka saba iishe! Tutakuja kuua watu kwa presha
 
Tatatizo la taasisi ya urais si umri bali uungu mtu unaomfanya rais wetu ajifanyie atakavyo hata bila kuwa na nguvu za kisheria za kumzuia. Hivyo tungeshughulikia kuweka mipaka kwenye cheo cha urais badala ya kuhangaishwa na umri kwa vile kuna personalities tunazotaka zigombee au kuziengua. Kama wanataka umri wa kuanzia basi waweke na kikomo pia.
 
Back
Top Bottom