Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili la urais kuwa miaka 35 linalenga zaidi kuisambaratisha CDM, kwani Mh.Zitto lazima atalianzisha tu hapo 2015.
Kwakuwa tunakubaliana kwamba ujana unakomea kwenye umri wa miaka 35 basi nakubaliana na hoja ya kupunguza umri wa mgombea uraisi ili wale tuliovuka ujana tupate haki ya kugombea uraisi badala ya kutulazimisha kuwa wapiga kura tu katika kipindi cha mpito kuelekea miaka 40.
Ila sasa twende mbele some extra miles tuweke vigezo mahsusi kwa mgombea uraisi na mojawapo na ya lazima iwe ni uadilifu wake usiwe wa kutiliwa shaka hata kidogo.
Lengo la kutaka mgombea ubunge kuwa na mgombea mwenza ni nini hasa? Je mgombea anaposhinda huyo mwenza nae atahudumiwa kwa kodi hii hii? Au itakuaje? Ila kufanya wilaya kuwa majimbo ya uchaguzi ni bora zaidi maana itapumguza idadi ya wabunge na hivyo kupunguza gharama.
Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano, pamoja na mambo mengine..Wataka Umri wa mgombea uraisi upunguzwe tka miaka 40 hadi 35...Wataka Mawaziri wateuliwe nje ya wabunge...Uteuzi wa viongozi wa juu uthibitizhwe na Bunge...Idadi ya Wizara ijulikane kikatiba na ziwe chache...
Wataka matokeo ya rais yapingwe mahakamani...Muungano wa kimkataba (treaty-based union)...Rais wa Zanzibar awe Makamu wa rais...Majina matatu ya jaji mkuu yapendekezwe kwa rais kwa uteuzi na jaji athibitishe na Bunge na Rais asiwe na mamlaka ya kuwaondoa mpaka ridhaa ya wabunge, Hapa inahusu pia uteuzi wa CDF,IGP, Mkuu wa TISS, Magereza, Uhamiaji nk....
Wataka pia ubunge na udiwani uwe na kikomo...Viti maalumu vifute na badala yake majibo yawe ni wilaya na kuwe na mgombea ubunge na mgombea mwenza wake..Kama mgombea ni mwanaumwe, mgombea mwenza awe mwanamke na akichaguliwa mmoja wote wameshinda kama kwa rais...Uraisi uwe wa Kipindi kimoja cha miaka 7.....
Pia uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship)...Kuwe na tume kikatiba itakayo shunghulikia kero za Muungano...Chiligati ataka Articles of Unioni zirejee kama ilivyokuwa mwanzo mambo 11...Mafuta gesi visiwe vya Muungano (hapa ni wabunge wa CCM na CUF bara na Visiwani waliungana)....Ubunge na Udiwani uwe na kikomo cha vipindi viwil (Miaka mitano kila kipindi)....Na mambo mengine mengi...
Source Mimi Mweneyewe Bungeni Dodoma leo...
Hoja zako dhaifu pia! Point no.1 wewe unaamini mpaka leo rasi kuwa mtoto basi atapelekeshwa? Vipi KIM wa North Korea? Na kama una hofu ya ujana wake may be kwenye uwizi pia chaka, hao wazee marais ndio tunaowaona daily wanapelekeshwa Africa na sehem kubwa ya dunia..kwani marais wa sasa wengi si wazee na mbona vibaraka/wezi wa kupelekeshwa kama unavyodai juu hapo??
Ukitakafari kwa kina, 'mbunge mwenza' technically ni viti maalum. Wanachofanya hawa walafi wa vyeo kupumbaza watu kuwa wanataka kufuta viti maalum lakini wanarudisha kwa 'jina' la mgombea mwenza. This is 'structural unemployment' Mbunge mwenza maana yake nini hasa?
Kama sikosei sasa tuna Wilaya 133 (naomba nisahihishwe), kwa maana hiyo tutakuwa na wabunge 266 (133 x 2=266). Hapa kila mtu atakuwa mbunge kamili kwa maana ya malipo/posho etc.
Tujiulize, kama tuna uwezo wa kuhudumia (posho etc) wabunge 266 kwa nini tusitenge majimbo 266 ili kila mmoja akagembee kwenye jimbo badala ya huu UKUPE? Kuna Wilaya nyingine ambazo ni kubwa sana - kioneo na hata kwa idadi ya watu. Mfano Kinondoni ni Wilaya, kuna watu wangapi Kinondoni? Kwanini tusiwe na formula ya kugawa majimbo ili kuhakikisha uwiano mzuri katika representation?
Uraisi miaka saba? Hata kama ni kipindi kimoja siungi mkono hoja hiyo hata kidogo.
Miaka mitano mitano kwa mihula miwili bado inafaa sana.
Viti maalum kuondolewa naunga mkono hoja hiyo lakini mgombea ubunge kuwa na mgombea mwenza siungi mkono. Wazo langu wilaya ziwe majimbo ya uchaguzi na kuwe na wagombea wanaume na wanawake. Ukiweka mgombea mwenza itasababisha wagombea wabovu kuchaguliwa kwa kubebwa na wale wazuri.
pamoja na kwamba yataongelewa mengi juu ya maoni haya, na kwa kuwa kila mmoja wetu hupenda kuskia kile anachotegemea kusikia, na ikiwa tofauti ndio mtafaruku kama huu huwa unatokea.
kwa mimi binafsi sioni kama kuna shida yoyote kwa raisi akiwa madarakani kwa miaka 7, maana ni michache zaidi kwa nchi yenye demokrasia changa kama tanzania kuliko miaka 10 ya utawala uliogawanyika katika vipindi viwili. kwa demokrasia tulioifikia sasa bado inampa nafasi ndogo mno raisi alieko madarakani kuachia ngazi baada ya awamu yake ya kwanza, na hii husababisha mmatumizi makubwa ya pesa za serikali kumwezesha aendelee kwa kipindi kijacho hata ikibidi kwa matumizi ya rushwa au mabavu. kwaiyo miaka 7 afu anag'atuka inatosha kabisa
pili'kipindi cha miaka mitano cha awamu ni kipindi kifupi sana kwa raisi alielo madarakani kufanya mabadiliko makubwa ya kisera na kiuchumi. mabadiliko ya kiuchumi na hali ya maisha ya raia hayawezi kubadilika katika kiwango cha kuwa noticed kwa muda wa miaka mitanoN hivyo ni vyema pia kama akiongezewa miaka miwili ili malengo ya kukuza uchumi yaweze kuonekana.
tatu, kipindi cha miaka saba cha utawala wa raisi husika kitakuwa na chaguzi mbili za wabunge wenye awamu za miaka mitano, nikiwa na maana awamu ya kwanza ni ile itakayofanyika katika uchaguzi mkuu wa raisi na wabunge na awamu ya pili ya wabunge ni pale ambapo raisi atakuwa amemaliza miaka yake mitano na kubakiza miwili. mantiki ya hii ni kwamba kwanza kitawapa wananchi fursa ya kubadili wabunge katika awamu moja ya uongozi kama wakibaini sera za raisi hazitekelezeki kwa uzembe au udhaifu wa mmbunge wao, pia itampa raisi nafasi ya kufanya kazi na bunge tofauti tofauti lenye ari na uzoefu tofauti sio kama sasa wabunge wamekuwa wale wale (mabadiliko kidogo tu) kwa awamu zote za uongozi
Kuna points tatu za kipuuzi kabisa ambazo kwa namna yoyote ile wananchi wazipinge.
1. Umri wa urais usiwe chini ya miaka 40. Cheo cha urais kimeharibika to the point kwamba kila mtu anaona anaweza kuwa rais. Tunahitaji mtu ambaye ameshakuwa tested. Kwa nchi kama yetu ambayo 'institutions' zake sio imara ni hatari sana kuweka rais-mtoto. Na mbaya zaidi Tanzania ina madini mengi, mafuta na gas. Mafioso wengata sana kupata rais-dogo ili wamplekeshe kama Kabila wa DRC.
2. Kipindi cha urais 7 yrs na kiwe kimoja. Mtu aliyetoa hii hoja anatakiwa apelekwe Keko! 7 yrs kama unakuwa na rais mwizi hakutakuwa na kitu kimabakia, na akijua kwamba hana nafasi ya pili atachukua hadi shuka!
3. Mbunge kuwa na mgombea mwenza. Another silly point. Mgombea wa ubunge awe ni mtu mmoja na asimame kwa miguu yake. Bunge la mbeleko ni kitanzi. Maana mgombea mwenza anawajibika kwa nani?
Kwa tulipofikia tutangaze tenda wazungu waje kututawala kwa mkataba tumeshindwa tumejaribu hatuwezi tumelala