Ifike wakati tuwe na Taasisi imara kuliko kutegemea maono ya mtu mmoja! Leo akija kiongozi mwingine atakuja na mtazamo tofauti juu ya wamachinga. Hivyo basi tutaishi kwa kuyumbishwa kutokana tu na maono ya kiongozi fulani na walio chini yake wataunga mkono kwa ajili ya maslai yao binafsi.
Nasikia wamachinga wanaviongozi wao, na kama kweli ni viongozi wa kweli watakuwa na tija ya kweli ya kumaliza tatizo hili bila kuongeza migogoro mingine, kama wamewekwa kufuata maono ya mtu! Wataendelea kupelekwapelekwa tu. Binafsi nafikiria mambo haya;
(i) Viongozi wa Machinga kujitokeza hadharani- kuongea na vyombo vya habari, kuhusisha mashirika ya haki za binadamu katika maongezi yao. Kuiomba serikali kusitisha zoezi mpaka watakapo kaa mezani kutafuta njia muafaka ya jambo lao.
(ii)Maandamano- Ni njia nzuri ya kufikisha kilio chao sehemu husika, njia hii imekuwa na msaada mkubwa sehemu mbalimbali Duniani na itumike pale tu njia ya majadiliano imeshindwa kuzaa matunza mazuri kwa pande zote. Miaka ya nyuma ilisaidia sana katika Taasisi na Mashirika mbalimbali lakini kwa sasa imekuwa na changamoto kubwa hapa kwetu, ila wakiweza itawashtua na kuwakumbusha wajibu wao hasa Wabunge, Madiwani na viongozi wengine.
ZINGATIA- Mpangilio mzuri unaitajika kwa ajili ya kufanya biashara vizuri bila kukera watu wengine, sehemu nyingine wamejaa barabarani hata kupita na gari au kwa miguu ni kero na kuna mazingira mengine hawaitajiki kutokana umuhimu wa eneo.