Ukweli kuna wabunge wengi wa CCM wanataka Tanganyika irudi lakini huo si msimamo wa CCM, hivyo wanataka kupiga kura ya siri. Kwa mtazamo wangu nilikuwa naona ni hekima kupiga kura ya wazi ili kuwapa nafasi watanzania kuwajua wabunge wao wanasimamia nini. Wabunge wa CCM wanaotaka Tanganyika irudi simamieni msimamo wenu ili muonekane. Ni unafiki wa hali juu kuficha kile ukitakacho eti kwa sababu ni msimamo wa chama chako.
Katiba si mali ya chama, ni mali ya watanzania na ndiyo waliokutuma huko Bungeni kwa lengo la kupata katiba mpya na bora. Ombi langu kwa wabunge wanafiki, Chama kisikupelekeshe wala kisikufanye ushindwe kusimamia kile unachokiamini na kile watakacho wananchi wa jimbo lako. Taifa kwanza na chama baadaye.