Wabunge zaidi 300 - nchi masikini kweli zina pesa nyingi

Ndio maana wanauwa watu, wanalipana mishahara Mungu ndio anajua. 300+ wabunge, wengi wao ni bogus tu hamna kitu.

Ndio maana nchi masikini umasikini wake hauishi kirahisi.
 
Nasikia kuna mbunge mpya kaingia mjengoni kaanza kushangaaa jengo la bunge.
 
Mkuu tatizo la africa liko kwenye uongozi tu na si vinginevyo, baada ya vifo vya wale wanasiasa wetu mahiri kizazi cha mwalimu, nkurumah, mandela nk, basi ikawa ni kama balaa limeshuka africa! kuna wakati unaangalia kiongozi anaongea kwa sauti kubwa hadi shingo imekakamaa anasema anapambana na umasikini unaishia tu kusema Nhiiiiiiiii...!!
 
Umewaza kizalendo sana mkuu wabunge niwengisana, kodi zinateketea bila huruma.
 
Hiyo ni njaa tu na wivu vinakusumbua, tafuta pesa achana na siasa
hv kwa nn unakuwa na akili za kuazima kiasi hcho? umeshindwa nn kujibu hoja kwa hoja? ni siasa gan unayozungumzia ww hapa??
 
unakuta wilaya 1 ina majimbo ma3,eti kusogeza maendeleo. labda maendeleo ya mbunge
 
Hivi unaweza kufikiri mambo bila kuhisi labda aliyeleta hoja yuko chama flani? Sijui hili jambo la kuwaza kwamba kila hoja inaletwa kwa kuegemea chama flani iantoka wapi.
hawa ndo akili visoda yan hawez jibu hoja badala yake anafanya personal attack
 
mm huwa nabadilisha channel kabisa assee
 
Ukianza kufatilia baadhi ya mambo kwa nchi hii unajikuta tu hasira inapanda mdogo mdogo ila basi tu, wapo kwa ajili ya maslahi yao,acha wananchi tupambane na hali zetu
 
Inashangaza wabunge wengi mno wakati kila mkoa una mkuu wa wilaya mkuu wa mkoa ,diwani, mwenyekiti na kadhalika hizo hela za kuwalipa wabunge zaidi ya 150 tanzania ingeamua kujenga visima kila wilaya kata ,zahanati.mambo yangekuwa safi Wala tusingekuwa na haja ya UCHAGUZI kila baada ya miaka mitano.
 
Viti maalum ni mzigo tu vingefutiliwa mbali

Ova
 
CCM ipo kwa ajili ya maslahi yao na familia zao .
Cha ajabu hata vyama vya upinzani miaka yote wamekaa bungeni wanafurahiya tu kuongezeka kwa majimbo ya uchaguzi na viti maalumu.
Wabunge wa CCM walipitisha hizo sheria na kuweka idadi kubwa ya wabunge ili wengine wafike Bungeni na wake zao, wengi vimada,wengine na watoto wao alimradi wanufaike na keki ya Taifa.
Mbali na yote wakajiwekea mamishahara makubwa na viinua mgongo kila baada ya miaka mitano .

Potelea Mbali wawe hata 1000 lakini waingie Bungeni kihalali basi. Sio waibe kura kwenda kuiba pesa za kodi zetu.
Tumeona tena mchakato wa wizi wa kuwapata wapinzani kwenye viti maalum. Badala ya kuachana na wabunge waliokosa siafa baada ya Chadema kugoma wao wanataka kutuletea wabunge wa NCCR. Hapo ndio utagundua kuwa kuna watu pesa za nchi hii zinawawasha hivyo wanatamani ziishe kwa Siku moja alimradi wameamua wao na sio sheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…