Wacha nimtetee kidogo goal keeper wa Fountain Gate John Nobo

Wacha nimtetee kidogo goal keeper wa Fountain Gate John Nobo

Kuna wachambuzi na baadhi ya wajinga ikiwa ni pamoja na coach wake Matano aliyemtupia lawama baada ya kufungwa goal 2

Goal keeper Nobo amefanya saves 4 kubwa na kuinusuru timu yake ila analaumiwa Kwa makosa ambayo magoli kipa hufanya

Zile goli ni kupongeza tu washambuliaji wa Yanga Mzize na Dube

Goli la kwanza mpira ulidunda,Goal keeper akapoza ili audake, Mzize akawa amefika na kumfunga
Na hili sio tukio geni kwenye football

Goal keepers wengi washafungwa sana hivi

Goli la pili. Golikipa alipokea mpira na akawa anarudisha mpira kwenye box, hivyo Dube aka press na kipa akafanya makosa akafungwa

Tukumbuke Camara alitoka mpira uliounatoka zake nje na kumpa Kijili aliyefunga goli Bora la msimu
Kiongozi wa Simba Magori alilaumu ila Camara alipata watetezi wengi

Tuheshimu football. Huu ni mchezo wa makosa bila kosa kufanyika goli halifungwi

Kumtuhumu mchezaji aliyefanya makosa kuwa ameuza ni ujinga kiwango cha lami
Mbumbumbu watakupinga. Ila ukweli ndiyo huo. Mpira wa miguu ni mchezi makosa. Ukikosea unaadhibiwa pasipo kuangalia unacheza na nani.
 
Back
Top Bottom