Taarifa hiyo imebainisha kuwa gari ya Toyota Prado ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, na kwamba ilikuwa ikiendeshwa na Neechi Msuya, huku Scania ilikuwa ikitokea Arusha na kwamba iliendeshwa na Philipo Mtisi.
Taarifa hiyo iliwataja waliofariki kwenye jali hiyo kuwa ni Neechi Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 45 hadi 50, Dayana Mageta, mfanyabishara na makazi wa Dar es Salaam anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45, Nora Msuya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 hadi 45 ambaye ni mwalimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Dar es Salaam, na abiria wa kike ambaye jina lake halikufahamika na anakadiriwa kuwa na miaka 30 hadi 35. Polisi imeeleza chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Prado kuhama kutoka upande wa kushoto wa barabara kwenda upande wa kulia kisha kogongana uso kwa suo na lori hilo.
“Miili ya marehemu imehifadhiwa Zahanati ya Lugoba kwa uchunguzi wa daktari na itakabidhiwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya maziko,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha Jeshi hilo
la Polisi limetoa wito kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara kuchukua tahadhari na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zinazoweza kusababishwa na uzembe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.