Hili mie naweza nikakubaliana nawewe kwa asilimia 100% ajali nyingi ni matokeo ya ku loose control ya magari na hii yote ni sababu ya kupenda overtake za ajabu ajabu tu[emoji41]!
Mtu anaona kuna gari inakuja upande wake anabet eti akate semi 3 halafu atoke kabla gari ya upande wake haijafika! Hio huwa ni ngumu sana kutoboa hasa ukiwa na mgari wa diesel au engine yenye horsepower ndogo on full throttle!
Ni muhimu sana pia kujua hali ya chombo chako, means uwe umekizoea kimatumizi na mwenendo wake. Mie kabla ya kusafiri hata na gari ngeni huwa lazima nizunguke zunguke nayo kwanza niangalie aerodynamics zake. Ukamataji wa brakes pia, Cornering ikoje, Sio unaazima gari tu unasafiria huelewi.