Wachaga zindukeni, VICOBA vya kuzikana ni Umaskini!

Wachaga zindukeni, VICOBA vya kuzikana ni Umaskini!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Imeibuka tabia, wanafunzi waliosoma pamoja "alumni", watu walioishi mtaa mmoja, Ukoo mmoja na kabila, Parokia au jumuia moja, kuanzisha vikundi vya Watsup na baadae kujisajili kuwa Rasmi.

Vikundi hivi huwa lazma kuwe na kisebengo ambaye ata-anzisha M-Koba na kutaka watu wachangieni iwapo mwenzao atapata msiba au ugonjwa wa kudumu.

NIWAPE SIRI: KUFA TUTAKUFA TU, NDUGU WASIPO KUZIKA , HALMASHAURI ITAKUZIKA MANA HAKUNA ATAKAYE KUBALI KUKAA NA MZOGA, wenzetu wenye asili ya ASIa wanaunda group za fursa za biashara, kuwekeza UTT , tuwekeze kwenye soko la hisa na Kufungua kampuni kugombea tenda, sisi tunawaza kuzikana tu.

Imekuwa ni ufahari kumzika mama yako, kumjazia maua rose kwenye kaburi, kuchapisha mabango, kuandika historia nzuri ya kuonyesha namna alikuwa mtu wa watu, mabango ya Sijui tutakumis, kumpost marehemu status-insta, ticktok wakati akiwa hai hukuwahi kumuweka status bali ulimuweka Zuchu, Dai na wamama wengine ambao hawakuhusu! ambayo kipindi cha uhai wake hukuwahi kumpa hata "ua mgomba" wacha mbali "rose za plastiki zile za kichina" siku ya kinamama duniani!

Mnaweka na kuandaa Bufee, watu wale mpaka wasaze, mnaweka vinywaji vikali na bia lakini kipindi cha uhai wake alikuwa anakula mashona-nguo, mchunga na miguu ya kuku na ugalli wa jero au anashindia chai kavu !

Maziko ya mama yenu mnaleta vikundi vya ngonjera na sala na kupiga kila aina ya sifa ambayo kipindi akiwa hai hamkuwahi kufanya hivyo!

huu ni unafiki na ndio unaleta umaskini.

HITIMISHO:
Mtu yeyote, asiniunge magroup ya michango ya kuzikana, niunge kwenye group za kupeana biashara, viwanja, kazi na uwekezaji!​
 
Kwenye kusanyiko lolote wakiwepo wachaga wawili lazima kianzishwe kikoba cha kuzikana.

Hawa watu hawajawahi kuwaza kingine beyond hela
Al Watani, Wanazingati kuzikwa kwa hesha,ma kuliko kuish kwa heshma, Ndio maana hata hizi Speacil Hire ni safari za uchagani tu, bora hata wazaramo wanaenda ucheza ngoma !
 
Hizo hela wanizipata wapi za kuzikana kifahari?Tafsiri nyepesi ni kwamba wanafanya kazi wanawekeza pesa za nyakati za starehe na huzuni.Jambo ambalo mi naona wako Sawa.
Kipaumbele kiwe kuishi, kifo kipo tu, ni aibu kumzzika bibi au mama pale mndenyi kwa sherehe au bajeti ya milioni 20 wakati amekufa kwa njaa!
 
Watu wamefika mbali sana mtoa mada, siku hizi vikundi vinasaidiana kwenye maisha, kuugua na kuuguliwa, hawasubiri tena mtu afe ndio wajikombe.

Kama jamii yako bado inawekeza kwenye kuzikana tu pole sana, waambie wawekeze kwenye kuuguzana pia maana hakuna kazi ngumu kama kuwa na mgonjwa bila pesa.

Issues za kuwa na makampuni nk zinahitaji knowledge kidogo, watu watafika huko wala sio mbali, hata kusaidiana watoto kwenda shule watu wanafanya, familia zitafungua makampuni, viwanda nk ila ni sensitive kidogo, maarifa na elimu vinahitajika.
 
Siku akifa mkeo/mumeo au mtoto.
Huna hela ya kuutoa mwili Hospitalini, amefia mbali huna nauli ya kwenda kuuchukua mwili au kwenda kumzika.

Huna pesa za wachimba kaburi.
Hapo ndio utajua umuhimu wa hivyo vikundi.

Wazo lako la kusaidiana kiuchumi lilikuwa zuri pasipo kuponda wazo la michahgo ya misiba.

Au hujawahi kufiwa katika mazingira tata au hali ngumu?

Achana ni Kifo mzee.

Kama ingekuwa zamani ndugu wote mpo kijiji kimoja hapo sawa.
Lakini dunia ya leo.

Unasafiri kutoka Arusha unaelekea Dar. Unafika Segera unapata ajali unafariki.
Unafikiri mwili wako utasafirishwaje mpaka hospitalini bika gharama ya pesa? Utahifadhiwa bure hospitalini?

Unafikiri wapendwa wako watakubali uzikwe bila wao kuja kukuaga(kuaga mwili wako)
Hapo utakuwa umekufa kama kama waliopotezwa na wasiojulikana
 
Acha kabisa mkuu, nadhani watu hawajawahi kufiwa, hawajui kubeba mizigo ya misiba, hawajawahi kuuguza kwa miezi, hawajui relief inayopatikana ukiwa na kikundi cha watu wanaokupa support!!
 
Acha kabisa mkuu, nadhani watu hawajawahi kufiwa, hawajui kubeba mizigo ya misiba, hawajawahi kuuguza kwa miezi, hawajui relief inayopatikana ukiwa na kikundi cha watu wanaokupa support!!

Na mtu wa aina hiyo anajaribu kueleza aidha hana familia, mke, mume na watoto.
Hategemewi. Ila anawakubwa zake so anajua wapo watakaoshughulikia jambo hilo.

Msiba usikie tuu.
Picha linaanza amekufa mtu unayempenda. Dadeki
Pili, ni umeshtukizwa na mara nyingi matukio haya yanakuja kwa kushtukiza. Ndani huna hata pesa alafu mbele unamajukumu kibao ikiwemo kodi au Ada.

Aiseeh!
Alafu mpendwa wako aanze kuhangaishwa au kuletewa drama na kuwa habari za mji.
 
Ninakuunga mkono mleta mada. Upendo wa kweli kwenye familia lazima uwepo bila hata kuunda groups za watsapp. Kwani zamani watu walikuwa wanafanyaje bila watsapp? Sisi kwenye ukoo wetu hakuna group ila ukitokea msiba hadi aliyepo nje ya nchi atatuma mchango wake. Hivi vikundi ni show offs za kifala na kupotezeana muda. Mimi nimejitoa kwenye vikundi vyote vya watsapp ila likitokea jambo huwa nashiriki kikamilifu.
 
Kipaumbele kiwe kuishi, kifo kipo tu, ni aibu kumzzika bibi au mama pale mndenyi kwa sherehe au bajeti ya milioni 20 wakati amekufa kwa njaa!

Hivyo vikundi vya kuzikana vipo kwaajili ya waliohai.
Kuwasaidia waliohai kuzika wapendwa wao.

Siku ukifiwa utaelewa michango inatolewa kwaajili ya marehemu au kwaajili ya kusaidia waliofiwa
 
Suala hilo sioni tatizo , kwa vile msiba unakuja ghafla so kujiandaa ni muhimu ;kila mtu atakuja

Kuna hii tabia ya kifala ya michango ya harusi , kuna jamaa yaani anakusumbua kama demu vile , kuomba michango mpaka sasa kafikisha mil kama 16 , bajeti ya harusi ni mil 30 na ushee ila inafanyika mwezi Agosti mwishoni .Wanasumbua sana huo ufala .
 
Ninakuunga mkono mleta mada. Upendo wa kweli kwenye familia lazima uwepo bila hata kuunda groups za watsapp. Kwani zamani watu walikuwa wanafanyaje bila watsapp? Sisi kwenye ukoo wetu hakuna group ila ukitokea msiba hadi aliyepo nje ya nchi atatuma mchango wake. Hivi vikundi ni show offs za kifala na kupotezeana muda. Mimi nimejitoa kwenye vikundi vyote vya watsapp ila likitokea jambo huwa nashiriki kikamilifu.

Zamani watu waliunganishwa kwa damu na ukabila. Na kuishi sehemu moja.

Siku hizi koo zimekuwa kubwa. Fikiria koo zenye watu mpaka elfu 1000 bila teknolojia watawasiliana vipi?
Watajuaje nani anaumwa na nani amekufa.

Kwa koo ndogo ndugu wasiofika hata 20 hapo sawa.
 
Imeibuka tabia, wanafunzi waliosoma pamoja, watu walioishi mtaa mmoja, Koo moja na kabila kuanzisha vikundi vya Watsup na baadae kujisajili kuwa Rasmi.
Vikundi hivi huwa lazma kuwe na kisebengo ambaye atanzisha M-Koba na kutaka watu wachangieni iwapo mwenzao atapata msiba au ugonjwa wa kudumu.

niwape siri:KUFA TUTAKUFA TU, NDUGU WASIPO KUZIKA , HALMASHAURI ITAKUZIKA MANA HAKUNA ATAKAYE KUBALI KUKAA NA MZOGA, wenzetu wenye asili ya ASIa wanaunda group za fursa za biashara, kuwekeza UTT na Kufungua kampuni kugombea tenda, sisi tunawaza kuzikana tu.

Imekuwa ni ufahari kumzika mama yako, kumjazia maua rose ambayo kipindi cha uhai wake hukuwahi kumpa hata "ua mgomba" .
Mnweka Bufee, watu wale mpaka wasinzie, lakini uhai wake alikuwa anakula samaki na ugalli wa jero au anashindia chai!

Maziko ya mama yenu mnaleta vikundi vya ngonjera na sala na kupiga kila aina ya sifa ambayo kipindi akiwa hai hamkuwahi kufanya hivyo!

huu ni unafiki na ndio unaleta umaskini.

HITIMISHO:
Mtu yeyote, asiniunge magroup ya michango ya kuzikana, niunge kwenye group za kupeana biashara, viwanja, kazi na uwekezaji!
Kuna baadhi ya wanafunzi waliosoma pamoja shule za sekondari wamepiga hatua sana na wako mbali, kama wale wenzetu wa Mzumbe hawashikiki.

Hayo ndiyo mambo yetu sisi Wakristo tu! Wenzetu waislamu wamestaraabika sana, haya mambo ya kuzikana wala sio shida zao! Sijui sanduku la gharama, gari jeusi la kukodi la kisasa kubeba mwili wa maraehemu, Tshirt, madela au sare nyeupe! Hizo zote ni gharama tu zisizo na maana yoyote.
 
Waislamu kwenye suala la msiba wana taratibu nzuri kuliko dini zingine zote.
 
Back
Top Bottom