Hizi zenu ndio akili za kuwaza mali badala ya kuwaza uhai na thamani yake. Kama umewahi kuuguza huwezi kubeza michango kutoka kwa ndugu na marafiki, labda wewe ni toto la mwisho lisilojali welfare ya ndugu/wazazi.
Kuumwa siku hizi ni gharama sana, hata serikali haitoi tena huduma kwenye ugonjwa, ni malipo. Kuhudumia mgonjwa ni gharama sana, kama umewahi kufanya hivyo continuously hata mwezi tu utashuhudia.
Sasa imagine unahudumia mama yako yupo Muhimbili kwa zaidi ya mwezi, familia yako haijigusi kwa chochote so upo wewe na mkeo kila siku nenda rudi, unaishi Chanika, nauli tu sio mchezo. Huna hata mtu wa kukupa pole ya kuuguza, rudi tena useme sijui hela wanapiga mtu akifa.
Nimeishi hayo maisha, nimeuguza wazazi wangu wote, ninajua nilichopitia, kama sio mshikamano wa familia na vikundi kadhaa, lazima yakushinde na unaonekana umeshindwa kuhudumia mpendwa wako.
Hapo nimesemea kuuguza tu, habari ya msiba wala sijagusia. Nyie watoto msiojua majukumu it's hard for you to understand.